Chukua hii: 2022 ujio wa Tundu Lissu utaleta Kimbunga

Nawashangaa watu wanaochukulia kama vita. Hata Bideni anapingwa wazi wazi na anaendelea kudunda.

Ni mambo ya kawaida.

Kiongozi na chama chenye uwezo huwezi kuona wakiogopa kupingwa, ila wenye uwezo duni na ushawishi hafifu hawako tayari kupingwa.
 
Siku zote umekuwa very NEGATIVE kwa nchi yako. sijawahi ona msg of HOPE from you
 
Mkuu hoja zako zimekaa vizuri ila kwamba wazungu wamemwandaa Lisu Kuna kitu wanataka kuchukua si kweli kwani chini ya CCM kitu Gani wameshindwa kuchukua hao wazungu?
 
Mtu yotote anaye mshabikia Tundu Lisu ni wa kupimwa akili

Ana ushawishi wa wazi, ni karma automatic toka kwa Mungu. Iwapo Tundu Lisu asingerejea uchaguzi wa 2020, uchaguzi ule usingekuwa na msisimko ilioupata dakika za mwisho, wala usingefikisha hata hao wapiga kura wachache waliojitokeza. 50% ya wapiga kura wachache waliojitokeza, walifanya hivyo kutokana na hamasa ya uwepo wa Lisu. Hali ile ndio ilichangia Magufuli kuagiza mchakato wa uchaguzi uporwe, maana aliona aibu kwa matokeo yaliyokuwepo.
 
Siku zote umekuwa very NEGATIVE kwa nchi yako. sijawahi ona msg of HOPE from you

Vumilia tu huu ndio ukweli uliopo hata kama huupendi. Sina tabia ya kutoa mawazo positive ya kuhadaa watu. Kilichopo ni negative, hivyo nikiaddress kama kilivyo na sio kinyume chake.
 
Mkuu hoja zako zimekaa vizuri ila kwamba wazungu wamemwandaa Lisu Kuna kitu wanataka kuchukua si kweli kwani chini ya CCM kitu Gani wameshindwa kuchukua hao wazungu?
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Hii ni roho ya kuku...acha woga wa kibongo mkuu.
Samia akifanya vizuri atasifiwa, akikosea atakemewa regardless alimsslimia au la!
Hiyo ndiyo roho ya Bata kunya kunya tu hovyo
 
Pascal Mayalla wewe unawaza uchaguzi 2025 (unawaza cheo)wakati Lissu yeye anawaza hatma ya uhuru wa demokrasia wa Tanzania ya sasa na sio kutamani cheo.
Lissu anawaza uhuru wa leo wa wanaonyanyasika kwa kukosa haki akiwemo Mwenyekiti wa chama chake Freeman Aikael Mbowe.

Hisia zimekufanya uzuge kuwa humjui Lissu mliyemshindwa kwa hoja miaka kadhaa kabla ya uchaguzi hadi mkammiminia risasi 19 kama mnauwa tembo.

Inshort humjui Lissu ama umeamua tu kuzuga kuwa humjui Lissu.
Huyu mtu ni wa moto mwanzo mwisho ndiyo maana ngosha mwenzako alijaribu kumjibu kwa risasi za moto ambazo nazo hazikufua dafu.
 
Sikusililiza hotuba yake, anasema anarudi lini Bongo?
 
TL inabidi aachane na tabia ya kutumia lugha isiyofaa wakati wa uwasilishaji wa ujumbe wake pia ajiepushe kujiona mtu anayejua sana kuliko wengine wakati siyo sahihi

Pia ajifunze kuwa na busara na hekima
 
TL inabidi aachane na tabia ya kutumia lugha isiyofaa wakati wa uwasilishaji wa ujumbe wake pia ajiepushe kujiona mtu anayejua sana kuliko wengine wakati siyo sahihi

