CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Kinachonishangaza ni kuwa ccm wamesikitika uamuzi wa Chadema kujitoa,,, ina maana ccm hamfurahii ushindi huu wa kishindo mmeoupata?
 
Kinachonishangaza ni kuwa ccm wamesikitika uamuzi wa Chadema kujitoa,,, ina maana ccm hamfurahii ushindi huu wa kishindo mmeoupata?
Hela ya uchaguzi wanakosa, kupiga hela hakuna tena, anakula jiwe na mwanawe.
 
Haya maamuzi sahihi ila yamechelewa sana,sijui hata mlipopanga kushiriki mlikuwa mnafikiria nini.

Huwezi kufanya siasa na mtu asiyetayari kushindwa.

Wasingevuta subira, nina hakika ungepinga pia, au wengine wangepinga. Hata mimi ningejiunga katika kundi hilo kama wangejitoa mapema.
Baada ya wagombea wao kukataliwa, wamepata sababu ya kujitoa ambayo hata wewe nina hakika unaiona ipo wazi kabisa, au sio?
 
Tangu lini umekuwa msemaji wa chadema

Tusiwatambua tutapata utambuzi wa serkali za mtaa kwenye ofisi za mbowe acheni upumbavu wajinga nyie

Waacheni wananchi wapate hudumu

State agent
Sasa Kazi ndio imeanza rasmi
 
inawezekana vipi usimtambue mtu unayehitaji muhuli wake kila mara?
Nani atakusikia bank kwamba humtambui mwenyekiti wako?
Nadhani hii ni sehemu nzuri sana ya kuanzia harakati za ukombozi.

Huyo mwenyekiti wananchi wengi wa eneo lake hawawezi kumkataa? Yeye atakuwepo tu kuongoza hata kama watu hawatambui uongozi wake?

Uongozi hauishii kwenye kushika mihuri tu, yapo mambo mengi yanayohitaji ushiriki wa watu unaowaongoza. Kama hao watu hawakupi ushirikiano, utawaongoza vipi?

Au sasa hadi mahabusu yatahamishiwa hadi huko mitaani? Na bunduki zipo huko?

Mijadala ya JF ingekuwa na nguvu, hili ni swali zuri la kulijadili.

CHADEMA wakiwa makini, wasiishie tu katika kususia uchaguzi. Huu ndio ungekuwa mwanzo wa kuangalia njia zinazofaa kuwa'undermine' hawa watu wanaoteuliwa kuongoza watu ambao hawakuwachagua kwa utashi wao.
 
Mihuri ipo hata leo hii hata kabla ya uchaguzi kufanyika , mihuri ni mali ya umma , kutumia mhuri haimaanishi kumtambua Shetani .
Eeenh, Erythro, kweli mmeshikwa babaya safari hii kiasi kwamba nguvu zinaisha.
Ukiishia kukubali 'mihuri' lakini mwenye 'mihuri' humtambui, na ukaishia hapo; hiyo itakusaidia nini?

Ningekuelewa vizuri sana kama ungesema 'mihuri' utakwenda kuitumia, hata kama ingekuwa imeshikiliwa na shetani ili ukidhi mahitaji ya lazima kwenye maisha yako, lakini hapo hapo unafanya kila njia ya kumshinda, kumwondoshea mbali huyo shetani.

Huu ni wakati mzuri kwa CHADEMA kwenda huko mitaani kufanya kazi na wananchi wanaoporwa haki zao za kuwachagua viongozi wao. Acheni mengine yote, jikiteni huko huko mitaani kuwasihi wananchi watuondolee hili zimwi lililovamia nchi yetu. Hata CCM waliobakiwa na akili kidogo watawaunga mkono mkiwaelewesha vizuri hatari inayotukabili kutokana na matendo ya utawala huu.
 
Mbowe wewe ni kiongozi wa chama cha siasa.
Lengo kuu la chama chochote ni kushika dola.

Unatakiwa kutambua kususia uchaguzi maana yake ni kuwadhulumu wananchi.
Sio kila mtaa majina yamekatwa, sasa madudu mliyofanya huko kwenu Hai unataka tuumie na tusiousika.

Hiki chama sio cha viongozi, maana ya maamuzi yenu ni kuua chama, serikali inaanzia mtaani, kama mnaona hamtendewi haki mbona ubunge mnaendelea?

Mbowe ni jipu litumbuliwe.
 
Back
Top Bottom