#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
How much does Big Pharma lobbying cost?

Leading lobbying industries in the U.S. 2020

In 2020, the pharmaceuticals and health products industry in the United States spent the most on lobbying efforts, totaling to about 306.23 million U.S. dollars.4 Mar 2021
Hehehehe,
Mzee unahangaika na tafiti za Ulaya hapa Bongo kuna Makampuni ya madawa kila mwaka lazima yasafirishe madaktari ulaya na Marekani kwa tour na kila mwezi bahasha hutembea.

Ni wachache tunaujua huu mchezo ni kitu cha kawaida sana kwenye Pharma Industry,

Kwenye Pharma Industry figisu ni nyingi sana ukimbwela you are out,

Daktari hawezi kuandikia Mgonjwa wake prescription ya brand yako kiboya tu, wewe umekuwa nani, mama yake? [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Gwajima aliuliza
"Kwa nini takwimu za idadi ya wagonjwa wa magonjwa mengine kama malaria hazitolewi?

Ukipata chanjo hutaambukizwa, hutaambukiza wala kuugua corona? Kama jibu ni hapana, kwa nini mtu apate chanjo hiyo ya corona?"
 
Hahaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] acha nicheke tu maana kuna mijitu humu kila siku sukuma gang sijui nn !!Ila yule mwamba mtamkumbuka sana siko kikabila ila wasukuma tumejaribu kuweka kumbukumbu ya uongozi bora na usio chekea wapuuuzi.
 
Hzo chanjo zote zilipita hatua mbalimbali kuanzia na majaribio mbalimbali mpk kufikia matumizi ambapo si chini ya miaka 5-10...

Watalaam wanasema zinatoka guarantee ya 70% na zipo ambazo zinakwenda mpaka 90%... chanjo hii imeruhusiwa kutumika maana dunia nzima iko kwenye dharura na watu wanakufa hivyo WHO waliruhusu zianze kutumika ila study ziendelee ipatikane yenye uwezo wa 100%.

Tafsiri ya WHO ni kuinusuru dunia ambayo watu walikuwa wanakufa hovyo hivyo isingekuwa busara kusubiri 5-10 yrs wakati wapo watu wamedevelop chanjo zenye uwezo wa 70% to 90%.

Duniani Kote CHANJO NI HIARI, kama unataka unadunga kama hutaki unaacha....ijapokuwa tunakoendea mbele inaweza kuwa lazima automatically tu.

Serikali ya Samia imeleta chanjo na kuifanya hiari ili kukidhi haja za watanzania wenye uhitaji wa chanjo ndio maana ikawa HIARI sio Lazima uchanjwe ila wapo watanzania wengi wanauhitaji.
 
Walipinga vyandarua hao kipindi kile USA imetoa msaada maswali ya kitura yalikua mengi mno leo nyumba zina vyandarua bila kuzungumzia tena kuwa zinaleta ugumba...Elimu ya mzungu haiwasaidii bora wasingesoma kabisaa..
 
Gwajima aliuliza
"Kwa nini takwimu za idadi ya wagonjwa wa magonjwa mengine kama malaria hazitolewi?

Ukipata chanjo hutaambukizwa, hutaambukiza wala kuugua corona? Kama jibu ni hapana, kwa nini mtu apate chanjo hiyo ya corona?"

Corona ni Pandemic hayo mengine sio pandemic....ndio maana hata ebora ikizuka basi takwimu hupaswa kutolewa kila siku.... Lakini pia takwimu za malaria na HIV hutolewa na kuwekwa kwenye data base.

Kumbuka pia malaria inatibiki na sehemu nyingine duniani wameidhibiti haipo....Corona ni pandemic disease na ni ugonjwa mpya unaoua watu wengi kwa haraka lazima kuwe na tahadhari za haraka.

Chanjo hizi zote zinatoa guarantee ya 70% to 90% kwenye kuukinga mwili ndio maana unashauriwa bado uchukue tahadhari maana haina guarantee ya 100% japo wapo pia zinazowakinga.
 
