Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Sasa cha kushangaza Mabeyo pamoja na kujitahidi kutabasamu ila chozi lilimshinda nguvu kwa sekundę kadhaa ameonekana akibubijikwa machozi ya hudhuni mbele ya camera
Acha uongo hakuna mahali amelia kwenye video, why unaleta misinformation na fake news!!

Nakuonaga mtu makini sana kumbe propagandist tu
 
Intelejensia ya Jeshi vs Intelejensia ya "TISS" kuna sehemu ipo shida.

Yawezekana kuna kundi liloegemea Chama Tawala (CCM)au wapenda maslahi binafsi na kuacha misingi kazi .

Mambo mengi ya msingi hayazingatiwi na utashi wa wengi (wananchi)unapotoshwa.
Mfano:
1.Katiba ya nchi ina kasoro,inajulikana,lakini yanaletwa maneno ya kisiasa kuchelewesha marekebisho.

2.Sheria ya kodi na tozo bado zina mtazamo wa kijamaa(bado kumiliki gari inaonekana ni anasa).Badala ya kupunguza kodi ili wengi waingie kwenye kundi la walipa kodi ili mapato yaongezeke!!

3.Sheria ya uchaguzi kuwa na kasoro(mfano "kipengele kinachosema "mshindi ni aliyetangazwa",hii imetumiwa vibaya na viongozi walioteuliwa kutangaza matokeo yasiyo kuwa na uhalisia,rejea uchaguzi wa mwaka 2020)
TISS imejaa makada tupu
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=9Hyg_T0yb-8

Katika dunia hii mtu wa mwisho ambae unaweza kuona chozi lake hadharani ni senior army officer na army general ndio kabisa awezi kuonyesha weakness hiyo hadharani.

Sasa cha kushangaza Mabeyo pamoja na kujitahidi kutabasamu ila chozi lilimshinda nguvu kwa sekundę kadhaa ameonekana akibubijikwa machozi ya hudhuni mbele ya camera. Kumbuka ata alipofiwa na mtoto wake rubani, general akutoa chozi alipofika eneo la tukio.

Je anajutia kutosikiliza maamuzi ya watu waliomshauri wapindue męża ya katiba huyo mama hiyo nafasi sio size yake na kinachoendelea leo Tanzania.

Mabeyo anasingizia eti two thoughts ndio zilichelewesha kumuaoisha Rais wakati huo huo anasema kikatiba inatakiwa within 24hrs,hivi anajaribu kumfanya nani ni mtoto hapa wa eti huo ndio ulikuwa mjadala? 🤣🤣🤣🤣

Huyu huyu alitoa Kauli ya utata baada ya Mazishi kule Chato.Aache kujikanganya kama sio mzungumzaji mzuri.

Kwanza sio sawa kabisa kuwafahamisha PM na KMK taarifa za kifo Cha Rais kabla ya VP Kwa kisingizio Cha eti VP Yuko ziarani Tanga.

Hapo Kuna maswali mengi kuliko majibu ya ule uvumi.

Kiufupi Mimi ndio ningekuwa Samia ningewafyeka wote waliopindisha utaratibu.
 
Chozi la Mabeyo linaungana na machozi ya maelfu ya watanzania waliolia na wanao endelea kulia kutokana na madhira waliyo yapata wakati ule wa mtu yule.
Kwa uchache tu nawakumbuka watumishi 12 Elfu walio ondolewa kazini kwa kuwa eti walifoji vyeti.
Wengine walikuwa wamefanya kazi zaidi ya miaka 20...!
 
Mabeyo alipewa cheo na kila kitu na Jiwe.

Ndio maana analia.

Maana ingekuwa ni UBINADAMU tunheuona kwa kina Azory Gwanda, Tundu Lissu na kina Been Saanane
Mkuu kwema? Yani tangu upigwe ban eti siku hizi unasusa jamvin
 
Kama umesikiliza mwishoni ile ni diplomatic language tu kwa nafasi lazima awe responsible kwenye kauli zake kutoingilia siasa zinazoendelea.

Lakini body language ndio kila kitu hasa akielezea siku za mwisho ilivyokuwa hadi mauti yanamkuta marehemu.

Itakuwa kuna kitu kinamuumiza mpaka leo yale malengelenge ya machozi sio bure na kushindwa kuzuia emotions zake ata kwenye kuongea kwa majonzi ile się tabia ya army general kushindwa kujizuia. Kwa nafasi yake mtu kama yeye kwa kwa nilichokiona ni big deal kiaskari duniani.
Kumpoteza Magufuli kwa ghafla namna ile iliumiza na bado inaumiza watu wema wengi wanaoitakia mema Nchi hii. 🙏🙏 !
 
