Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Maelezo ya mwisho wamesema watapewa wahusika pande mbili (Feisal na Yanga)

Sasa ungeelewa hoja yangu umezungumzia TFF kuwasilisha public kama ilivyofanya kwenye kesi zingine ambazo ilialika hafi waandishi wa habari kuuliza na maswali basi usingeandika hivi ulivyoandika.
EBHANAAE...UNACHOSHA KWELI...WEWE MBONA UNAKAZA SHINGO HIVYO...TOKA PAGE 1 MPAKA SASA YA 9...UPO PALEPALE ...BORING...KAKUSANYE WEWE WAANDISHI UWASIMULIE MAAMUZI YAKO NA FAMILIA YAKO...
 
Usiri wa mkataba ni wewe mchezaji kuto leak taarifa za mkataba kwenye taasisi nyingine au sehemu nyingine

Usiri wa mkataba hauzuii watu kujadili yale yaliyokiukwa ndani ya mkataba

Nitajie mfano wa kitu gani ambacho kinafichwa kwenye mkataba hakijulikani

Au ndio huwezi kwasababu hakijulikani?

Okay sasa hayo unayoyasema wewe kuhusu kutoshiriki matangazo ndio yale ambayo yanakuwa siri kati ya mchezaji na Club kwamba hatakiwi kwenda kutangaza nje

Ila ikitokea mgongano wa jambo hilo akalazimishwa kufanya matangazo unafikiri watasema Yanga imekosea bila kutanabaisha wamekosea wapi kwasababu hicho kitu ni siri?

Tuna mifano mingi sana kama hiyo na mwisho wa siku lilipokuja swala la mahakama kila kitu kilikuwa wazi
WEWE JAMAA MBISHI ..UNAONGEA UTUMBO MAHARAGE ..LAKINI MWENYEWE UNAJIONA UNA HOJA KWELI...
 
Akili ndogo zilikua zinadai jamaa alikua sahihi kuondoka maana amesharudisha fedha.

Kwani kila mxchezaji akitaka kuondoka kama Fei itakuaje katika vilabu vyao? Éti usiporidhika na mshahara unaondoka

Hivi akijitokeza mtu mwenye uwezo wa kuwapa hela wachezaji kama watano waondoke kwenye klabu moja kwa mtindo wa Fei itakua kuna mpira tena?
Mbona jamaa alinikumbusha enzi za wanasiasa kuunga juhudi mkono. Chama kinalala na wabunge ishirini kinaamka na wabunge pungufu kisa hamahama?
Mimi sijui sheria ila nimetumiatu akili ya kawaida nahakuna klabu itakayokua dhaifu kiasi hicho.

Afanye ushawishi na sio kuondoka kitoto
Alafu kuna mijitu inaforce yanga imuonee huruma...imuache aende atakapo kirahisi tu...
 
Nendaa kwenye case hiyo kaitaje Azam na Yusuph [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mmevurugwa vibayaas, kwan ulaya ipi unasema wee

Neymar aliendaje PSG kutoka Barca?
Nani kavurugwa mpaka sasa,tokea alivyo ondoka na sasa ww unaona kunautofauti Yanga.

Aliondoka ila kwa kukaa na Barca au kamu unajua tofauti ni juavyo niambie.
 
Haya uliyoyaandika ni kama mtu ambaye hajafatilia hili sakata

Ni mara ngapi waandishi wa habari wamefata wakili wake kuhoji kuhusu kuridhishwa na maamuzi ya TFF na yeye akasema hajafurahishwa akitaja na sababu?

Na ndio sababu ya watu kuanza kutilia shaka swala hili

Unajua uovu wote unafanyikia gizani

Kwanini kesi zingine zimetolewa ufafanuzi halafu hii imewekwa kizani? TFF ina maslahi gani na hii kesi?
Hawakuridhishwa si wakaomba review na jana ndio review ikafanyika na Feisal akaona umuhimu wa kuwepo Fatuma Karume katika upande wake. Baada ya review je Fatuma Karume hakukiri kuwa ameridhika na mchakato?
Wewe unataka isiwe gizani kwani kesi inamuhusu kila mtu? Waliopelekeana kwenye sheria ndio wamejadiliana vifungu vya sheria.
 
