Familia ya Freeman Aikaeli Mbowe yathibitisha mwanafamilia kuwa na Corona

Familia ya Freeman Aikaeli Mbowe yathibitisha mwanafamilia kuwa na Corona

Nyinyi ndiyo mankers nyuzi za kuigawa nchi Katikati ya janga la corona
 
Kwahiyo Corona imekuja Tanzania simply because Technically aliombea ije?!

Wakati mnaambiwa ndege toka China bado zinatua kwenye viwanja vyetu mlichukua hatua gani?

Tanzania inawezekana ndio ilikuwa nchi ya mwisho kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya Corona, hapa Mungu hausiki, ni uzembe tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuache kutishana rais wetu kisha sema. Corona itakuja itapita.Muhimu tuwakinge wazee wetu na wale wenye upungufu wa kinga. Wengi wetu tutaishi nao kama mafua ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kufikiri kwa kiwango cha chini kabisa.......sasa hawa ndiyo watunga sera za CCM ...duh!! no wonder Membe hajuti....!!
 
hii corona mm naona ipo kwenye media hasa huku mitandaoni tuu, nimepita dar jana watu hawana habari kabisa wanachapa kazi! Acheni kupeana presha kijinga.

Capo Dei Capi
 
Inasikitisha sana.

Iangalie Italy,....iangalie Spain, UK, USA, Afrika ya kusini na hata jirani zetu Kenya hali inatisha na sisi siyo kisiwa.

Hata Corona ikimalizwa leo bado maumivu ya uchumi tutakayokutana nayo huko mbele ni makubwa kuliko watakayokutana nayo Spain au UK.

Tulioishi wakati wa vita vya Kagera tunakumbuka namna ile miezi 18 ya kufunga mikanda tuliyoahidiwa ilivyogeuka kuwa miaka 18
Pia tunakumbuka tulivyokula ugali wa njano mahindi yakitoka Brazil na tulivyokunywa uji wa chumvi na kufulia majani ya mpapai.

Ninaamini wanaochukulia kama mzaha mtoto wa Mbowe kuugua Corona ni watoto wadogo kama huyo mgonjwa lakini watu wazima tunapaswa kukemea.

Mungu hapendi dhihaka na kamwe tusiifananishe Corona na Siasa, tutajutia.

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Sky Eclat, Je, ni wangapi katika familia wameambukizwa? Ni hatua gani walizochukua mapema huyo mtoto asiwaambukize na wao wasiwaambukize wengine.
 
Je, ni wangapi katika familia wameambukizwa? Ni hatua gani walizochukua mapema huyo mtoto asiwaambukize na wao wasiwaambukize wengine.
Mama yao ni daktari ana fahamu hatua za kuchukua.
 
Bashite niwakupeleka ICC maana vyombo vya ndani vimemshindwa.
Mkuu si uliomba ugonjwa huu ufike Tanzania na kuna jamaa alihoji kama ki akili uko timamu? We ukasema jamaa alipewa mshiko na mamvi. Na ukadai utamvua nguo hadharani! Sababu unayafahamu maskendo yake kibao.
 
Mama yao ni daktari ana fahamu hatua za kuchukua.
Ingawa mama ni daktari, taarifa ya Mbowe inaashiria kuwa uwezekano ni mkubwa kwa mtoto kuwa amewaambukiza wanafamilia kabla ya kungundulika na wao kuwaambukiza watu wengine. Taarifa hiyo inasema:

... ni kweli mwanangu Dudley amethibitika kupatikana na virusi vya Corona baada ya kupata homa za vipindi, kuumwa kichwa mfululizo na kukohoa kwa siku tano.

Mama yake, ambaye ni Daktari alipobaini hali hiyo alizitaarifu mamlaka za Serikali zinazoshughulikia Janga hili nazo zilimtaka kijana apelekwe Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam kwenye vipimo zaidi ambapo ilithibitika rasmi kuwa ana virusi vya Corona
 
Kwa majina anaitwa James ambowe

Kama mnavyo fahamu ndugu zangu Watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam leo afajiri aliamkia kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo. Na akawa anazungumza na abiria wanaokwenda mikoani. Lakini Jambo la kushangaza ambalo ninaamini hata nyinyi Watanzania limewashangaza ni la bwana Makonda kujivika usemaji wa familia.
Bashite ni mke mdogo wa mbowe ndio kajiteua kua msemaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom