Yes ilikuwa interview nzuri sana kwa bahati mbaya sana walioendesha interview hawakuwa na weledi.
Laiti wangalikuwa nao tungejua mambo mengi sana
1. Wakati hali ya Mh Rais ikiwa mbaya kwanini Makamu wa Rais na Waziri mkuu hawakuitwa warudi Dar ?
Kwanini Makamu wa Rais na Waziri mkuu hawakuwepo kusimamia matibabu ya Rais. kwanini walikuwa ziarani?
Ilipofikia mahali Kadinali na Paroko wanaitwa, je, hiyo haikutosha kuwaita viongozi wakuu
2. Kwanini wakuu wa vyombo vya usalama walisimamia jambo hili bila kuwa na support ya Serikali
3. Kwanini Jenerali Mabeyo atafute taratibu ndani ya katiba wakati Mwanasheria mkuu wa serikali yupo?
4. Jenerali Mabeyo ametueleza mambo muhimu sana kuhusu Katiba. Kwamba nchi inaendeshwa bila muongo ndiyo maana kila jambo lilionekana kama ''novelty' na kwamba hakuna anayejua
a. Rais akiwa mahututi nani awepo nani aongoze nini
b. Rais akifariki taratibu gani zifuatwe kutangaza kifo, nani afanye hilo
c. Makamu wa Rais anaapishwaje na vitu kama bendera vinakuwaje
Ukimsikiliza Jenerali ni kama vile tuliongozwa na ''busara' na siyo taratibu ndiyo maana kuna wale waliotaka iwe tofauti kwasababu kulikuwa na mwanya huo. Tunatakiwa tukae chini hili halipaswi kuwa jambo la kubahatisha au kusema 'hatukuwa na experience'' hapana.
JokaKuu