Airport wanawapima joto tu.
Yes nafahamu. Je, ina maana yoyote ile katika hali inayoonekana?
Hoja yangu ni moja,kwamba, kupima joto ni sehemu tu lakini haikuwa njia ya kubaini tatizo.
Viongozi wetu waliamini kupima joto kutasaidia na hivyo kuacha watu waingie tu hata wanaotoka 'hot spot'
Kilichotakiwa ni kujua msafiri na historia yake, na akiingia anakuwa chini ya karantini iwe ''self isolation'' au ya lazima.
Tulikuwa na fursa ya kufunga mipaka mapema, hakufanya hivyo, tunageukia shule na vyuo ikiwa too late
Tulikuwa na muda mwingi sana wa kujiandaa, hatukuutumia vema kama kawaida yetu.
Hofu, tunaelekea majira ya baridi Tanzania, na Covid inastawi vema katika hali hiyo.
Ukichanganya na udhaifu wa healthcare system na social distancing ya 0 katika dalaladala, tujiandae kwa tatizo kubwa.
Tumepoteza muda, hatukujifunza na hatukutumia fursa ya kujifunza na kujiandaa.