KWANINI CHANJO YA KORONA IMELETWA

Kama kuchanja ni hiyari, na Mh. Rais ameamua kupigia debe chanjo, basi ni haki pia kwa wale ambao hawaungi mkono chanjo nao kupigia debe upande wao...
Nimeangalia bandiko lako refu, nilichokiona ni kumsifu Magufuli maana ulikuwa na mahaba niue naye. Halafu ukamalizia kwa kuitaja cdm Katika namna hasi, kama wanaccm wengi wafanyavyo hapa jukwaani kwenye mabandiko yao. Huyo Magu unayemsifia hakuwa na lolote zaidi ya kuwa ni mtu anayeamini ushirikina, na kwa kuwa alikuwa na ulevi wa madaraka, basi akawa analazimisha wote tuwe na imani za kishirikina kama yeye.

Hao cdm uliowataja kuhusu demokrasia, tatizo sio demokrasia wafanyayo cdm, bali ni hofu waliyonayo ccm dhidi ya Cdm kwani ccm tayari imeshapoteza mvuto kwa umma.

Sasa kwakuwa cdm imeonyesha kuwa na mvuto kwa umma, jambo hili linaiumiza ccm iliyopoteza mvuto ndio matumizi ya nguvu yanapooanzia.

Kama uwepo wa cdm na aina ya demokrasia wanayoitaka ni kikwazo cha hayo maendeleo, tueleze maendeleo yaliyokuwepo kabla ya hiyo cdm kuwepo.
 
Wewe askofu gwajima sio mtu mdogo ana marafiki wakubwa maaskofu marekani,uingereza urusi,canada,denimak nk amabao ni madokita na wenye fani zaidi ya uchungaji
 
Mkishaanza kuchanganya siasa na sayansi mnaharibu. Kama hizi chanjo siyo nzuri kwetu, toeni sababu za kisayansi na siyo za kisiasa za kwa nini watu wasichanjwe. Kama ni side effects za chanjo, kila dawa ina side effects. Kama chanjo hazifanyi kazi, leteni takwimu zake tuzisome.
Taarifa za kisayansi na vyombo vya habari vinasema ukichanjwa unaweza kuambukizwa au kuambukiza Corona, pia unaweza kufa, ina maana inapunguza tu. Na kama ndivyo inapishana vipi na kujipiga nyungu?
 
Thanks brother naona unajibu kwa hoja maridhawa, tofauti na wale jamaa zangu.
Hiyo ni hoja ya kusema kwamba kama zamani ilikuwa safi basi na leo itakuwa safi. Yaani ni hoja ya kuuza akili yako na kuweka imani 100% kwa mtu baki...
Bado nawazoom jamaa zangu wa ANAUPIGA MWINGI.
 
Mwanafalsafa upo bado katika dunia hii? Ulipotea sana!

Sisi wengine tunaungalia huu mchezo kwa mbaliiiiii mpaka mwisho wake!
🤣👇
images (85).jpeg
 
Hoja za Rais zinatokana na matokeo ya study na majaribio ya kitaalamu yaliyofanywa kuhusu chanjo husika!!!

Sasa wewe unataka Wahuni kama akina Gwajima nao waachwe waendelee kuwajaza watu ujinga kwa kuzingatia study zipi alizofanya?...
Waliofanya study una waamini?

Kama hazina madhala kwa nini hawataki kuji commit ili chancho ikileta madhala wawajibike?

Ina maana study yao bado haina mashiko na ndio maana wanakwepa.

Sasa subili baada ya miaka utaona unaanza kuota matiti ndo utajua.
 
Haya mambo mnaona ni maigizo kisa hamjaona mtu wenu wa karibu kayapata au nyie amjayapata ndio maana mnajidai kuongea hizi pumba ...huu ugonjwa mmbaya jaman na sio lazima ukupate ww ndio uone mazara shukuru mungu kakuepusheni amjapata .
 
