Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Hapo kulikuwa na wavunja kabita na wafuata katiba ambao walikuwa wanaongozwa na CDF
Kwa hisani...Then my perception is nchi ilipinduliwa Kwa siku kadhaa ikarejeshwa baada ya kuapishwa Kwa Rais mpya....Maana Katiba ilikuwa clear kwamba Rais akishindwa majukumu ni Makamu ndiye Rais by default kama akienda nje ya nchi anapomwachia ofisi, Sasa CDF alikuwa ana amua wakati anayetakiwa kuamua akiwa Hana habari...Huoni hapo Kuna shida?
 
Kwa hisani...Then my perception is nchi ilipinduliwa Kwa siku kadhaa ikarejeshwa baada ya kuapishwa Kwa Rais mpya....Maana Katiba ilikuwa clear kwamba Rais akishindwa majukumu ni Makamu ndiye Rais by default kama akienda nje ya nchi anapomwachia ofisi, Sasa CDF alikuwa ana amua wakati anayetakiwa kuamua akiwa Hana habari...Huoni hapo Kuna shida?
Of course kuna shida, naona umeandika kitu ambacho sikuwahi kukifikiria, kweli nchi ilikuwa chini ya jeshi Kwa masaa kadhaa
 
Sasa kama unalijua Hilo,Kwa nini uone Magufuli as if hakustahili Kufa? Yeye alikuwa anaimiliki kesho? Muwe mnajifunza sio kusingizia wasiohisika na vifo.

Mtu mgonjwa wa Moyo miaka Mingi still was living a stressful life unategemea nini?

Hakuna anayebisha mtu kufa, ila kuna swali kwa kiongozi mkubwa kama yule, amekufaje?

Usanii kwenye mambo magumu haulipi. Au ndio nyinyi watu wema msiokufa?

Hata na tezi dume au covid au lolote lile lazima tutakufa.

General amefungua Pandora box. Muda utayamaliza hayo mengine.

Mimi sina lolote la ziada zaidi ya kujiuliza kulikoni
 
Huyu ndiye CDF wa hovyo kuliko wote kuwahi kutokea hapa nchini.

Kwanini hakumpindua dikteta jiwe, badala yake akamuacha aendelee kuteka, kupora na kuua watu?

Damu za watu wasiyo na hatia zinamlilia, ndiyo sababu anajuta kwa kulia hadharani.
 
Tuliongozwa na 'Busara' za Jenerali Mabeyo, kungeweza kutokea matatizo makubwa sana.

AG (Mwanasheria Mkuu) alitakiwa asimame kutafsiri na kuelekeza Katiba inatamka nini na kama haitamki kisheria kipi kinafanyika.

Makamu wa Rais alipaswa kuapishwa usiku saa 6 na si kusubiri siku 3 au kujiuliza viongozi watapokewaje.

Rais yupo mahututi yupo na CDF, IGP na DGIS , Makamu na Waziri mkuu wanahanja hanja! ni hatari sana.

Jamani tuacheni ubishi, tukaeni chini na kutengeneza katiba ili tupate sheria zenye miongozo
Kusema eti hatuna uzoefu kama Marekani si kweli. Tulitakiwa tutumie uzoefu wa Marekani kufanya vizuri

Ni kama vile 'tunajitahidi kutengeneza kompyuta yetu from the scratch ' badala ya kutumia zilizopo kupiga hatua

Hii interview imeeleza mambo mengi sana

Hii interview imekuja wakati muafaka. Anayedhani amesimama, aangalie asianguke
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=9Hyg_T0yb-8

Katika dunia hii mtu wa mwisho ambae unaweza kuona chozi lake hadharani ni senior army officer na army general ndio kabisa awezi kuonyesha weakness hiyo hadharani.

Sasa cha kushangaza Mabeyo pamoja na kujitahidi kutabasamu ila chozi lilimshinda nguvu kwa sekundę kadhaa ameonekana akibubijikwa machozi ya hudhuni mbele ya camera. Kumbuka ata alipofiwa na mtoto wake rubani, general akutoa chozi alipofika eneo la tukio.

Je anajutia kutosikiliza maamuzi ya watu waliomshauri wapindue męża ya katiba huyo mama hiyo nafasi sio size yake na kinachoendelea leo Tanzania.

Alishindwa kuweka uzalendo akazidiwa na Msoga
 
Back
Top Bottom