Chonde chonde Rais Samia, Kipengele cha Dini kwenye sensa ni muhimu sana kwa sababu hii

Kila utafiti huwa na malengo yake. Hayo uliyoyaainisha yanatakiwa kuwa katika National Surveys siyo census ambayo ni total head count. Dhumuni kuu la Sensa yeyote ni kwa ajili ya kupata takwimu kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo ya sehemu husika.

Maswali yanayoulizwa ni kwa ajili ya kupata data ili serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo. Mfano umri, serikali inataka kujua Watoto ni wangapi, ili iandae Chanjo; nguvu kazi ni wangapi, ili Ijidhatiti na Ajira; wanaopaswa kuwa shule ni wangapi ili iandae madarasa; wazee ni wangapi etc.

Maswali haya ni yale ambayo kwa utashi wako huwezi kuyabadili. Mfano mwanamke hawezi kujibadili kuwa Mwanaume au ukiwa na miaka 10 huwezi Kurudisha nyuma umri wako.

Dini ni kitu kinachobadilika Leo mimi ni muislam, kesho naweza kwenda kwa Zumaridi nikawa mlokole wa kizumaridi. Je, huoni hii kitu hakina tija? Leo utasema kuna waislamu 100 kesho wote wamekuwa wahindu! Uliza wakatoliki waumini wanavyoondoka kuwa walokole wakupe experience. Hivyo swali la dini katika Sensa halina maana ila katika tafiti ambazo zinatanywa ili kupata majibu ya matokeo fulani. Mfano kwanini sehemu hii watoto wengi wanakufa, hapo swali la dini ni muhimu
 
Hahaha Eti mlokole wa kizumaridi

Unajua mwanzoni nilikuwa naona Zumaridi anaonewa, kuwa aachwe afanye huduma yake, ila sasa namtazama tofauti baada ya kupitia video zake nyingi

Ni kweli ana uhuru wa kufanya anachofanya na aachiwe tu kama hana hatia ila anachohubiri kina uelekeo wa kufuru hakina utakatifu wowote
 
Huna hoja hata ya maana

Serikali haihudumii watu kwa msingi ya kidini au kikabila sababu Haina dini

Yenyewe huhudumia sababu ya kuweko mahitaji eneo husika.Na kujua kuna hitaji nini Serikali wala Haina haja ya kufanya utafiti wa kina sababu mbunge wa eneo ambaye ni mwakilishi wa eneo husika yupo.

Serikali Haina dini hivyo haihudumii dini
Unasema mtumushi akifa eti huzikwa na Serikali kwa mujibu wa imani yake? Mnadanganya huko mnakokutana.Toka lini Serikali ikazika mtu kidini? Mtumishi Akifa ndugu wa marehemu ndio huamua azikwaje sio Serikali. Na ndugu ndio hutafuta shehe au padri wa kufanya shughuli hiyo ya mazishi sio Serikali
 
Nonsense
 
Wewe ni Mmasai, kabila ya Baba.
Kuzaliwa na Mama Mchagga, kulelewa Uchagani, kukulia Uchagani na kuzungumza lugha ya Kichagga, hakukufanyi upoteze asili yako halisi ya Umasai. Naomba kukuuliza swali dogo, jichunguze ukikasirika kama unakasirika Kichagga au Kimorani wa Kimasai?.
P
 
Mkahesabiane huko huko misikitini na makanisani kama mnataka kujua mko wangapi

Mfano katoliki wanajuana idadi yao dunia nzima
Ila wao huhesabiana kwa lengo kuu moja kujua waweke huduma za kijamii mfano wajenge shule kiasi gani za ukubwa gani kwa ajili ya waumini wao.Kama zilizopo chache waongeze zingine au kuzipanua nk Sababu waumini wao huamini katika ubora wa shule za katoliki

Pili huhesabiana ili kujua majengo ya ibada yajengwe ya ukubwa kiasi gani kulingana na wingi wa watu

Hizo takwimu zinawasaidia huko kwao sio kazi ya Serikali kuwatafutia hizo
 
Katika ambavyo vina muda mchache kufa ni vikabila na Lugha za kikabila

Pascal wewe msukuma watoto wako wanaongea kisukuma?

Fikiria maasai anao mzaramo .Mtoto atakayezaliwa kumwita ni maasai sio sahihi yule chotara wa mchanganyiko wa maasai na mzaramo

Huyo chotara akikua anakuja kuoa Mchaga atazaa chotara lingine mchanganyiko wa chotara na mchaga

Kifupi kwa sasa asilimia kubwa ya vijana na wasichana ni machotara waliotokana na ndoa mchanganyiko. Kuna kabila jipya la machotara
Msukuma unazaa na Mzungu bado mtoto unasema kabila msukuma haiko sahihi sana hiyo
 
Erooo Msalimie Laltaika
 
Hakuna haja kabisa ya Kipengele cha Dini kuwekwa katika Sensa
 
Ukianza kuzungumzia Udini na Ukabila nahisi UKABULU unapiga hodi katika nchi yetu!
 
Naona wanakuponda lakini nadhani wewe umekuja na hoja nzito na bila shaka umebobea sana kwenye utafiti. Tatizo wengi huku hawatakuelewa.
 
Dini ni kitu kinabadilika badilika ujue
 
Hapa ni suala la kufanya utafiti siyo sensa
 
Sina tabia za kimasai kabisa. Yani mimi ni mchaga hata tukikutana leo utajua tu ni mchaga mpaka nikuambie kuwa sio.


Biologically ndio nakubali mimi ni mmasai. Lakini socially huwezi kusema mimi ni mmasai. Nafit zaidi kwenye uchagga.
 
Uko sahihi yeye yuko wrong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…