Hiyo ni hoja ya kusema kwamba kama zamani ilikuwa safi basi na leo itakuwa safi. Yaani ni hoja ya kuuza akili yako na kuweka imani 100% kwa mtu baki.
Hoja ni kwamba, usalama na effectiveness yake imethibitishwa na Watalaamu! Gwajima yeye ana utaalamu wowote?! Ana timu ya wataalamu waliomwelekeza huo msimamo wake?
Ngoja nikufunue kichwa ili usiendelee kulala kwenye mambo ya zamani.
I doubt kama una cha kunifafanulia hapa...
Chanjo ya Polio ndo inaleta Polio Afrika.

Haya sio maneno yangu bali ni maneno ya WHO wenyewe. Wameandika kwenye ukurasa wao hapa, aya ya sabab kutoka juu kuwa:

--- nukuu ----

Today, the fight continues against all forms of poliovirus. A rare vaccine-derived version of the poliovirus is affecting African countries with low immunization coverage, particularly among remote communities and those experiencing migration or conflict. Renewed efforts are underway to rid Africa of all remaining vaccine-derived polioviruses.
Hivi huoni aibu?!

NIna uhakika umeelewa kilichomaanishwa hapo juu ni nini hasa, lakini bila aibu unataka kujaribu kupotosha...

Yaani una-highlight " vaccine-derived version of the poliovirus " lakini kwa makusudi unaacha neno RARE!!!!

Kila anayetumia akili yake sawasawa anafahamu majority if not all of the medical solutions zinaacha side effects!!

Na kama kweli hujui ulichoandika mwenyewe, wanachosema WHO ni uwezekano wa kupata a rare vaccines derived version of the poliovirus baada ya kuwa umepata chanjo....

Lakini kama ilivyo side effects zingine, such rare derived version of poliovirus zinatokea kwenye maeneo yenye watu wenye kinga dhaifu!!!

Na kama ungetumia dakika moja tu ya ziada kufahamu hiyo Vaccine-Derived Polio Virus ni nini hasa; ungekutana na haya maelezo kutoka CDC.
A vaccine-derived poliovirus (VDPV) is a strain of the weakened poliovirus that was initially included in oral polio vaccine (OPV) and that has changed over time and behaves more like the wild or naturally occurring virus. This means it can be spread more easily to people who are unvaccinated against polio and who come in contact with the stool or respiratory secretions, such as from a sneeze, of an infected person. These viruses may cause illness, including paralysis.
Kisha wanaendelea...
VDPVs can cause outbreaks in countries where vaccine coverage is low. Long-term excretion can also occur in people with certain immunodeficiency disorders.

Kumbe basi, hiyo polio yenyewe unayoisema ina uwezekano mkubnwa wa kutokea kwenye jamii zenye watu aina yenu!! Watu wanaojaribu kupingana na science bila kutumia sayansi!

Now tell me: Kama wewe ndie mwenye mamlaka kwenye nchi, unaweza kuzuia chanjo ya polio kwa sababu inasababisha "A rare vaccine-derived version of the poliovirus"?
--- mwisho wa nukuu ---

Sasa unapoonza maneno kama hayo ni kwamba wamejaribu kudogosha ishu ili wale waliolala muendelee kulala.

Na pili unaijua historia haswa ya chanjo ya polio ilivyopatikana?
Hayo maelezo yako hayana mashiko kutokana na ushahidi niliokuwekea hapo juu!!

Unafahamu kuwa chanjo ya polio ndo ilitengeneza virusi vya HIV?

Hiyo historia ipo katika kitabu kinaitwa, "The River : A Journey Back to the Source of HIV and AIDS" (kiko Amazon)

Hicho kitabu sijakisoma... Je, unaweza kuweka scientific evidence iliyotajwa kwenye hicho kitabu na ku-conclude kwamba HIV imesababishwa na Chanjo ya Polio?

Hata hivyo, nimesoma review ya hicho kitabu kupitia US Library of Medicine, na wanapozungumzia polio wanasema:-
The hypothesis of this book is that the drive to conquer another scourge, polio, is the crux. The preparation of live attenuated oral polio vaccine originally used cultures of monkey kidney cells; there were monkey laboratories in Africa devoted to testing these vaccines and providing kidneys for the vaccine factories; the kidney cells (or associated lymphocytes) could have been infected by SIVs that could adapt to humans and cause disease (which they do not in their natural hosts); then administration of oral polio vaccine infected adults and children with SIV during the mass trials in the late 1950s.
Kwanza, kumbe ni hypothesis, na sio findings! Sitaki kuamini kwamba hujui what's hypothesis!