Hao waliosahau katiba mpaka wakakumbushwa na cdf kuwa raisi akifariki makamu ndo anakua raisi ni kina nani? Ni kweli walsahau au walitaka kujisahaulisha, kama walisahau jambo kubwa kama hilo, mengine wanayakumbuka? Nadhan kuna haja vyombo vyetu viendelee kuwakumbusha watawala wetu hawa "wasahaulifu" kwa vitendo kama Africa magharibi walivyoamua kufanya, wawakumbushe wamesahau umasikini wa wananchi wao, elimu, afya, maliasili, bandari, barabara, maji, umeme, haya yote wamesahau wakumbushwe, ila pia wakumbushwe wamesahau sasa hivi chai na mkate haviwezekani tena kwa raia wao walio wengi, wamesahau pia Milo mitatu hata kwa mtumishi wa umma ni mbinde na balaa kwa bibi yangu pale nyabange na babu yangu wa nyalusulya. Wamesahau katiba, sisi tutakumbukwa? Wasomi andikeni vitabu vingi kutoka kwenye maneno haya machache ya cdf mstaafu, vitabu hata elfu.
 
Kwanini taarifa za kifo cha Rais walianza kupewa W/Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi na sio M/Rais?
Nadhani ilikuwa sahihi asipewe kwanza hizo taarifa za kifo Cha Raisi Makamu wa Raisi taarifa.Kwa kawaida kama keep kikao hata Cha uchaguzi wajumbe wanataka kumjadili mgombea ni kawaida kumtaka mgombea atoke Nchi wajumbe wamjadili bila yeye kuwepo.Sasa Makamu wa Raisi ndie mrithi wa kiti Cha Uraisi .Ilibidi mambo mengi ya kuhusu kurithi kiti ,taratibu za kuapishwa Kwake nk zijadiliwe na kupangwa tayari ili akitaarifiwa kifo Cha Raisi Kila kiti kiwe kimejadiliwa na kimepangika vizuri

Hebu fikiria anapewa taarifa halafu anakuwa sehemu ya mjadala Wengine Wanasema asiapishwe apewe mwingine mbele yake ni very embarrassing.Heri mivitano yoyote ilikuwa huko ndani bila kumhusisha Makamu wa Raisi ingeleta shida mfano mama angegoma kuwa sitaki kama Hali ni hii Nchi ingeingia kwenye mgogoro mkubwa wa kikatiba nk

Nilichoona kwenye Haya mahojiano inaonyesha yalikuweko mambo mengi muda mchache kuyaongea CDF ila Jeshi lilisimama kidete kuhakikisha mwishowe katiba inazingatiwa japo Kwa kuchelewa kinyume na masaa 24 ya katiba Inavyotaka

Yote heri tushukuru Mungu Nchi ilivuka salama
 
Mabeyoo..
Mungu akubariki kwa kulinda katiba pengine bila wewe saivi nchi ingekuwa vitani.

Vipi unaonaje twenzetu Ukraine kumsaidia Zelensky Maana vijana wa Putin wameanza kuharibu HIMARS, Mitambi ya kurusha Patriots, mpaka vfaru vya Abraham's M-1 vinateketea!
 
Hakuna anayebisha mtu kufa, ila kuna swali kwa kiongozi mkubwa kama yule, amekufaje?

Usanii kwenye mambo magumu haulipi. Au ndio nyinyi watu wema msiokufa?

Hata na tezi dume au covid au lolote lile lazima tutakufa.

General amefungua Pandora box. Muda utayamaliza hayo mengine.

Mimi sina lolote la ziada zaidi ya kujiuliza kulikoni
Mkuu huko mbele ya safari majibu yatatoka ....kufa ni lazima kwa binadamu ....
Lakini binadamu ndiye anaweza kujiondoa mwenyewe mapema zaidi kutokana na mazingira yake na kazi zake ...

Mfano MTU ni dereva ..akishika usukani lazima afikishe 180 ...kila siku na anaona furaha ...sasa hapo huyo dereva anaweka asilimia za karibu kufupisha maisha yake kutokana na mazingira ya kazi yake na mwendo hatarishi kila siku ..

Nimekupa mfano tuu .... Mazingira yanaweza kukupa stress ukapata magonjwa ya moyo...na kuondoka pasipo kutarajia ...

Japo najua lazima ushangae kwa bwana yule ....ni mazingira ya kazi ikamlazimu kupumzika
 
Back
Top Bottom