Inasikitisha sana.
Iangalie Italy,....iangalie Spain, UK, USA, Afrika ya kusini na hata jirani zetu Kenya hali inatisha na sisi siyo kisiwa.
Hata Corona ikimalizwa leo bado maumivu ya uchumi tutakayokutana nayo huko mbele ni makubwa kuliko watakayokutana nayo Spain au UK.
Tulioishi wakati wa vita vya Kagera tunakumbuka namna ile miezi 18 ya kufunga mikanda tuliyoahidiwa ilivyogeuka kuwa miaka 18
Pia tunakumbuka tulivyokula ugali wa njano mahindi yakitoka Brazil na tulivyokunywa uji wa chumvi na kufulia majani ya mpapai.
Ninaamini wanaochukulia kama mzaha mtoto wa Mbowe kuugua Corona ni watoto wadogo kama huyo mgonjwa lakini watu wazima tunapaswa kukemea.
Mungu hapendi dhihaka na kamwe tusiifananishe Corona na Siasa, tutajutia.
Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka.
Maendeleo hayana vyama!