Na hypothesis yenyewe ni kwamba, so long as polio vaccines ilitumia cultures of monkey kidney cells, basi inawezekana figo za nyani zilipata maambukizi! Na kwavile inawezekana figo zilipata maambukizi ya SIV, na kwavile inafahamika HIV imetokea kwa nyani, basi inawezekana hao nyani walikuwa na hayo maambukizi yaliyosababisha HIV kutokana na chanjo ya polio!

Narudia... hiyo ni HYPOTHESIS!!!

Hypothesis must be concluded with scientific or research findings! Kwa wasiofahamu what's hypothesis in research ni kwamba!

The question is: Is the hypothesis supported with scientific findings?! Intro inaendelea...
The idea is not new, having been proposed in 1992 (and rubbished or deflected by the scientific community).

Kumbe, hiyo idea, iliyozua hypothesis imetupwa kapuni na WANASAYANSI! Imetupwa kapuni kwa sababu haina scientific evidence, lakini wewe unataka kuileta hapa as scientific argument!!!

Hiyo review hapo juu imeandikwa na Professor Sebastian Lucas, Department of Histopathology! Vipi kuhusu Edward Hoper alieandika hicho kitabu unachojaribu kutolea conclusion?
Edward Hooper has worked as a United Nations official and BBC correspondent in Africa.
Kumbe ni Mwandishi wa Habari!!!!
Utafiti huo ukapeleka kutengenezwa kwa kirusi cha HIV. Majaribio ya chanjo ya polio waliyafanya mwaka 1957 kwa wakongomani na wanyarwanda-urundi. Na kwa kule Marekani waliwafanyia watu wasiowapenda (mashoga) na watu ambao hawana ndugu wa kuwalilia (yatima 20 kwenye kituo kimoja cha kulelea yatima jijini NYC).

Mwaka 1959 kesi ya kwanza ya HIV ikaibuka Kinshasa. Huku Tanzania kama unakumbuka ugonjwa uliingilia Kagera kwa wahaya kutokana na ukaribu wao na Rwanda-Urundi.

Dr. Remmy anatokea eneo la Mashariki ya Kongo ambako ndo maabara ilikuwepo kwenye mji wa Kisangani (enzi hizo ukiitwa Stanleyville). Aliujua UKIMWI mapema sana kutokana na ndugu zake na watu kadhaa anaowajua kufariki huko Kongo. Ndo alikuwa mwanamuziki wa kwanza kuimba kuhusu UKIMWI kwenye wimbo wake wa "Mambo kwa soksi"

Ila alikuwa mbele ya wakati, maana huku Bongo UKIMWI ulikuwa bado haujashika chati. Wimbo wake huo ulifungiwa na BASATA kwamba ni matusi. (Soksi alikuwa anamaanisha ni kondomu. Sasa enzi hizo za Nyerere bado yuko hai, kuongelea kondomu ilikuwa ni ishu nyeti sana).

Na kwa Marekani kama unaijua historia ya UKIMWI kule ulipoingia ulikuwa unaitwa ugonjwa wa mashoga.

Kwa hiyo mdau kuna mengi sana nyuma ya pazia. Haya ni machache yanayojulikana. Mengi yanafichwa.
Maelezo yako hayana maana yoyote kwa sababu unajadili sayansi kwa kutumia arugments ambazo hazina scientific evidence!!
Ukiona kichwa kama Magufuli anakupa warning ujue kuna vitu ameshaviona.
Ndo tatizo lenu hili...
Sasa ni uzembe sana wa akili kuwaza kwamba "Kama zamani tumefanya basi tuendelee kufanya"

Nyerere angekuwa na akili hiyo unadhani angedai Uhuru? Maana kama amezaliwa ameukuta ukoloni sasa anadai uhuru wa nini?
Kama hadi hapo bado hujajua ni yupi kati yetu mwenye uzembe wa akili, then I must sincerly say "Una safari ndefu sana"!!
 
