Chonde chonde Rais Samia, Kipengele cha Dini kwenye sensa ni muhimu sana kwa sababu hii

Sina tabia za kimasai kabisa. Yani mimi ni mchaga hata tukikutana leo utajua tu ni mchaga mpaka nikuambie kuwa sio.


Biologically ndio nakubali mimi ni mmasai. Lakini socially huwezi kusema mimi ni mmasai. Nafit zaidi kwenye uchagga.
Bwana wee naenda ukasalimie huko Umasaini upajue vyema.
Kuna umuhimu asee.
 
Hii hoja ishindwe 100%
Nimejaribu ku-google nchi nyingine. Kila nchi niliyoona taarifa zake wameweka takwimu za dini za raia wao mfano nchi ya Chad iko hivi:
Religion
(2015)[2]
Hiyo ni kwa mujib wa sensa waliyofanya 2015.
Kimataifa nchi zote wanaoyesha hivo. Mimi sijui faida au hasara yake. Kuna nchi ambayo hata bila kuhesabiana, tayari wanajua, hata watu wa mataifa mengine wanawajua takwimu zao za dini. Mfano Misri wanajijua kabisa idadi ya waislam ni kubwa kuliko dini nyingine. Poland wanajijua, na sisi tunawajua kuwa wakristo wakatoliki ni wengi kuliko dini nyingine. Je kwa takwimu hizo kujulikana kumekuwa na faida gani? Je kumekuwa na hasara gani?
Tujiulize (hapa utafiti ni muhimu) kwa Nini mataifa mengine wanapofanya sensa wanatoa na takwimu za imani za raia wao? Kwa Nini sisi tuache jambo ambalo wengine wote wanafanya? Na kwanini tufanye kwa vile wengine wanafanya?
 
Kwenye makabila pia nako kuna tatizo la ukabila.
 
Acheni ubaili taasisi yenu itenge fungu ili mjihesabu mjijue mpo wangapi. Itawasaidia kujiendeleza Kama taasis. USIJIBANZE KWA SERIKALI IKUFANYIE KAZI MAANA SERIKARI HAIONI MASIRAI YAKE.
 
Sasa kama kundi flani ambao wanaongiza kwa utajiri Tanzania na Asia misaada wanayopeana ni misikiti na visima vya maji misikitini? Utafanunishaje na wanawekeza kwenye mashule na mahospitali?
 
Kwenye makabila pia nako kuna tatizo la ukabila.
Kabila linabeba historia ya mtu maana kabila unapata kwa baba na kurithi vizazi kwa vizazi milele. Kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayokuja tunahitaji data za makabila ili mbeleni tuzidi kujua chimbuko la jamii zetu na uhusiano wa kihistoria/kibaologia na jamii zingine.

Japo hata Tanzania kwa haraka haraka unaweza kujua dini gani wapo wengi hata kwenye internet unaweza pata hizo data bila hata kuweka kwenye sensa.
Just hesabu nyumba za ibada kila kata uone misikiti, makanisa, hekalu au nyumba za mizimu zipo ngapi utapata majibu ni dini gani wapo wengi

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kipengele cha dini ni upuuzi kuwekwa kwenye sensa. Sensa inalenga kutathmini maendeleo mutually na sio mafungamano yake na dini. Sioni hoja yeyote yenye msaada uliyoitoa pale serikali itakapogundua mikoa fulani iko nyuma kimaendeleo kwasababu watu wake ni wa dini fulani, zaidi ya kusema 'serikali inakazi ya kufanya' kazi ipi sasa? Kwa maoni yangu Kama ambavyo umeshindwa kuisema kazi hiyo inayotakiwa kufanywa na serikali basi ndivyo upuuzi wa hoja ya dini unaanzia hapo hapo. Ukishajua mkoa wa Lindi unawaislamu wangapi vs wakristo then what? Itakusaidia nini kwenye kupanga ujenzi wa barabara, shule, zahanati na upatikanaji wa maji? Kama shule haikujengwa wakati wa ukoloni mtwara kisa uislamu Kama hoja yako inavyojielekeza implicitly, ni muislam gani atakataa kwenda shule ukijenga leo kule tandahimba. Hitimisho hoja ya dini leo bado haina mashiko Kama ambavyo haikuwa na mashiko siku za nyuma Kama utachukua muda wako kujielimisha juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi kwa muktadha wa maisha ya sasa ya mtanzania. I rest my case.
 
