Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Umeongea ukweli mtupu mkuu.
Kitu chengine cha kuongezea ni jinsi audience wa Lissu wanavokuwa engaged anapoongea Lissu. Hawa watu ukiwaangalia unaona shauku yao ya kutaka kujua na kufahamu wanachoambiwa. Kwa ufupi wako very attentive na wenye shauku wa kusikia na kujuwa kila sentensi inayotoka mdomoni mwa Lissu.

Ama kwa upande wa Magu hali inakuwa ni tofauti kabisa. Utakuta watu hawako engaged kabisa na kinachoongewa. Wengina wanaongea, wengine wanafanya biashara na katika uwanja kila mmoja yuko na direction yake! Na wengine wakiwa na shauku ya kuwaona na kuwasikiliza wasanii.

Unaona kabisa kwamba watu wengi ndani ya hadhara za Magu kila mmoja kaendea lengo lake. Kwa tathmini ya haraka haraka unaweza kuona kwa asilimia 70 au zaidi hawana hamu na kinachoongewa na mgombea.
 
Natofautiana na mawazo ya mleta mada.
 
Lissu hatoshinda.,,
Viongozi wote njaa walioanguka walikuwa na wapambe njaa kama wewe , walikuwa na watu wa kabila zao , waliwaapisha majenelari na Mapolisi waandamizi , kung'olewa kunapofika hakuna cha wapambe wala cha mswalie mtume
 
Walau wewe kidogo una akili.

Ila manyumbu wenzio hata akili ya kutambua kuwa Lissu hatoshinda, hawana.
Kama vita mlikuwa mnavisikia mataifa mengine, mtaviona nchi hii iwapo Lisu atashinda na asitangazwe. Uzuri wa nyakati hizi teknolojia ya mawasiliano imefanya usiri usiwepo. Tutajumlisha namba za kura nchi nzima na matokeo tutakuwanayo. Ole wenu mtangaze tofauti, mtaikimbia nchi.
 
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Hiyo vita utapigana wewe na nyumbu wenzio?
 
Walau wewe kidogo una akili.

Ila manyumbu wenzio hata akili ya kutambua kuwa Lissu hatoshinda, hawana.
Kama umetoka kutoamini Lissu hatashinda mpaka kuamini kuwa Lissu atashinda ila hatotangazwa basi jiandae kuamini kuwa Lisu atashinda na atatangazwa
 
Mchwanwi nchi hii sio Jiwe ni Tume na vyomvo vya usalama vinavyompa kiburi
 
CCM Wanaujua ukweli ndo maana walizuia mikutano kwa miaka 5, walizuia bunge live, walimpiga lisasi, Sasa wamefungia magazeti, na kuzuia habari za charismatic leaders zisitangazwe
Wameshafeli Zinatangszwa bila kujua zinatangazwa na nani
 

Wewe inaonekana haujaposa bado... acha matusi bradha... haisaidii... na hata hivyo watakimbia wakiwasahau 'their better half' nyuma?
 
Charisma ya Lissu ni kama ya marehemu Thomas Sankara, yani huyo alikuwa akiongea hata kama huelewi lugha unapata mzuka. Halafu wote wanafanana kwa kujali maendeleo ya watu.

CCM walete wanamuziki toka Nigeria na Marekani ndio fiesta yao itabamba. Otherwise JPM ataendelea kuwa gumzo kwa pumba atakazoongea, Lissu atakuwa gumzo kwa madini atakayotema.
 
Kwa sisi watu wataalamu wa Sayansi ya Siasa tunaposhuhudia mgombea wa Chama Kikubwa Kikongwe (Vanguard Party ..ya Kijamaa) anapelekeshwa hivi tunajua tuna kitu hakipo sawa!

Kwa hii miaka mitano mfumo wa Utawala ulifsnya jitihada kubwa ,nyingi za kuua CDM matokeo yake Ni kinyume! Je Nini kimesababisha haya!

Mosi,mabadiliko makubwa ya kifikra ,na hii inaashiria Watanzania wao tayari kwa mabadiliko.Kinachosekana Ni wakala wa kuongoza haya mabadiliko! Na Sasa yaelekea Tundu anajaribu kuziba ombwe hili! CCM walitakiwa wajiuluze Sana kwa yaliyotokea 2015! ,Ambapo almanusura watu wampeleke Lowasa Ikulu !

Lowasa angekuwa na uwezo wa kujenga hoja Kama Tundu sijui Hali ingekuwaje!?

Pili,Kuna tatizo kwenye mfumo wa Uongozi wa CCM . Pengine Mwenyekiti Hana washauri wazuri au hashauriki.

Sababu ya tatu Ni Mwenyekiti kushika hatamu! Tumexhuhudia miaka 5 ya Zidumu Fikra za Mwenyekiti! Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Idara na Taasisi , RC, DC , WEO, Madiwani wote wanamtukuza Mwenyekiti! Na Bahati mbaya sana hili linafanyika kinafiki.

Nne', Kosa kubwa wanalofanya CCM, ni kutumia nguvu kuwanyamazisga wapinzani. Leo hii nguvu kubwa ileile inatumika kunadi Sera ziluzotukuzwa kwa miaka mitano!

Tano, CCM wameshindwa kubaini kuwa kizazi kiaminifu' na Sera za Chama bila kujali chochote kinapotea kwa Kasi. Hawa walizaliwa , wamekua na TANU,CCM na Nyerere huwaambii kitu!

Mwisho, CCM Ni muhimu wajiandae kuyapokea mabadilko makubwa Sana katika Fikra za Watanzania. Ni aibu na fedheha mtu mzima akitaka kuongea na wananchi kutumia nguvu kubwa namna hii .. wasanii na wachekeshaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…