Anapewa mil 4,anakula ugali na chumvi then alikuwa na uwezo wa kulipa 110m Yanga bila kufuata utaratibu na kwenda Dubai kutrain na trainer mkubwa anao watrain wachezaji wanaocheza ligi kubwa ulaya.

Hamna logic kabisa, bi mkubwa alizani ana mtetea mwanae kumbe kamwaribia.
Wengi wanailaumu Yanga badala ya anayempa hela kumdanganya,ametoka Singida united akawa anapata 1.5m,2020 akaboreshewa kuwa 4m mpaka 2024,amepata umaarufu kidogo anaanza kudanganywa kijinga jinga tu,na saizi thamani yake inazidi kushuka,labda hao Azam wao kwasababu hawana jipya watamchukua tu baadaye ila acha aonje joto la jiwe
 
Hapana. Ila Swali langu limebase kwenye kumlipa mchezaji ambaye hata mazoezini haji. Au hatolipwa?
Yeye ndio atailipa yanga fidia kwa kutoonekana kambini kwa mda mrefu sana, asilolijua wanamlia timing tu...
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo tarehe 2 Machi, 2023 kwa ajili ya kusikiliza pamoja na mambo mengine shauri la mapitio (Review) ya uamuzi wake wa tarehe 9 Januari 2023 kati ya Feisal Salumu na Klabu ya Young Africans kama yalivyowasilishwa na muombaji Feisal Salum dhidi ya Klabu ya Young Africans.

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi

Kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali hivyo imetupilia mbali shauri hilo.

Sababu kwa undani za uamuzi huo zitatolewa kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo siku ya Jumatatu 6 Machi, 2023.

View attachment 2535208
Hili Sakata limeshusha hadhi ya Shangazi Fatuma Karume, pamoja na kutua TFF kwa mbwembwe hatimaye mteja wake kaangukia pua
 
Swala la kuvunja Mkataba sio utovu wa nidhamu. Kajifunze hilo kwanza

Mahakama ikishaamua kwa kutoa hukumu lazima hukumu ifanyike kupitia mamlaka za kimahakama na sio uongozi wa Club

So kama Feisal amegundulika kafanya kosa kuvunja mkataba basi mahakama ndio yenye wajibu wa kutoa adhabu na sio Yanga.

Yanga sio mahakama mpaka itoe hukumu na ndio maana nimekuuliza kwenye ishu ya Morrison uliona Club ndio iliyotoa hukumu ya faini au ni Mahakama?
Itoshe tu kusema wewe ni Mbumbumbu ulie shindikana hautibiki

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Haipo hivyo

Ukisema hivyo utajikuta unawakataa hata mawakili wanaomtetea Feisal kwasababu nao hawahusiki kwenye mkataba wa Yanga na Feisal ila wapo

Point yangu ilikuwa kuonesha msimamo wa mzazi kumuwakilisha mwanae

Yani alichokisema mzazi ndio kile ambacho Feisal anakiamini. Kwa hiyo hoja yako ya kusema Feisal hakutoa idhini sidhani kama itakuwa na mashiko kwasababu tukisikiliza kauli ya mzazi wake pamoja na wakili wake wote walitaka hili jambo liwe public
Hivi wewe shule ulienda kusoma nini? Mama yake Feisal kwenye hii kesi anahusika kama nani kiasi kwamba akisema kitu kufuatwe?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hebu tukubaliane kutokukubaliana kwenye "usiri wa mkataba". Nataka nikuulize, kwanini wanaolalamika kwamba TFF wanafanya siri ni mashabiki wa Feisal badala ya Feisal na wakili wake?
Na mama yake ni shabiki?
 
tulisema dogo anajiharibia mkabisha sasa ni zamu ya yanga kuamua wamfanye nini
 
Back
Top Bottom