Ni kweli maendeleo ya kiuchumi/kijamii yanahitaji takwimu sahihi, lakini je nikweli takwimu hizo ni pamoja na dini ya mtu? Kwamba eneo hili linahitaji kituo cha afya basi tujue watu wake ni dini gani? Naomba nikuulize, umetetea kipengele cha dini kwa hoja hiyo hiyo ya mazishi ya mazishi au unahoja nyingine ambayo ungedhani ni muhimu serikari ikajua dini yako?
 
Kipengele cha dini hakitatuletea tija yoyote ila kitaleta vurugu tu hapa nchini. Maswala ya dini yanatakiwa kufanyika huko huko kwenye familia. Serikali haina dini- ila wananchi wana dini zao. Serikali inatakiwa kuhakikisha maendeleo ya kila mwananchi yanapatikana kwa kupanga mikakati mizuri- kujenga mashule, zahanati, kuboresha huduma za maji,kuboresha barabara, kupiga vita mila potufu, kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule, kutunga sheria nzuri, kuhakisha uhuru na usalama wa raia mahali popote. Je Ukijua Tanzania kuna waumini wa dhehebu fulani ni asilimia 51% - je hii itakusaidiaje kuleta maendeleo kama si utengano tu. Itakuwa sisi tupo wengi tunatakiwa tupewe nafasi zaidi katika kila kitu.
 
Nimeorodhesha sababu kadhaa hapo sijui umesoma au umekimbilia tu kujibu
Kuweka sababu haina maana kuwa zitakuwa na mantiki. Hujawahi kuona mwanafunzi kajaza karatasi ya majibu na bado kapata 0.

Serikali inakatazwa kufanya mambo kwa ubaguzi wa aina yoyote, isipokuwa tu kwenye maeneo machache mfano upendeleo wa wanawake na walemavu. Serikali ikiamua kuanza kufanya sera za maendeleo kwa kuangalia dini, itashitakiwa mahakamani kwa kuvunja katiba; kwa hiyo point yako ni null and void. Hakuna umuhimu wa kutafuta hizo taarifa maana haziwezi kutumika.

Kama unataka kujua wapi umaskini unatokea, angalia vitu kama wapi eneo lipo, geografia na climate ya eneo. Jiulize, huo mkoa una-produce kitu gani cha maana cha kuwaondolea umaskini. Nyanda za juu Kusini wana mipaka na nchi muhimu, ardhi na hali ya hewa ya kulima mazao muhimu ya biashara kama kahawa etc Nyanda za juu Kaskazini ni kilimo na utalii. Sasa kama pia maeneo hayo yana watu wa dini fulani, ujue yana maendeleo sio kwa sababu ya dini, kuna sababu nyingine za ziada.
 
Bora dini iulizwe kuliko kabila la mtu maana wazilankende hawakawii
 
Dini kwa macho ya kawaida inaonekana siyo muhimu kutajwa, ila kuna mahali ambapo ni muhimu kujua dini ya mtu.

Let's say hospital umeenda hujajaza kipengele cha dini, ikatokea umefariki na hakuna mtu wa karibu hapo utazikwa kwa akina kinjekitile.

Kwa watanzania dini ni muhimu vinginevyo Roman Catholic watatawala wao milele
 
Point yangu kwenye makabila kuna tatizo la ukabila hilo unalizungumziaje?
 
Point yangu kwenye makabila kuna tatizo la ukabila hilo unalizungumziaje?
Nimekupata. Ukabila Tanzania ni ngumu sana kuutekeleza kwa vile makabila ni mengi sana. Udini ni rahisi kuleta madhara kwa vile una makundi makuu mawili yaani ukristo na uislamu. Ni rahisi mkristo mchaga kuwa na ukaribu na mkristo msukuma kuliko mkristo mchaga kuwa na ukaribu na mwislamu mchaga. Dini hizi zinapingana na kubaguana kwenye mafundisho yake lakini tamaduni za makabila hazipingani wala kubaguana.
Ni rahisi mtu kuoa mtu wa kabila tofauti lakini sio rahisi mtu kuoa mtu wa dini tofauti.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
UMEANDIKA UPUMBAVU NA UPUUZI.

HATA SIJAKUELEWA NAONA UNALIA LIA TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…