Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Mgombea wa Urais anayetarajiwa kupata ushindi mkubwa Tundu Lissu leo ataitetemesha Chato na viunga vyake katika kampeni zake zilizoivuta Dunia.

Taarifa kutoka ndani ya Team yake ya Kampeni kabla ya kuhutubia mkutano wa Hadhara atautembelea Uwanja wa ndege wa Chato uliozua gumzo nchini kote kutokana na Ujenzi wake.

Tundu Lissu amepata uungwaji mkono mkubwa kutoka Makundi yote ya Jamii hususan Wafanyakazi ambao wanalaani kupitishwa kwa sheria Haramu ya kupora Mafao yao. CCM na serikali yake walipitisha sheria ya kuzuia Mafao ya Wafanyakazi hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30 haruhusiwi kupewa haki yake ya mafao mpaka afikishe miaka 60.Sheria hii Haramu imelaaniwa na kila mfanyakazi na Tundu Lissu ameapa kuifutilia mbali Mara tu baada ya kuapishwa.

Ingawa Chato ni nyumbani kwa mgombea Urais wa CCM Lakini kwa muda mrefu CHADEMA imekuwa na uungwaji mkono mkubwa na inao wafuasi wa kutosha.Mmoja wa makamanda mashuhuri wanaotokea Chato ni mwanamama Husna Amri ambaye anajulikana nchi nzima kwa ujasiri wake.

Tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika mapokezi na Mkutano wa Kampeni hapa Chato.
Mara ya tatu hii anazurura kanda ya ziwa! Mwambieni imekula kwake haoni kitu hapo!!! Akamuulize mzee lowasa!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kutembelea uwanja wa ndege Chato ni kichekesho. CHADEMA bana, hata hawajielewi.
Kwani kuujenga nayo ilikuwa kichekesho?
 
Robert Amsterdam ameandika leo kuwa ni wazi Lisu hatatangazwa . Ameshauri international community ijiandae kwa njia za amani aliyeshinda atangazwe!
Kwani Rob ndio msemaji wa tume , au ina maana sisi watz hatuna uwezo wa kuamua nani tunamtaka awe rais wetu hadi tusikilize maoni ya huyo wakili wa Lissu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya ccm kuiba fedha za wafanyakazi wakaamua eti kuunganisha mifuko na kuzuia wafanyakazi kuchukua michango yao pindi wanapohitaji baada ya kazi kuisha, hili la kuweka hadi ifike miaka 60 ni zuluma sawa na zuluma zingine mfano rambirambi, wakulima wa korosho, uporwaji pesa za bureau de change, nyongeza za mishahara, nk.

Hii michango inafaa iwe kujiunga Ni hiari kwa anaetaka maana haina faida kujiunga na kitu kisichofaida.
Waliofilisika mifuko kina Dau wakazawadiwa na ubalozi kabisa ili wapate nafasi ya kutumbua pesa zetu huku tukiambiwa tusubirie miaka 60 utadhani una ahadi na Mungu kufika hio 60 lengo wanajua wengi watakuwa wameshakufa bila kupata michango yao.
 
Unamfananishaje Mh.Lissu na kutumwa?Nani mwenye uwezo huo hapa duniani?Yaani umtume Mwalimu wa Sheria eti kwa kivuli cha ubeberu!

CCM mnamfahamu Mh.Lissu na Utetezi dhidi ya wanao/walioonewa na kunyanyaswa kwa maisha yake yote,siyo kama hawa wasanii.
Tunataka kumuandalia magufuli darasa rasmi la sheria chini ya Mwl Lissu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya aende akajionee..
Nikukumbushe tu kuwa uwanja wa ndege wa chato si kwaajili ya wanachato pekee. Labda ulitaka watalii wafikej vipi mbuga ya Burigi? Ndege sio kwa kila mtu..tunaopanda mabasi ya kuungaunga tutaendelea kuwepo. Wenye uwezo wa kupanda ndege watapanda.
Geita ni mkoa mkubwa kibiashara lazima maendeleo yapelekwe
Maendeleo Yana maeneo Yana chama,ama nimeelewa vibaya.
 
Kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii na fao la kujitoa hapa Lisu ndo anatakiwa apigilie misumari ya nchi 10 kabisa ili kuisambaratisha kabisa ccm, iweje pesa yangu nipangiwe mda wa kuichukua
 
Screenshot_20201013_111646.jpg
 
Mkuu kwanza usinitishe ili nikuele navijimaneno vyako hivi "Ukishindwa kujua umuhimu wake basi hata wewe umuhimu wako hapa tanzania haupo"
kwanza ujuwe mimi sio mujinga au pumbavu kama wenzio wana Lumumba am undecided voter .nimekuuliza economic benefit ya Chato Airport to this country niipi?? wewe unarukaruka kuniletea habari za barabara,hospitali n.k umeshindwa kujibu swali rahisi huna akar kabisa wewe usije rudia tena kuita watu hawana akiri wakati IQ yako mwenye ipo very low and norrow.Goat kabisa wewe
Maandishi yako na kutokuwa makini katika silabi na ilabi ni kweli huna hizo akili anazodhani unazo.

Jamaa yuko sahihi
 
Mgombea wa Urais anayetarajiwa kupata ushindi mkubwa Tundu Lissu leo ataitetemesha Chato na viunga vyake katika kampeni zake zilizoivuta Dunia.

Taarifa kutoka ndani ya Team yake ya Kampeni kabla ya kuhutubia mkutano wa Hadhara atautembelea Uwanja wa ndege wa Chato uliozua gumzo nchini kote kutokana na Ujenzi wake.

Tundu Lissu amepata uungwaji mkono mkubwa kutoka Makundi yote ya Jamii hususan Wafanyakazi ambao wanalaani kupitishwa kwa sheria Haramu ya kupora Mafao yao. CCM na serikali yake walipitisha sheria ya kuzuia Mafao ya Wafanyakazi hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30 haruhusiwi kupewa haki yake ya mafao mpaka afikishe miaka 60.Sheria hii Haramu imelaaniwa na kila mfanyakazi na Tundu Lissu ameapa kuifutilia mbali Mara tu baada ya kuapishwa.

Ingawa Chato ni nyumbani kwa mgombea Urais wa CCM Lakini kwa muda mrefu CHADEMA imekuwa na uungwaji mkono mkubwa na inao wafuasi wa kutosha.Mmoja wa makamanda mashuhuri wanaotokea Chato ni mwanamama Husna Amri ambaye anajulikana nchi nzima kwa ujasiri wake.

Tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika mapokezi na Mkutano wa Kampeni hapa Chato.
Kuna tetesi kuwa Polisiccm wanawatishia watu wasiende kwenye mkutano huo maana Duniani kote wanautizama kama live mechi ya Liverpool vs man u au Barcelona vs Real Madrid
 
Hii hesabu feki. Tanzania ni kubwa sana, hakukuwa na sababu ya Lissu kurudi kanda ya ziwa mara ya tatu. Anapoteza muda wake na resources, wasukuma hawezi kuacha kumpa kura mtu wao.
Kwani Lissu ndiye anapanga ratiba?
 
Back
Top Bottom