CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Yaani wew jamaa ni mnafiki mkubwa, unamtofautishaje jiwe na haya makando kando yanayoendelea? Ina maana unajifanya ufahamu aliyetugawa watanzania kufika hapa.
'mkurugenzi nimekuteua mim, nakulipa mshahara, posho, gari na nyumba alafu ole wako umtangaze mpinzani ameshinda'
 
Huyo anatii amri ya Jasusi Membe,

anasubiri maelekezo kutoka kwa mlezi wa chama
 
Na domo lake lile limepinda kama mkia wa pweza hovyo kabisa.
 
Kauli ya Raisi ni sheria, Raisi ndio mwajiri mkuu, haujui kauli ya Raisi imemfanya DPP hawasamehe makosa watuhumiwa wa Uhujumu Uchumi endapo wakikubali kutoa mzigo?
Kwa upande wa uchaguzi hauwezi kwenda kwa maelekezo kwa kuwa ni chombo huru kinachojitegemea.
 
Sasa, Mhe. Suleiman Jafo, anashangaa nini apo. Ni mwananchi gani anayenyimwa haki yake ya msingi baada ya CHADEMA kujitoa, ama ni nani katika ya watendaji na CHADEMA wanaowanyima wananchi haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wawatakao? Yani, kabisa Mhe anashangaa, kwamba haelewi bado uzito wa sababu za CHADEMA kujitoa katika uchaguzi. Nafikiri CHADEMA wametumia busara kubwa sana kujitoa, maana consequences za kuendelea kwao,zingekuwa kubwa na za gharama sana kwa watanzania.
 
Zitto atakuwa mjinga sana kama atatoa Chama chake katika uchaguzi maana haina faida kubwa kulko hasara zake.Wapinzani kwa viherehere vyao hadi walihamasisha watu kujiandikisha wakati zoezi liliposuasua sasa wananchi wamejiandikisha halafu mjitoe tena.Ni ujinga kama watafikiria kuisusia UCHAGUZI CCM ni kuikomoa maana toka waanze kususa haijawa msaada kwao.Zanzibar CUF na CHADRMA walisusia najua tunajua nini kilitokea.Njia bora ya kumsinda adui ni kupambana nae sio kumkimbia.
 
Hata Zitto akishiriki hapati kitu maana wananchi hawatashiriki atapigiwa kura na nani? Yaani hapo ndio Zitto na Act yake wanaenda kuumbuka kama ni mpinzani wa kweli au msakatonge mtu wa kitengo, safari hii Zitto atajianika mwenyewe.
 
Inatakiwa Zitto atoe chama chake kwenye huu uchafuzi unaoitwa uchaguzi kwa sababu ukishiriki wakati unajua kuna figisu na maagizo yapo wagombea wa upinzani wasitangazwe Washindi maana yake ni kuubariki uchaguzi haramu uonekane halali, Watanzania hawatamuelewa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…