DC Albert Msando: Gwajima ajitokeze alipojificha aelezee umma kilichotokea

Gwaji boy aliwezaje kutoka pale kwa ule wingi wa Polisi waliozagaa pale kanisani ? [emoji2]
Gwaji boy alipenyezewa taarifa mapema akasepa usifikiri humo kwa wenye mamlaka hakuna anaeungana na jasusi la mbinguni

kama tu ndani ya selikali kuna wanaompa taarifa kimambi aje akoswe gwaji boy taarifa ya nini kinaendelea

Unaambiwa jasusi lilijirekodi eti nipo kanisani saa tano za usku tumezingilwa na polisi kumbe hakuna lilisepa mapema ndipo likaenda kujirekodi kwingine na maaskofu feki
 
Huyo msando kumbe hana akili kiasi hiki! Hivi anaweza kutuambia Mdude alikuwa na kosa gani? Anaweza kutiambia Kibao alikuwa na kosa gani?

Kuna watu ukiwatazama wanaonekana wana akili, kumbe wakirushiwa kacheo kadogo tu, akili zote zinapotea, zinahamia tumboni, kisha wanazitupa chooni. Msando ni miongoni.
 
Wewe umejuaje kama wale wote ni Maaskofu feki au original ? Au wale original kwa kuwa walikupanda ndio maana umeweza kugundua kwa uharaka zaidi kama wale ni feki
 
Viongozi wengi vijana wa CCM wangejifunza kwa Anthony Mtaka
 
Wewe umejuaje kama wale wote ni Maaskofu feki au original ? Au wale original kwa kuwa walikupanda ndio maana umeweza kugundua kwa uharaka zaidi kama wale ni feki
Taarifa za kupenyezewa yaani hii ni asst nmeiunga golini mazima
 
Huyu naye ana LLB eti, elimu yetu inahitaji overhaul kubwa sana yani! Either tuiboreshe au tuanzishe mtaala rasmi wa degree ya Uchawa (Masters au Bachelor au hata post graduate diploma) maisha yaendelee tu
 
Jasusi la mbinguni si alisema maombi ni siku 7
 
Haka ka jamaa bana, yaani ajikokeze kwa wafilisti wamle nyama.
 
Hahaha wasiojulikana wanaanza kujitokeza.

Kumbe hawakumpata Licha ya kuzingira kanisa usiku kucha?

Kwanini yeye asitueleze tu, ni nini kilitokea?
 
Hahaha hawa watu wakipata vyeo huwa wanajiona ni zaidi ya malaika.

Kila wafanyacho wanakiona kiko sawa kabisa.

Ukipeleka barua ya kumuita si unamsubiri aje kituoni au barua huwa inataka afike muda huo huo?

Barua unapeleka jioni na polisi wanafuata nyuma kumkamata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…