Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Hakuna kitu kama hicho, wakina Shafii Dauda wanafungiwa kila kitu kilikuwa open

TFF ndio chombo kinachohitajika kufanya hayo yote kuweka kila kitu bayana, hizi habari za kusema wahusika hivi wahusika vile inaongeza mashaka kuwa maamuzi yaliyotolewa hayakuwa fair.
 
Yanga timu yangu pendwa, muachieni kijana aende zake pale nafsi yake inapomtuma, fei amekosea dhahri lakini kukosea kwake isiwe kigezo cha kumkomoa kijana huyu na kumuharibia maisha na kumuumiza kisaikolojia, fanyeni wema huo, aende zake huku mkimpa onyo.
 
Faini yenye faida kwa timu anayochezea?
Unapigwa na TFF sababu wao ndio wenye mpira wao na Yanga ni mwanachama wao.

Kwanza tushukuru tu Tz sio kama ulaya ila mbele ,wasingeishia hapo ,wangetrace ile mil 110 imetoka kwa Fei au kwa timu nyingine.

Tunajua nyuma hili sakata yupo Azam na Yusuph, sema kibongo bongo hili hatuto lifuatilia.
 
Biashara haina huruma mkuu ukifanya biashara kwa kuoneana huruma utakufa masikini, unamkumbuka singano wa simba jinsi alivyowasumbua na kesi yake ya madai???
 
Mahakama gani umewahi kuona inaweka mwenendo wa kesi gazetini zaidi ya hukumu? Mbona mnajitoa ufahamu kama watoto?
Mchanganuo wa hukumu mbona unawekwa wazi

Hata kesi ya mbowe mbona watu tulikuwa tunajua kila nukta inayoendelea, hata jaji akikohoa tunajua
 
Mchanganuo wa hukumu mbona unawekwa wazi

Hata kesi ya mbowe mbona watu tulikuwa tunajua kila nukta inayoendelea, hata jaji akikohoa tunajua
Mahakama ipi uliona inaweka mwenendo wa kesi ya Mbowe zaidi ya Martine Maranja Masese ambaye ni mwanachama wa CHADEMA? Wewe ukajua Jaji ndo alikuwa anaandika mitandaoni?
 
Kuna watu Wana viwango vya chini vya uelewa mpaka unashangaa wanatembeaje barabarani bila kugongwa na magari.
Wewe na Uyanga wako jikite kwenye hoja achana na mipasho ya kimhemko haikusaidii chochote zaidi inakushushia credibility

Nimekupa mifano jinsi kesi zinavyotolewa mchanganuo wa kimaamuzi ikiainisha vifungu vya sheria walivyotumia kuhukumu

Kesi ya Mananra mbona TFF ilikaa masaa mawili mbele ya mic na waandishi wa habari ikitoa mchanganuo?

Una mahaba sana na Yanga mpaka unajisahau
 
Huyu dogo alikuwa sahihi kabisa kujiita Fei Toto!
 
Aondoke kisheria, sio kihuni. Ana/alikuwa na mkataba wa kisheria na Dar Young Africans, angetumia sheria kutengua mkataba wake na Yanga. Kijana anajiumiza na kujimaliza mwenyewe kisoka, soka ni career fupi sana, asipokuwa makini atajutia mda anaopoteza.
 
OKey, embu tusubiri kama itatoka faini iwapo hatorudi na itakuwa kiasi gani na iwapo italipwa na kama haitolipwa ni nn kitatokea. Uwezekano wa Yanga kumwachia Fei bado upo, sioni "WIN" kwa Yanga iwapo hakuna dau kubwa la fei hata akirudi kambini akakaa tu.
 
Mahakama ipi uliona inaweka mwenendo wa kesi ya Mbowe zaidi ya Martine Maranja Masese ambaye ni mwanachama wa CHADEMA? Wewe ukajua Jaji ndo alikuwa anaandika mitandaoni?
Nani kasema jaji ndio anayepaswa kufanya hilo?

Unaelewa hata unachokiandika hapa?
 
Geuka mzazi, mkataba uweke pembeni, huyu ni kijana, ujana maji ya moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…