Kuna Waziri mmoja anaitwa "JAFO", bila aibu wala kupepesa macho leo anasema eti kususia uchaguzi ni kuwanyima raia haki yao.
Hivi inaingia akilini kweli "CCM" wamejipitisha nchi nzima bila kupingwa, wamewakata wagombea wa upinzani wote, na kama mgombea akipitishwa bila kupingwa maana yake hakutakua na uchaguzi wowote wa mitaa.
Swali kwa Jafo,
Hao wapinzani wanawanyima haki gani raia??? Au ni serikali kwa mabavu ndio wamewanyima haki raia ya kuchagua wagombea wanaowafaa na kuwachagulia viongozi kwa nguvu???
Wasifanye watanzania wapumbavu. Ama kweli tanzania hatuna mawaziri wala serikali. Aibu hii dunia nzima.
#CCM subirini wananchi wenye hasira kali #2020.