Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Unaendeleza ukoo ili iweje?
Nani amekupa majukumu ya kuendeleza ukoo?
Ukoo usipoendelea kuna tatizo gani??

1. Ukoo unaendelea ili kuendeleza Bloodline, undugu, ujamaa, mila na desturi za watu. Kila mtu ana kwao, kila mtu ana chanzo. Hakuna mtu anaanguka tuu kutoka mbinguni.
2. Nature ndio inayoendeleza ukoo, umezaliwa na jinsia gani. Kelele iliyopo hapa ni juu ya jinsia ya mtoto, mtoa mada anaona wazi anakwenda kupoteza ukoo wake. Anakwenda kuzaa kwa ukoo wa mtu mwingine na kuundeleza kwa kuzaa kwake. Mwanamke hana jina, na hana ukoo kiasili wala dini. Atakapoolewa ndipo kutakuwa ukoo wake, atapewa jina huko na atakuwa wa huko. Ndio maana leo unasikia mtu anaitwa Asharose Migiro, Salma Kikwete, Magreth Sitta, Hillary Clinton, Michelle Obama, Margaret Kenyatta. Janetg Museveni, Rachel Ruto. Wale wamekuja kwenye koo hizo kwa kuhama, koo zao (surnames) ziliishia pale walipoolewa. 😁
3. Ukoo usipoendelea maana yake kizazi hicho kimepotea.
 
Kisayansi anayeamua jinsia ya mtoto ni mbegu za baba
Hata ukitoka nje usishangae unapata tena wa kike

Ni Bora ukaenda hospitali au ukafuata kale da labda unaweza kufanikiwa
All in all mtoto ni mtoto wape elimu nzuri hao mabinti huku ukimshirikisha Mungu ile wakulee vizuri ktk uzee wako
 

Sio kumdogosha mtoto wa kike, mtoto wa kike kweli ni dhaifu.
 
Kwani ushajijua kama utafika uzeeni kabla hujafa na unavowaza kwenda kuzaa nje uko ushaongea na Mungu kwamba atakupatia uyo wa kiume
 

Haya ni maneno tuu ya kupeana moyo. Kwa ndani unatamani ungepata dume hapo home. 😊
Siku ukipata mtoto wa kiume utafutahi kwa asili, wala sio kwamba utalazimika, ila utajikuta unafurahi pasipo kifani. Siku mkeo akikupigia simu kutoka chumba cha kujifungua kwamba ni wa kiume, kuna vibe waga linakuja kwa asili kabisa. 😊
 
Watu wanaweza kukubeza kwamba uridhike na ulichopata ila upo sahihi.

Ngoja nimwambie Atoto tutafute kidume.
Halafu ujue kuna fursa hapa kwa mtoa mada. Ngoja niichangamkie.
πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
 
Unaweza usizeeke ukafa kwa ajili,
Halafu pia unamaanisha ukizeeka mtoto wako wa kiume ndiye atakuwa mtu wa kukuuguza kwa maana ya kukulisha, kukuogesha na kukutawaza au kukulipia gharama za huduma za kukuuguza manesi wafanye hizo kazi?

Mke wako akizeeka yeye atauguzwa na nani??
 
Masikini makupuku wa Africa wasio na chochote cha maana hasa maeneo ya bara ndio zaidi wana mawazo ya aina hii.
 
Unamaanisha ukoo au jina lako binafsi?? Haiwezekani ukoo wenu ukaisha kwa sababu ya wewe mtu mmoja kutokuwa na mtoto wa kiume. Koo za Obama, Bush Jr au Putin haziwezi kuisha kwa sababu ya wao kutokuwa na watoto wa kiume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…