Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Matumizi yako yanaendana na kipato chako, kunawengine wapo town, matumizi per month ni bajeti yako ya Vocha.
 
Tutafute hela tu.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
JF kila mtu matawi..et natumia 15k kwenda kazini na kurudi mara chache dalaladala huwa natumia daladala..humu mnatupanga sana kama una uwezo wa kutumia 15k unalalamika nini hiyo nauli? Au ndo kipato chako laki 2.5 unajifanya unasemea wengine?
Wewe kwa siku unatumia kiasi gani cha pesa?
 
Kweli mkuu mfano watumishi wa umma wanaoishi mikoani haswa miji midogo huwa wana nafasi ya kufanya maendeleo kuliko walio mjini kutokana na gharama za maisha
Ni kweli.

Mara nyingi miji midogo ipo karibu na mashamba ambapo vyakula ni rahisi sana.

Kuna mtumishi alihamishiwa mji mdogo akitokea Jiji: alilalamika sana, ila alipofika kule akahamasika kulima.

Sasa hivi hataki kusikia kuhamishwa toka huo mji mdogo.

Nimeishi miji ya Kibaya (Kiteto), Kisarawe, na Kibaha. Ukweli usemwe tu watu wa huko ni 🔥
 
Sema na kuishi mbali sana jau,
Hapo mkuu kama hio ratiba ni kweli nakuonea huruma,

Sometimes tunakimbilia viwanja vya bei rahisi ila mara mia ulipe pesa kubwa upate sehemu nzuri sio kujificha huko porini.
Kuna jamaa alikataa kununua kiwanja tabata mwaka 1992.......leo?
 
Hata ukilaumu hakuna wakujibu au kutatua changamoto yako, Hata wapinzani sio wapinzani wa kweli.. labda Tuanzishe chama chetu cha siasa.. cha JF
 
Ombeni uhamisho mkoani kwa pesa hiyo unafanya vitu vingi vya msingi ikiwemo uwekezaji mkuu
 
Mashambani kazi zimejaa hamtaki.
  • Je Uma maanisha vibarua vya mashamba ya makampuni ambavyo hulipa 5,000/- kwa siku inayoanza saa 1 mpaka 10 jioni?
  • Kama ni mamba ya kujilimia, kilimo si kazi lelemama kama wengi wanavyodhani.
  • Ushauri wangu: Ni vyema kijana kwenda mji mwingine wenye ahueni ya maisha - hasa miji ya mipakani - akaendeleze pambano huko.
 
Mkuu ukiwa unatafuta maisha , lazima uhakikishe kwa namna yoyote unajibana , ukipiga andazi la Mia 500 sidhani kama utakufa.

Kama haujatoka familia zenye uwezo unatakiwa uishi kibabe sana kutoboa.
Mwana wewe ni hustler nakumbuka zama zangu najitafuta nishapiga sana Andazi chai mchana siku Mambo yakiwa poa tunapiga menu CBE pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…