Watanzania hasa upande wa CCM waache kuwa na hali inayoitwa homo sovieticus yaani kujishuku kuwa wanatumia lugha isiyofaa kwa viongozi wanaotawala kwa mabavu huku ukichunguza maneno yaliyotumika hayana tusi, hayaudhi wala kunyanyapaa bali yanaelezea hali halisi ya kisiasa iliyopo. Huwezi kuwafundisha raia namna ya kuzungumza wala kuwashurutisha maneno gani wayatumie.
Mfano hotuba hii ya Tundu Lissu ya kufunga mwaka 2021 haina neno lolote la tusi pia hata maoni ya wanaCCM kama spika Job Ndugai kuhusu mzigo wa madeni na nchi kupigwa mnada haina ma neno yeyote unayoweza kuyaita matusi au lugha isiyofaa. Nashangaa wana CCM tayari wapo katika taharuki kubwa kumshambulia mwenzao Spika / Mbunge Job Ndugai wakati alikuwa anatoa mawazo yake tena kwa lugha safi tu ya kisiasa.


Dokumenti ya kijani : GRIN - The homo sovieticus mentality. The failure of socialism and its consequences.

Introduction

1. How the homo sovieticus originally was conceived

2. How did the homo sovieticus come into being?
2.1 The functioning of an ideology
2.2 How the communist ideology shaped people’s minds
2.3 How economic issues and consumption were conceived
2.4 How the concept of freedom was conceived

3. The consequences of this probihiting of every individual initiative and the denial of individual freedom.

4. The β€œcaptive mind” mentality and the culture of fear

5. Political consequences till today

6. The legacy of communism in the Constitutions of the New Democracies of East-Central Europe.

7. The homo sovieticus in some East-Central European countries and Russia:
7.1 The homo sovieticus in the Czech Republic
7.2 The homo sovieticus in the Russian Federation
7.3 The homo sovieticus in Poland
7.3 1 The position of the Church in Poland
7.3.2 Politics in Poland as the pendulum swinging between AWS and SLD.

8. Constradictions between East and West

9. Some words about Polish love relationships Conclusion

Bibliography : GRIN - The homo sovieticus mentality. The failure of socialism and its consequences.
 
Kama ni kweli unachokiongea sasa mtifuano ndani ya CCM unasababishwa na nini kama siyo udhaifu wa kiutendaji wa mama mwenyewe?.
 
Pascal Mayalla wewe unawaza uchaguzi 2025 na hatma ya uhuru wa demokrasia wa Tanzania ya sasa.
Lissu anawaza uhuru wa leo wa wanaonyanyasika kwa kukosa haki akiwemo Mwenyekiti wa chama chake Freeman Aikael Mbowe.
P
 
Tundu lissu akija atampelekea mama Moto hatari..wananchi wengi hawaipendi hii serikali kutokana na utendajiwa mama ktk tozo,suala la machinga,hali ngumu ya maisha,wizi na ufujaji kushamiri, Mambo ya ajabu ajabu yamerudi...akitoke mpinzani strong lazima mama aondoke..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

..wapinzani hawawezi kukosa point kwasababu changamoto haziishi ktk jamii yoyote.

..watawala wanatakiwa wakumbushwe na kusumbuliwa wakati wote ili watatue changamoto nyingi inavyowezekana.

..kama wapinzani wapo hata ktk nchi zilizoendelea, na wanakosoa na kusimamia watawala wao, kwanini wasiwepo Tz nchi ya dunia ya tatu?

..kama unaona serikali ya SSH haijihusishi na kashfa, na itatatua kero kwa haraka, basi huenda sababu ni kuogopa makelele ya wapinzani ikiwa jitihada za kuleta maendeleo zitadorora.

..kwa hiyo ni muhimu wapinzani wawepo. Na ni muhimu zaidi wakiwa imara na huru kufanya shughuli na harakati zao.
 
Kwani wakigawanyika ndio wanashindwa kupatana kwenye ishu ya maslahi ya chama Chao?
 
Unabeti sio? Lisu ampelekee Rais moto? Mbowe anampelekea mama moto? 😁😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…