Waliofanya study una waamini?
Kwahiyo unataka niwaamini ambao hawajafanya study yoyote sio?
Kama hazina madhala kwa nini hawataki kuji commit ili chancho ikileta madhala wawajibike?
Ina maana study yao bado haina mashiko na ndio maana wanakwepa.
Sasa subili baada ya miaka utaona unaanza kuota matiti ndo utajua.
Kila medical solution ina side effects! Kinachoangaliwa ni mizania inaegemea wapi!

Una lingine?
 
KWANINI CHANJO YA KORONA IMELETWA

Kama kuchanja ni hiyari, na Mh. Rais ameamua kupigia debe chanjo, basi ni haki pia kwa wale ambao hawaungi mkono chanjo nao kupigia debe upande wao.

Sioni sababu ya wanaopinga chanjo kama Mh. Gwajima kutolewa kauli za vitisho na baadhi ya wana-CCM. Ndo maana ya hiyari hiyo. Hiyari ina pande mbili.

Sababu kuu haswa ya kuletwa chanjo nchini Tanzania ni kwa sababu Magufuli hayupo. Angekuwepo zisingekanyaga hapa. Kifo cha Magufuli kitatugharimu sana waTanzania.

Sababu ya pili ni ikumbukwe kwamba maudhui ya kuleta chanjo ilikuwa ni kuwasaidia mahujaji na waTanzania wengine wanaotaka kusafiri kwenda kwenye nchi ambazo zinahitaji chanjo. Lakini hata waSaudi wenyewe ni kwamba hawana imani na chanjo; na ndo maana wameamua kupiga marufuku mahujaji wa kutoka nje ya nchi yao.

Kwa mfano tuna chanjo ya homa ya manjano hapa Tanzania, lakini hakuna mtu anayehangaika nayo isipokuwa tu kama unataka kusafiri kwenda kwenye nchi ambayo wanataka uwe umechanjwa ndo wakupokee. Na hata hiyo chanjo yenyewe ya homa ya manjano kuchanja ni hiyari. Unaweza ukailipia tu na kupewa kadi kuwa umechanja ili usisumbuliwe huko uendako.

Sababu ya tatu ni ubeberu. Mh. Rais tuliona aliwapigia simu mabeberu wa EU siku ile akawaweka na loudspeaker. Kwa kuwa amejipendekeza mwenyewe kwenye anga zao ni lazima wampelekeshe wanavyotaka wao. Mabeberu siku zote hawapendi kuona fikra huru ya Mwafrika. Hawakufuruhishwa kabisaaaa na msimamo tofauti na ambao ulikuwa unaonesha matokeo chanya wa Magufuli. Matokeo chanya kwa maana ya kwamba waTanzania tumeishi kwa uhuru bila matatizo yoyote wakati wao mabeberu wakifungia ndani kama kuku.

Kwa wale wenye uzoefu naamini mtakubaliana nami kwamba Mzungu hata siku moja hayuko tayari kupokea wazo jipya na tofauti na anachojua yeye kutoka kwa ngozi nyeusi. Duniani huko watu wanatudharau ngozi nyeusi kwa kiasi kikubwa. Hilo sio tatizo. Tatizo ni pale sisi wa ngozi nyeusi tunapoanza kujidharau wenyewe. Hilo ni tatizo kubwa sana ambalo linawatafuna waAfrika wengi sana.

Leo hii mTanzania ukimwambia aachane na Ukristo au Uislam kwa kuwa sio falsafa za kiAfrika mtazozana sana.

Sasa kwa kujidharau huku leo hii tunaona serikali ikiwa imekamatwa akili na mabeberu, inaanza kufuata miongozo yao na kuagiza chanjo. Kwa hiyo sababu ya tatu ni hiyo ya ubeberu. Mabeberu walikuwa wanapambana kuhakikisha kuwa mwafrika anaendelea kuwa kwenye usingizi na kuwa kwenye himaya yao kifikra. Mwafrika kama Magufuli aliyezinduka dunia nzima kwa fikra tofauti alikuwa ni tishio kubwa kwa ubeberu.

