Erdogan azitaka nchi za kiislamu kuungana dhidi ya taifa la Israel

Huu ni ubaguzi wa kidini. Watu wanaopinga udhalimu wa Israel si Waislamu tu. Sasa yeye kwa kusema hivyo anaonesha kama hii ni vita ya kidini kati ya Waislamu na Wayahudi.
Unaakili nyingi sana mkuu. Hongera. Ingawa kwa kutumia akili umepotoshwa kwa habari ya uwepo wa Mungu kwa kuwa mambo ya Mungu yanahitaji akili na imani zaidi. Ni ombi langu kwa Mungu kwamba siku moja ajifunue kwako kama alivyojifunua kwa Sauli/Paulo. Barikiwa sana.
 
Huu ni ubaguzi wa kidini. Watu wanaopinga udhalimu wa Israel si Waislamu tu. Sasa yeye kwa kusema hivyo anaonesha kama hii ni vita ya kidini kati ya Waislamu na Wayahudi.
Ni lini waislamu hawajawa wabaguzi?
Asili yao ni ulalamishi na ubaguzi.
Huyo kaongea vile tamaa ya waislam ilivyo. Wao ndio wao.
S.A watajuta kwa kujipendekeza.
 
Anaweza yeye kuwaachia Antokia Instambul Waitalia Roman eneo lao, anaweza kurudisha maeneo yote ya wakurdi? Anaweza rejea kwao maana Yete na wenzie sio Waturkish original.. pumbavu zake..
 
Hizo nchi zenyewe za Kiislamu zinaongozwa na viongozi wakiambiwa wachague upande wa Marekani au Palestina watachagua Marekani.... maana ndio main sponsor wao. Egypt angeweza kuikomboa Palestina, lakini it is not in their leaders interest
 
Kwa maoni yangu:
Ni kama vile anawaamsha "Waislamu" kutoka katika usingizi wa pono. Nchi za kiislamu ziache kulala. Nchi kutoka maelfu ya kilomita (South Africa) isimame kidedea against Israel alafu majirani wameuchuna. 🤔🤔🤔
Hii ni issue ya kuiunganisha dunia nzima dhidi ya Waisraeli, si issue ya kuweka mbele Uislamu na kuugawa upinzani dhidi ya Israel kwa misingi ya kidini.

Kwa kauli hizi kuna watu wataaminishwa hii ni vita ya kidini, Waislamu wanataka kutawala dunia, unaona wanaitana wao kwa wao tu kumpinga Mu Israeli?
 
Kwa nini unaona Uislamu ni issue wakati hapa kuna violation za human rights ambazo mtu wa dini yoyote na mpaka asiye na dini anatakiwa kuzilaani?

Mtu akionewa kaonewa tu, hayo mambo ya kuitana Uislamu maana yake nini? Maana yake hili jambo la Waislamu, wasio Waislamu wasiingilie?
 

Kuomba kwako pia kunathibitisha Mungu hayupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo kusingekuwa nan haja ya mtu yeyote kuombe chochote.

Ukiona mtu yeyote anamuomba Mungu ujue huo ni uthibitisho kwamba huyo Mungu hayupo.

Angekuwepo, kwa sifa zake hizo za ujuzi wa yote, uwezo wote na upendo wote, angewapa waja wake wote mahitaji yao yote mazuri kabla hawajamuomba, na yasiyofaa angewanyima hata uwezo wa kuyajua was8ngeweza kuyaomba.

Umeelewa?
 
Awatume Ertugru bey, Osman bey na Alpaslan bey wakamkate mapanga Netanyau
 
Ni lini waislamu hawajawa wabaguzi?
Asili yao ni ulalamishi na ubaguzi.
Huyo kaongea vile tamaa ya waislam ilivyo. Wao ndio wao.
S.A watajuta kwa kujipendekeza.
Hili si suala la Waislamu, ni suala la kuvunjwa haki za binadamu.
 
Hili si suala la Waislamu, ni suala la kuvunjwa haki za binadamu.
Edogan kasema waislamu waungane kupinga hilo. Na hata Iran pia aliomba nchi za kiislamu ziingilie kati.
Wewe ni nani hadi uone sio suala la waislamu?
Wao wanaona ni suala la waislamu, kinyume chake mtakuwa mnajipendekeza tu.
 
Nikisema wewe hakuna unachojua nitakua nakosea!??
Hao BRAZIL,SPAIN,COLOMBIA,MEXICO,BELGIUM wote walifanya maamuzi baada ya kuona kilichofanyika na kilichosikika Arab peace summit.
Arab peace summit walihudhuria takriban MATAIFA YOTE YA G20 ikiwemo South Africa.
Kiongozi wa Brazil,Spain,Colombia n.k n.k wote walihudhuria,na wakatoa risala zao na maoni yao ya nini kifanyike juu ya mzozo wa Israel dhidi ya Gaza.
Na katika hiko kikao Elsisi na viongozi wengine walionesha ushahidi na mlolongo mzima wa kilichotokea Gaza kuanzia August mpaka kuja Oktoba 7.
Pia wakajadili mzozo kuanzia 1947 ilipochorwa mipaka ya Israel na Palestina kuja mpaka mipaka ya sasa ya Palestina iliyodhulumiwa.
Hadi ANTONIO GUTTERES GS wa UN alihudhuria.
Ndipo alitoa tamko UN security council akisisitiza kuwa"the cause of conflict is not October 7,this did not start October 7".
Asingeongea haya kama asingehudhuria Arab peace summit na kusikiliza na kuoneshwa ushahidi na WAARABU wenyewe kuhusu mzozo wa Gaza.
Na kikao kimoja cha mwisho kilifanyika wakati wa kutoa tuzo za UNRWA,kilifanyika DOHA QATAR.
Sheikh Tamim Al Thani alitoa hotuba ya wito wa mataifa yote kuungana na Palestina.
Hiko kikao viongozi wa mataifa ya EU walihudhuria akiwemo waziri wa haki za kibinadamu wa SPAIN.
Baada ya hapo ndipo mataifa yakaona alichofanya Israel ndio wakachukua hatua.
Kama isingekua WAZUNGU NA SOUTH AFRICA kuhudhuria Arab peace summit basi wasingejua ukweli uliotokea Gaza na wasingekua na mwangaza wa kufungua kesi na kwenda kinyume na Israel.
HUO USHAHIDI ALOTUMIA S.AFRICA KWENDA ICJ ALIUTOA ARAB PEACE SUMMIT.
Au wewe ulidhani kisa ni Arab peace summit basi walihudhuria mataifa ya kiarabu peke yake!!??
Hadi viongozi wa Botswana walihudhuria.
Walichofanya waarabu ni kumpa mbwa jina baya kwanza,walitumia mlengwa wa kisiasa ama kidiplomasia kuionesha dunia Israel ni taifa la namna gani,na hiyo imelipa.

Kiufupi Arab Peace Summit ndio iliyowaamsha South Africa na mataifa mengine kwenda kinyume na Israel.
Bado mweupe kuhusu huu mzozo wa middle east hujui siasa za dunia zinaendaje.
 
Pia cha kukuongezea kitu kimoja.
Kikao cha mwisho pale Misri cha peace summit King Abdullah wa Jordan alitamka kuwa ili huu mzozo uishe two state solution ndio suluhisho.
Mengine aliyoongea UN general secretary katika vikao vya UN security council ni matokeo ya alichokipata Peace summit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…