Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
[emoji16][emoji16][emoji16]kwann unasema hvyo mzee baba
ukiangalia hizo devu zake na hizo nyewele nitofauti kuna zile app unajizeesha unaweza weka mitindo tofauti tofauti ya nyewele na mtu asitambue kirahisi kama sio zako hizo nyewele
 
Watu wanakwambia CDM wamekosea kujishusha, wacheni hato...watu wakikutana kwenye kamati kuu wanafikiria mbali sana!
Kujishusha kwa nani? Ni hekima na busara tu ndivyo vinavyoongelewa hapa na si kwamba mshindi ni nani. Acheni mambo ya ki Primary ligi kila break time ikifika.
 
Ndani ya CDM mbona hakuna maridhiano mpaka wazee waandamizi Safari na Sumaye wameamua kujiweka kando..? Angeanza ndani kwanza.
Kwa hyo wewe umeona kaongea pumba. Akili nyingine ni shida sana
 
Leo nimeisikiliza hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Bwana Freeman Mbowe.

Katika hotuba yake hiyo fupi, Bwana Mbowe kapendekeza Rais Magufuli aitumie nafasi yake ya urais kuleta maridhiano nchini.

Mimi sikubaliani na hilo. Maridhiano [reconciliation] ya nini? Kwani Watanzania tumetendeana ubaya kiasi cha kufikia hatua ya kuwa na maridhiano?

Afrika Kusini ilibidi wawe na maridhiano baada ya Apartheid kuondolewa. Hilo lilibidi kwa sababu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu uliotendeka kipindi cha Apartheid. Ilibidi waandike ukurasa mpya wa historia ya taifa lao.

Rwanda nao ilibidi waunde tume ya kudumu ya Umoja wa kitaifa na maridhiano. Kilichotokea Rwanda nacho kilikuwa ni ukiukwaji mkubwa kupita maelezo wa haki za binadamu. Hakukuwa na njia nyingine ya kusonga mbele kama taifa kama wasingesameheana na kuridhiana kutokana na kilichotokea mwaka 1994.

Mwaka 2008 Kenya nao ilibidi waunde tume ya Ukweli, Haki, na Maridhiano kwa kile kilichotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na pia kwa matukio mengine yaliyotokea kabla ya hapo.

Sasa sisi Watanzania maridhiano ni ya nini?

Ndiyo, kuna matukio ya hapa na pale ambayo yametokea. Baadhi ya matukio hayo yana mwelekeo na harufu ya kisiasa na yenye kukiuka haki za kibinadamu.

Lakini, kama taifa, bado kabisa hatujafikia kiwango cha kuwa na sababu ya maridhiano.

Watanzania bado tuna umoja. Kwa ujumla hatuchukiani kwa misingi ya kikabila, kidini, wala kisiasa.

Tumechanganyikana mno. Waislamu wameoana na kuzaa na Wakristo. Wasio na dini nao wamo humo humo.

Watu wamechangiana makabila. Unakuta mtu babu yake ni Mpare, bibi yake ni Mnyamwezi, mke wake ni Mhaya, yeye mwenyewe ni nusu Mnyamwezi nusu Mhaya, wanae wana asili ya Uhehe, Upare, Uhaya, Unyamwezi, na kadhalika.

Ambalo naliona ni la muhimu ni ustaarabu.

Ustaarabu [civility] katika namna tunavyotendeana licha ya kuwa na tofauti zinazotutenganisha kisiasa na kiitikadi.

Tumezikubali siasa za vyama vingi. Siasa za vyama vingi ni siasa za kiushindani. Ushindani una mambo mengi. Mambo hayo, kwa uchache, ni propaganda, hisia kali, kutambiana, na kadhalika.

Sasa, kwenye muktadha huo wa ushindani, tunaweza kukumbushana kuhusu ustaarabu na uungwana, utawala wa kisheria, haki sawa kwa wote, na ufuatwaji wa katiba. Kwenye hayo sina tatizo.

Lakini hizi habari za kusema sijui tuwe na maridhiano sizikubali. Bado kabisa hatujafika huko.

Najua mpo mtaosema kwamba si busara mpaka tufike huko ndo tuwe na maridhiano na blah blah.

Nami nasema hivi, kama hatujafika huko kwa nini tufanye kitu juu ya jambo ambalo halipo ilhali kuna mengine tuwezayo kuyafanya ili kuboresha hali iliyopo?

Hatuhitaji maridhiano. Tunachokihitaji ni ustaarabu na uungwana katika vile tunavyotendeana.
 
Sasa kama wengine hawana huo ustaarabu na hawaoneshi dalili za kuwa nao unataka kifanyike nini?
 
.
Nilikua sijajua ubinafsi wa Wabongo hadi awamu ya 5 ilivyoingia na U turns na kujitoa akili kwa "Nzagamba" wengi wa JF
politics-religion.jpeg
 
I wish Magufuli angekuwa na angalau 50% ya performance kwenye demokrasia, ukiongezea na hizo dreamliner, SGR, na vingine, angekuwa our best president ever!
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano

Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:

Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!

Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.

Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.

Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.

Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
Yaani sijaelewaga ishu yao ni nini hasa Chadema. Wao si ndo waligoma kumtambua na wakatoka bungeni siku akifungua bunge? Wao si ndo waligoma kuhudhuria mikutano na shuguli alizokuwa akizifanya majimboni mwao? Aliyesema wakamchinjie Magu baharini ni nani? Yaani aliyenuna ndo anataka maridhiano? Kuridhiana ndo nini? Siwaelewi. Yeye aseme anataka msaada wa Magu kuonekana ni muhimu kwenye hili taifa ili watete matumbo yao 2020, huku wameoka kuwakosesha makambanda wao wengi ulaji ambao wangepata ajira kwenye serikali za mitaa. Hivi mtu kama yule aliyekuwa meya wa Ubungo akikosa ubunge 2020, kile kitambi atakilisha nini?

Inashangaza sana baada ya miaka karibia 30, Chadema bado wanafanya siasa za kipumbavu.

Yeye aseme anaomba poo. Binafsi nilimshangaa Magu kumpa airtime, alishamtaja kwenye itifaki mwanzo wa spichi ilikuwa inamtosha.
 
Naunga mkono hoja!

Hata mimi sikuelewa Freeman Mbowe anazungumzia maridhiano ya nini!
Wewe lazima usielewe hata sikushangai, mleta mada anataka mpaka yatokee majanga zaidi ndio tutafute maridhiano, sasa hivi hizi kesi wanazobambikiwa wapinzani na kuharibiwa mali zao ( Mbowe) kwake ni vitu vidogo tu, hajui kama vinachochea chuki kati ya kundi moja na jingine kwenye jamii, yeye anataka tuendelee kuwakumbusha tu huku mkizidi kuumiza wengine kila kukicha!
 
Back
Top Bottom