CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Sioni mtu wa kuvaa viatu vya Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti ndani ya CDM.

Namna pekee ya CDM kuweza kurudisha nguvu ya upinzani kama waliyokuwa nayo awali ni kuungana na ACT wazalendo na kumkabidhi Zitto uenyekiti Mbowe kaishiwa maarifa ya kupambana na changamoto zinazowakabili upinzani.

Unaposusa ujisaidii bali unawasaidia wenzako maana sidhani kama wanufaika wanajali sana nyuma ya pazia kama wanavyosema kwenye media.

Kwenye siasa nchi za wenzetu watu wanaposusia uchaguzi ni kwa sababu wameazimia kuingia kukiwasha mtaani.

CDM Wakifanya ivyo kuingia mtaani hawata pata support ya watanzania ya kutosha na virungu juu ambavyo kama vile watakuwa wanastahili if you ask me.

Kilichobaki kwao ni kupambana kwa namna zingine za kisheria na kutoa pressure, something which their strategist are not good at maana mbinu wanayoijua ni maandamano tu nothing else ambayo kwa sasa ni ngumu kuipata.

Lakini kususa susa kila kitu ni ishara ya kuwa Mbowe na safu yake wameishiwa na aina faida kwa movement yao.
 
Mnalia lia toka 1995....
Watanzania tumewakataa upinzani huu wa kinafiki...

Ni kweli, ila kwenye uchaguzi huu tumedhibitishia nchi na dunia kuwa jiwe hana mvuto wa kisiasa. Miaka minne anafanya siasa yeye na chama chake, lakini watu wamegoma kujiandikisha, na sasa imebidi figisu itumike. Hawa watanzania mnawaowategemea wamewakubali mngeenda kwenye uchaguzi tuwaone.
 
Afadhali, INAKUBALIKA KAMA HUJAJIPANGA, UNA-RETREAT KISHA UNA-REGROUP.....
Hapa nimewapongeza chadema. Sasa mjipange vizuri, mkija hovyo 2020 WATANZANIA watawafyekelea mbali kwenye boks la kura.

Jiwe hawezi ushindani wa box la kura, hata alipokuwa mbunge alikuwa hashindi kwa uchaguzi. Ushahidi ni sasa kwenye uchaguzi huu, kwani wananchi wamewapa hizo kura?
 
Jiwe hawezi ushindani wa box la kura, hata alipokuwa mbunge alikuwa hashindi kwa uchaguzi. Ushahidi ni sasa kwenye uchaguzi huu, kwani wananchi wamewapa hizo kura?
Hizo ni hisia zako. Yeye ndio rais WAKO na wa Tanzania kwa mujibu wa katiba. Hivyo alishinda uchaguzi. Hutaki acha.
 
Basi kwa akili za Mbogamboga leo V8 zinachezea kodi zetu usiku kucha kuwatafuta akina MREMA wajifanye kushiriki uchaguzi,na yjle mvaa kofia jekundu kama mumiani,ana njaa sana yule,na hawa ndiyo wasaliti wa demockrasia.
 
Sioni mtu wa kuvaa viatu vya Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti ndani ya CDM.

Namna pekee ya CDM kuweza kurudisha nguvu ya upinzani kama waliyokuwa nayo awali ni kuungana na ACT wazalendo na kumkabidhi Zitto uenyekiti Mbowe kaishiwa maarifa ya kupambana na changamoto zinazowakabili upinzani.

Unaposusa ujisaidii bali unawasaidia wenzako maana sidhani kama wanifaika wanajali sana nyuma ya pazia kama wanavyosema kwenye media.

Kwenye siasa nchi za wenzetu watu wanaposusia uchaguzi ni kwa sababu wameazimia kuingia kukiwasha mtaani.

CDM Wakifanya ivyo kuingia mtaani hawata pata support ya watanzania ya kutosha na virungu juu ambavyo kama vile watakuwa wanastahili if you ask me.

Kilichobaki kwao ni kupambana kwa namna zingine za kisheria na kutoa pressure, something which their strategist are not good at maana mbinu wanayoijua ni maandamano tu nothing else ambayo kwa sasa ni ngumu kuipata.

Lakini kususa susa kila kitu ni ishara ya kuwa Mbowe na safu yake wameishiwa na aina faida kwa movement yao.

Huu utoto ulioandika hapa mpelekee mkweo ndio ana muda wa kusoma huu ujinga. Unasema asisusie huku zaidi ya 80% ya wagombea wake wametolewa kwa mizengwe? Unaingiza timu yako ya wachezaji 11 uwanjani, kisha refarii anawatoa wachezaji wako saba kwa uhuni wa kitoto, kisha unasema unaendelea na mechi!?
 
Hivi mtu kama Lowasa akija na mzigo Mh. Mbowe awezi badili gia angani kweli.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

----
WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.

Pia soma

Kwanza nieaoongeze sana chadema kwa maamuzi hayo magumu lakini pili jambo hili ni picha ya hatari sana kwa amani na muono wa democracia msichezee .
Nionavyo mimi watu wamechoka na kwasababu wamechoka watakavyoamua hata kama wachache wakafa kaaajili ya kutetea Amani na democracy yanchi tayari watakuwa wameshaichafua nchi.

Itoshe wazee wa busara
Mzee mkapa
Mzee mwinyi
Mzee kikwete
Mzee mangula
Mzee msekwa
Mzee butiku
Mzee warioba
Na wengine wengi watoke mafichoni waseme jambo hili.
Kumbuka wengi wanatamani amani ivunjike na hata miradi ijayo hataweza kutekelezeka.

Viongoz msikubali kamwe kuingizwa katika mtego ambao mnaweza kuuzuia.

Vyama vifuatavyo vyaweza kujiondoa
Ili kufuata chama kilichotangulia
Chadema
Act wazalendo
Cuf

Mwisho sio kila jambo linahitajika ubabe mengine ni diplomasia tu
 
Basi kwa akili za Mbogamboga leo V8 zinachezea kodi zetu usiku kucha kuwatafuta akina MREMA wajifanye kushiriki uchaguzi,na yjle mvaa kofia jekundu kama mumiani,ana njaa sana yule,na hawa ndiyo wasaliti wa demockrasia.

Mkuu wale washiriki tu, lakini mshindani halisi anafahamika. Tena hata wakiweza wasajili chama kipya kisha wawatangaze wagombea wao kushinda vitongoji kibao.
 
Nchi nyingine zilianza hivi hivi,Huyu jirani mshauri wetu anataka na sisi tupitie waliyopitia,I can smell bloodshed.
 
Screenshot_2019-11-07-21-43-01.png
 
Hamuwezi siasa za ushindani, na huo upuuzi kupandikiza jiwe ndani vya ccm. Na kwakuwa ccm ilikuwa imechoka kushindana imeona ni sawa huu uhayawani uendelee.
Hakuna jingine zaidi ya kuwa chadema ilikuwa inatafuta sababu za kutafuta mlango wa kutokea unafikiri bila ya kutumia hiyo trick pesa ya kulipia mawakala ungepatikana wapi ilihali chama hakina hata kumi!
 
Back
Top Bottom