Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Wewe ni analytical na inawezekana ulikiwa sehemu ya kikao,,siyo wengine wanaona sifa kupinga na kumuattavk General Mabeyo kwa maelezo yake
 
Mtazamo wangu baada ya kuona hii video

Kwanza haikuwa ajabu kwa jiwe kutaka kuzungukwa na wanausalam wakati wa ugonjwa wake, naamini hao ndio ambao alikuwa anawaamini sana ukiangalia na uadui mkubwa aliokuwa nao hapa ndani ya inchi na nje ya inchi

Pili,kuhusu kupewa taarifa kwanza Waziri mkuu kabla ya makamu wa raisi nadhani ni hekima imetumika hapa, mwanamke ni mwanamke tu, namna ya upokeaji wa taarifa kama zile lazima itumike busara kubwa,, kwahiyo wakati mwingine si suala la kufuata utaratibu bali ni kutumia hekima na busara.

Tatu,naungana na wale wote ambao wamesema kuchelewa kuapishwa kwa raisi ndani ya masaa ya 24 ni kutokana na hii ni experience ya Kwanzaa ktk inchi yetu lazima kuna mambo ya kuyaweka sawa na kujadiliana

Jiwe atabakia kuwa Kiongozi wetu bora wa mda wote pamoja na mapungufu ya kibinadamu aliyokuwa nayo.

Ni hayo tu!
 
Alivuta kamasi na sio alikuwa analia
 
There is a reason amelia. Hawa watu wanajua mengi sana. Sababu za kiusalama, wanakaa nayo milele ndani ya roho zao.

Naombea roho ya marehemu JPM ipumzike kwa amani.
Kama kuna kitu anajua kwanini kama mwenyekiti wa usalama kitaifa haku take action? Hakuna lingine lililofichika zaidi ya alicho simulia hapo.
 
Hivi mnaamini hizo porojo anazosema Mabeho? Kwanza Magufuli hakufariki huo muda anaosema. Pili Magufuli alipelekwa Nairobi na ndiyo maana alikuwa anasema nirudisheni nikafie nyumbani. Ni kweli walimrudisha na akaja kufia Mzena. Tatu, suala la kuapishwa lilicheleweshwa kwa sababu ya mvutano wa kutaka Samia asiapishwe. Kwa kifupi amezungumza ukweli nusu.
 
Na umeamini yote aliyosema? Mbona hakusema kuwa Magufuli alifariki tangu tarehe 12? Mbona hakusema alipelekwa Nairobi na iliposhindikana ndiyo akarudishwa Mzena? Unajua ni kwa nini amesema Magufuli alikuwa anasema nirudisheni nikafie nyumbani? Ni kwa sababu alikuwa Nairobi!
 
Kuna kitu cha siri kukbwa kimo ndani yake anachokijua ila anachokiangoea ni kwa ajili ya kutasababisha taharuki. Lakini kwa ujumla kuna uwezekano wa uharifu kufanyika dhidi ya uhai wa JPM

1. Mtu anayetuhumiwa kuchangia kupotea uhai alikuwepo kwenye jopo la matibabu ya JPM muda wote
2. Rais aliyepo madarakani sasa hivi aliapishwa kinyume na sheria kwa kuwa zilipita siku mbili baada ya kifo badala ya saa ishirini na nne kwa mjibu wa sheria na katiba
3. Hata hivyo CDF apongezwe kwa kukataa agiza la JPM la kuwa sehemu ya mauti yake alipoagizwa awaamuru madaktari wamtoe hospitali na kumpeleka nyumbani huo ni msimamo wa ujasiri sana kukataa agizo la amiri jeshi mkuu.
4. Majadiliano kati ya CDF, DGSS, IGP, PM na CS baadae Makubi na Pengo ni yapi?
5. Inasemwa kwamba CJ na Shekhe mkuu waliitwa pia kuna ukweli gani?
6. Kwanini JPM yeye mwenyewe binafsi alitambua hatapona wakati madaktari hawakuwaambia wakuu wa majeshi mpaka JPM alipomwita CDF huku professa mmoja aliyekuwa JKCI alikuwepo muda wote hapo hospitali?

Upo muda kule mbele lazima uchunguzi utafanyika au kuna mtu ataamua kujitoa mhanga kusema ukweli ya kilichotokea ndipo kutakuwa na hali mbaya sana ya mahusiano kati ya wananchi na watawala wa sasa.
 
Usilete ujinga wako hapa kama mlimwua ipo siku mtajuta kuzaliwa
 

Kuna mtu kaeleza hapo kuwa kurudishwa nyumbani alimaanisha kuondolewa Nairobi na Kuja Tanzania ili asifie ugenini.
 
Maybe kuna watu walimfanyia vibaya marehemu then akaja lifahamu hilo and yeye hakuweza fanya kitu kuzuia hio hali,jiwe alikua na enemies mpk ndani ya system yake mwenyewe
 
Kuna mtu kaeleza hapo kuwa kurudishwa nyumbani alimaanisha kuondolewa Nairobi na Kuja Tanzania ili asifie ugenini.
Hakuna sejhemu CDF mstaafu kaeleza kutolewa Nairobi kwenda Mzena na mwandishi aliyekuwa anamhoji alipotea boya kuhoji kwamba walitoa walimtolea wapi.

Mimi nilivyoelewa ni kwamba kutoka Mzena kwenda Chato ambako ndio nyumbani kwao. Ikulu sio nyumbani kwake ni nyumba ya umma anayopangiwa na wananchi wa Tanzania.

Mzunguko wote huu hausaidii ipo siku itajulikana kilichotokea bayana
 
Watanzani bwana kwa kujifanya wajuvi wa mambo
 
Usilete ujinga wako hapa kama mlimwua ipo siku mtajuta kuzaliwa
Mimi ningepata wapi uwezo wa kumuua Magufuli aliyekuwa anachungwa na kila aina ya watu na zana? Sikiliza: Kwa hao wakuu wa vyombo vya usalama walitakiwa kuwajibika kwa sababu ya kifo chake. Walikuwa wanajua kabisa kuwa kwenye suala la covid, rais alikuwa kwenye risk group kwa sababu alikuwa na pacemaker, hivyo alitakiwa aji-isolate kadiri iwezekanavyo lakini wao wakaogopa kutumia powers zao kumshurutisha na badala yake wakamwachia ajichange na watu. Kusema kweli hawakutimiza wajibu wao. Mbona ugonjwa uliponza aliji-isolate kwa kwenda kukaa Chato? Kwanini walimuachia arudi?
 
Una uhakika gani alikuwa na COVID-19?

Wewe ni sehemu ya waliojipenyeza kutumia mwanya wa dhania ya COVID-19 kumwua ipo siku utajuta hili halitasahaulika na kuchwa lipotee bure bila wahusika ..................
 
Watanzania kujifanya wajuaji kwenye mambo msiyo yajua ,sasa hapa unachambua matukio kwa mawazo na maono yako utadhan kweli wakati hizo ni hisia zako tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…