Sasa kinachotia wasiwasi ni kauli kama ile ya kusema "Tutachanja 60%".

Ila tukirejea kwenye sababu ya pili, ni kwamba Mh. Rais ameonesha kwamba ni mpenzi wa safari za nje ya nchi. Kwa yeye kuchanja inawezekana kuwa ni lazima, maana hatujui atakwenda nchi gani safari zijazo.

Na Mh. Rais akishakuwa ni msafiri, viongozi wengine nao kama mawaziri, wakurugenzi, n.k. nao wataanza tu kusafiri.

Sasa kuyatambua mambo kama haya ndo msingi wa kujua ni tatizo gani haswa wanalojaribu kutatua kwa kupitia hizi chanjo. Sio unafuata mkumbo tu, wakati wewe maisha yako ni ya hapahapa Bongo.

Ingekuwa chanjo zimeletwa kwa ajili ya kupambana na "korona" basi zisingekuwa hiyari. Hatua zingine zinazoletwagwa kwa ajili ya kupambana na "korona" huwa si za hiyari (kama vile amri za kuvaa barakoa kwenye majengo na mabasi).

Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema kuwa kama wewe ni Mwafrika unayeamini kwamba kichwa chako kina akili, na unaweza kufikiri, kwamba hauna haja ya kutegemea fikra za Mzungu, basi usimsahau huyu kiongozi wetu aliyetutoka. Uthubutu alioonesha na jinsi alivyokataa kabisa kushikwa akili na wazungu katika masuala fulani muhimu (madini na korona) ni jambo moja la muhimu sana katika ukombozi wa Mwafrika, ambayo bado ni safari ndefu sana. Kila kizazi kina jukumu la kusukuma gurudumu.

View attachment 1870885

Na kwa CHADEMA mliokuwa mnamlalamikia sijui mambo ya demokrasia naamini sasa hivi mmeshamuelewa kama kweli mna akili za kikubwa. Ni kwamba alikuwa anayajua matatizo yake ya moyo na kwamba alijua anakufa saa yoyote ndo maana alijitahidi sana kupeleka mambo kwa kasi atimize kabla hajafa.

Haya mambo ya kutaka kupigapiga siasa kila saa (zile Operesheni Operesheni mlizokuwa mnazipenda) hayana tija yoyote kwa mustakabali wa taifa. Naamini mnaendeshwa kwa falsafa za kiMarekani. Sasa Marekani hawajaendelea kwa sababu ya demokrasia, basi wameleta demokrasia baada ya kuendelea. Na kama mnavyoona demokrasia yao ni upuuzi mtupu, hakuna kinachofanyika kule wanazozana tu kila siku.
This qualifies as food for thought 👏!
 
Hoja ni kwamba, usalama na effectiveness yake imethibitishwa na Watalaamu! Gwajima yeye ana utaalamu wowote?! Ana timu ya wataalamu waliomwelekeza huo msimamo wake?

I doubt kama una cha kunifafanulia hapa...

Hivi huoni aibu?!

NIna uhakika umeelewa kilichomaanishwa hapo juu ni nini hasa, lakini bila aibu unataka kujaribu kupotosha...

Yaani una-highlight " vaccine-derived version of the poliovirus " lakini kwa makusudi unaacha neno RARE!!!!

Kila anayetumia akili yake sawasawa anafahamu majority if not all of the medical solutions zinaacha side effects!!

Na kama kweli hujui ulichoandika mwenyewe, wanachosema WHO ni uwezekano wa kupata a rare vaccines derived version of the poliovirus baada ya kuwa umepata chanjo....

Lakini kama ilivyo side effects zingine, such rare derived version of poliovirus zinatokea kwenye maeneo yenye watu wenye kinga dhaifu!!!

Na kama ungetumia dakika moja tu ya ziada kufahamu hiyo Vaccine-Derived Polio Virus ni nini hasa; ungekutana na haya maelezo kutoka CDC.

