Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Angekuwa Zitto na ACT yake angeitwa msaliti

Hii nchi ngumu sana aiseeee

Tujifunze kuupa muda nafasi ili tujiridhishe.
Zitto hata kabla ya kukutana na rais alishawekwa kundi la wasaliti hivyo akikutana naye huo ni muendelezo tu wa usaliti ambao uko ndani yake kitambo, learn how to differentiate things.
 
Mkuu chadema ya sasa chini ya mwenyekiti wake itakupa presha ya bure. Jamaa anaangalia kwanza masilahi yake na ya familia yake, nyinyi wengine mmeachwa mtetee chama tu mitandaoni. Wengi mtaishia kulalamika tu lakini hamna ujanja wa kumfanya chochote.

Wakati anaharibiwa shamba lake na kufukuzwa NHC maslahi yake yalikuwa wapi?. Hicho sio kikao Cha Mbowe, ni kikao Cha CCM na serikali pamoja na chadema. Turuhusu watu waongee kwanza baada ya muda mrefu.
 
Wanasiasa wakiwa wanaitwa wanalambishwa asali, huwezi kusikia kelele tena za Ajira, mfumko wa Bei wala Bei ya petrol.

Nyumbu Ni nyumbu siku zote

Wewe ndio mkuu wa nyumbu. Kura uipe CCM Halafu mzigo wa wananchi uikabizi chadema?. Nenda kaililie ccm yako huko iliyoshindwa kudhibiti mfumuko wa Bei.
 
Haya ww endelea kuupa maumivu moyo wako. Kina prof Safari, Mabere Marando na wengine wengi wenye elimu zao na maono yao waliliona hili kitaambo, wakaamua kuwapisha wenye njaa waendelee kuuza utu wao kwa sababu ya njaa zao.

Wenye njaa walishahamia CCM. Kipindi chadema wanataka kuandama si wewe ndio ulikuwa unawadhihaki Leo wamekubali mazungumzo unawaita wenye njaa. Wewe kuwa na njaa usidhanie kila mtu ana njaa.
 
Huyu samia atakuja kuwageuka 2025 hamtoamini.
Hapa anawajaza tu upepo
 
Sio kwamba kukubali KUWA CHINI YA CCM?
To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara lenye umoja na nguvu kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
 
Wakati anaharibiwa shamba lake na kufukuzwa NHC maslahi yake yalikuwa wapi?. Hicho sio kikao Cha Mbowe, ni kikao Cha CCM na serikali pamoja na chadema. Turuhusu watu waongee kwanza baada ya muda mrefu.
Hahaha hayo mazuzu achana nayo Kaka.
 
Huu uzi ukiona negative posts za maneno makali yaliyojaa chuki na uchungu au posts zilizogubikwa na matusi usijiulize wala usishangae kwani hao ni SUKUMA GANG.
Wamafurah🤣
 
denooJ kwani unataka mwisho wa siku afanyeje? Aache kukutana na Rais?

Maridhiano ni mchakato (process). Unaweza usiyaone matunda ya kazi hii njema mara moja na papo kwa papo...

Let's be patient..

Surely, I personally see bright future ahead..

It's very difficult. But, surely there's hope..
Sawa maridhiano ni mchakato, but atleast basi wangeanza kuonesha kwa vitendo hata dalili za kufikia muafaka.

Kwangu mimi angalau ningemuona Lissu na Lema wamerudi ningekuwa na hope, au nione mikutano ya hadhara imeruhusiwa, lakini vyote hivi bado kimya...

Halafu hii tabia ya kulazimishana kukaa chini kujadili mambo yaliyopo kisheria ndio inanikera zaidi, hii ita-set bad precedence mbele ya safari, CCM ni wahuni hakuna asiyejua.

Hawa jamaa most likely wataharibu tena makusudi halafu tena wawaite kwenye meza ya mazungumzo, huu kwangu ni ujinga tu, mimi naona bora waseme kama wao ni madikteta ijulikane moja.
 
Mkuu chadema ya sasa chini ya mwenyekiti wake itakupa presha ya bure. Jamaa anaangalia kwanza masilahi yake na ya familia yake, nyinyi wengine mmeachwa mtetee chama tu mitandaoni. Wengi mtaishia kulalamika tu lakini hamna ujanja wa kumfanya chochote.
Nyie mlitakaje kama mazungumzo hayapo? Vita au ugaidi?
Chama cha siasa kinapambana kwa hoja, na msipoelewana ndio yanakuja mengine kama ya kule Congo au Msumbiji.
Samia kesha gundua chama makini cha upinzani ni Chadema ndio maana kawaalika wazungumze, sio wale ambao unapingana naye lakini ukimlambisha sukari anasema Samia anashinda uchaguzi. Kwani ccm walikuambia wanamsimamisha?
 
Duh, umegusa 'buttons' zote zenye maumivu kwa CHADEMA katika andiko fupi kabisa!
Acha tusikie yatakayoletwa kwetu juu ya mkutano huo.
Mtu bado anakukanyaga makusudi halafu anakwambia usilalamike, bado tupo kwenye meza ya mazungumzo, kuwa mvumilivu!
 
mwanasiasa akikuaga akakwambia anaenda kulala....we jifanye nawe unaenda kulalala kisha toka njee zunguka upande wa pili wa mtaaa mtakutana na kuendelea na stori
 
Back
Top Bottom