Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo tarehe 2 Machi, 2023 kwa ajili ya kusikiliza pamoja na mambo mengine shauri la mapitio (Review) ya uamuzi wake wa tarehe 9 Januari 2023 kati ya Feisal Salumu na Klabu ya Young Africans kama yalivyowasilishwa na muombaji Feisal Salum dhidi ya Klabu ya Young Africans.

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi

Kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali hivyo imetupilia mbali shauri hilo.

Sababu kwa undani za uamuzi huo zitatolewa kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo siku ya Jumatatu 6 Machi, 2023.

View attachment 2535208

Ugali Na Sukari Bado Upo Pale Pale [emoji23]
 
" ignorance of the law is not an excuse before the court of law"

"Ignorantia juris non excusat"
 
[emoji23][emoji23]ila wewe jamaa yaani unaleta reference za kuna Young Thug, Kodak black?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Watu wanapotoa uwanja mpana wa kutaka utoe mifano ili kuthibitisha, lazima nitoe

Hizo ni kesi ambazo nazifuatilia so inapotokea mnabishana kuwa hakuna swala la live kwenye ishu ya kesi na ukaombwa utoe mifano, sioni kama ni kosa kutoa mfano wa hivyo
 
OKey, embu tusubiri kama itatoka faini iwapo hatorudi na itakuwa kiasi gani na iwapo italipwa na kama haitolipwa ni nn kitatokea. Uwezekano wa Yanga kumwachia Fei bado upo, sioni "WIN" kwa Yanga iwapo hakuna dau kubwa la fei hata akirudi kambini akakaa tu.
Uwekano wa Fei kuuzwa upo ila cha msingi sheria na taratibu zifuatwe kama mkataba ulisainiwa na watu wawili utavunja na pande mbili.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
[emoji23][emoji23]ila wewe jamaa yaani unaleta reference za kuna Young Thug, Kodak black?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Mimi nilitaka mchanganuo wa maamuzi kuwekwa public, waru wakai flip hoja ikawa naonekana nataka kesi iwe live

Nikawaonesha uwezekano wa hilo kuwepo na pia nikirudi kwenye hoja yangu bado reference ninazo

Hakuna kitu kama hicho, wakina Shafii Dauda wanafungiwa kila kitu kilikuwa open

TFF ndio chombo kinachohitajika kufanya hayo yote kuweka kila kitu bayana, hizi habari za kusema wahusika hivi wahusika vile inaongeza mashaka kuwa maamuzi yaliyotolewa hayakuwa fair.

Kesi ya Dauda ni dhidi ya nani? Si TFF? wenyewe na ndio wao wanaweka wazi? Na je ushawahi kuona kesi zao waandishi wakaruhusiwa kuingia ndani kuona majadiliano ya kesi au unacholetea ni maamuzi/ hukumu ya kesi?

Na maamuzi yasipokuwa fair si mwenye shauri lake anayo fursa ya kuipeleka kesi yake mbele kwakuwa TFF hawajasema maamuzi yao ni kikomo.
 
Ingekuwa mimi ningevumilia msimu uishe mshahara wakiweka nachukua
 
Kesi ya Dauda ni dhidi ya nani? Si TFF? wenyewe na ndio wao wanaweka wazi? Na je ushawahi kuona kesi zao waandishi wakaruhusiwa kuingia ndani kuona majadiliano ya kesi au unacholetea ni maamuzi/ hukumu ya kesi?
Kesi ya Morrison ilikuwa ni dhidi ya TFF? Mbona waliitisha press kutoa ufafanuzi?
 
Hii ni Kesi ya Morrison inayohusu mkataba, na hadi feedback za CAS zipo

Na hii tunayojadili hapa, ni kesi ya Feisal inayohusu mkataba. Maamuzi ya TFF yapo hapo juu kwenye post ya mleta mada!

Sio kesi zote zinazohusu mkataba zinafanana. Na ndio maana maamuzi pia hayafanani.
 
Yanga ni taasisi, huwezi shindana na taasisi kama yanga kwenye anga la soka la bongo chini ya Tff...ni kutwanga Maji kwenye kinu! Sikio halizidi kichwa!

Yale yale ya R. Singano(messi) sasa yanamkuta Fei toto kwa kutumia akili za kitoto kabisa kuvunja mikataba.

Soka lake naliona wazi kabisa likiisha hivi hivi kama mwenzake singano!
 
Mimi nilitaka mchanganuo wa maamuzi kuwekwa public, waru wakai flip hoja ikawa naonekana nataka kesi iwe live

Nikawaonesha uwezekano wa hilo kuwepo na pia nikirudi kwenye hoja yangu bado reference ninazo

Unachotaka kiwekwe wazi ni kipi?

Maamuzi ya TFF, au mkataba wa Feisal na Yanga?
 
Wewe na Uyanga wako jikite kwenye hoja achana na mipasho ya kimhemko haikusaidii chochote zaidi inakushushia credibility

Nimekupa mifano jinsi kesi zinavyotolewa mchanganuo wa kimaamuzi ikiainisha vifungu vya sheria walivyotumia kuhukumu

Kesi ya Mananra mbona TFF ilikaa masaa mawili mbele ya mic na waandishi wa habari ikitoa mchanganuo?

Una mahaba sana na Yanga mpaka unajisahau
Umesoma sheria?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Na hii tunayojadili hapa, ni kesi ya Feisal inayohusu mkataba. Maamuzi ya TFF yapo hapo juu kwenye post ya mleta mada!

Sio kesi zote zinazohusu mkataba zinafanana. Na ndio maana maamuzi pia hayafanani.
Kesi ina conclusion ambayo haifahamiki imetumika kanuni gani kuhukumu yani kiufupi haina mchanganuo

Kwenye circumstances ya Morrison hapo watu waliweza ku question chochote ambacho hakikuwa clear ili ku prove kuwa kweli haki imetendeka

Kwanini swala la Feisal mchanganuo wa maamuzi yake ufanyike gizani?
 
Yanga ni taasisi, huwezi shindana na taasisi kama yanga kwenye anga la soka la bongo chini ya Tff...ni kutwanga Maji kwenye kinu! Sikio halizidi kichwa!

Yale yale ya R. Singano(messi) sasa yanamkuta Fei toto kwa kutumia akili za kitoto kabisa kuvunja mikataba.

Soka lake naliona wazi kabisa likiisha hivi hivi kama mwenzake singano!
Na lisipoisha na akafanya vzr kwenye club na timu ya taifa baada ya haya matatizo kupita? Utapatwa na hasira au utampongeza?
 
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo tarehe 2 Machi, 2023 kwa ajili ya kusikiliza pamoja na mambo mengine shauri la mapitio (Review) ya uamuzi wake wa tarehe 9 Januari 2023 kati ya Feisal Salumu na Klabu ya Young Africans kama yalivyowasilishwa na muombaji Feisal Salum dhidi ya Klabu ya Young Africans.

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi

Kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali hivyo imetupilia mbali shauri hilo.

Sababu kwa undani za uamuzi huo zitatolewa kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo siku ya Jumatatu 6 Machi, 2023.

View attachment 2535208
1. Ana washauri wapumbavu wa kiwango Cha juu kabisa.
2. Mawakili wake ni mbumbumbu mnoo.
3. Mla sukari Kwa ugali huenda amewahi kula haya [emoji263][emoji263]
 
Back
Top Bottom