Kisha wanaendelea...


Kumbe basi, hiyo polio yenyewe unayoisema ina uwezekano mkubnwa wa kutokea kwenye jamii zenye watu aina yenu!! Watu wanaojaribu kupingana na science bila kutumia sayansi!

Now tell me: Kama wewe ndie mwenye mamlaka kwenye nchi, unaweza kuzuia chanjo ya polio kwa sababu inasababisha "A rare vaccine-derived version of the poliovirus"?

Hayo maelezo yako hayana mashiko kutokana na ushahidi niliokuwekea hapo juu!!



Hicho kitabu sijakisoma... Je, unaweza kuweka scientific evidence iliyotajwa kwenye hicho kitabu na ku-conclude kwamba HIV imesababishwa na Chanjo ya Polio?

Hata hivyo, nimesoma review ya hicho kitabu kupitia US Library of Medicine, na wanapozungumzia polio wanasema:-

Kwanza, kumbe ni hypothesis, na sio findings! Sitaki kuamini kwamba hujui what's hypothesis!

Na hypothesis yenyewe ni kwamba, so long as polio vaccines ilitumia cultures of monkey kidney cells, basi inawezekana figo za nyani zilipata maambukizi! Na kwavile inawezekana figo zilipata maambukizi ya SIV, na kwavile inafahamika HIV imetokea kwa nyani, basi inawezekana hao nyani walikuwa na hayo maambukizi yaliyosababisha HIV kutokana na chanjo ya polio!

Narudia... hiyo ni HYPOTHESIS!!!

Hypothesis must be concluded with scientific or research findings! Kwa wasiofahamu what's hypothesis in research ni kwamba!

The question is: Is the hypothesis supported with scientific findings?! Intro inaendelea...


Kumbe, hiyo idea, iliyozua hypothesis imetupwa kapuni na WANASAYANSI! Imetupwa kapuni kwa sababu haina scientific evidence, lakini wewe unataka kuileta hapa as scientific argument!!!

Hiyo review hapo juu imeandikwa na Professor Sebastian Lucas, Department of Histopathology! Vipi kuhusu Edward Hoper alieandika hicho kitabu unachojaribu kutolea conclusion?

Kumbe ni Mwandishi wa Habari!!!!

Maelezo yako hayana maana yoyote kwa sababu unajadili sayansi kwa kutumia arugments ambazo hazina scientific evidence!!

Ndo tatizo lenu hili...

Kama hadi hapo bado hujajua ni yupi kati yetu mwenye uzembe wa akili, then I must sincerly say "Una safari ndefu sana"!!
Acha kujimwambafai kwa kukariri mambo usiyokuwa na uhakika nayo ndugu! Hayo yote ma citations yameandikwa na watu ambao hata hujui 'intentions' zao nyuma ya pazia! Hujui kama kilichoandikwa kilitengenezwa au ndio ukweli halisi! Ungeweza kujimwambafai kama ww mwenyewe ulishiriki na kuhakikisha hizo 'findings' ni halisi!
Ni pungu tu ndio hawezi elewa jinsi dunia inavyooperate hasa linapokuja suala la weusi! Tumekuwa guinea pigs kwa mambo mengi sana ya kipumbafu kwa faida ya wazungu!
Hii covax nayo inapita mlemle! Hili la corona kwetu sio issue kubwa ukilinganisha na makubwa tunayopitia! Isitoshe nguvu inayotumika 'is out of proportion'! Mimtu iliyopoteza uwezo wa kuhoji kama ww kwa kumeza kila kitu hao wazungu 'wanasayansi' wanachosema/kuandika ni hasara sana kwa kizazi hiki!
Eti 'scientific evidence' hivi unaelewa vizuri hata maana ya hilo neno!?
Una scientific evidence yoyote kuwa miaka 10, 30, 50 baada ya kudungwa covax madhara gani yatawapata waliodungwa na vizavi vyao!?
Useless people like you are really a huge set-back to our existence in this beautiful planet earth!
 
Back
Top Bottom