Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Kweli umenena tujikumbushe Mzee Karume kilicho muondoa ni chuki zidi ya mtu mmoja aliye umizwa na alicho tendewa Mzazi wake tusiende keze chuki binafsi mtu kwenda kuharibu mali ya mtu kisa siasa
haya kwao ni vitu vidogo sana, mijitu imelewa madaraka kwa kiwango cha juu sana!
 
unataka kila mtu akubali mawazo yako sio?!, kuita wengine wanyama coz wanakupinga sio ustaarabu, you are selfish arrogant!

Silazimishi mtu ayakubali mawazo yangu. Sina uwezo huo.
 
Leo nimeisikiliza hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Bwana Freeman Mbowe.

Katika hotuba yake hiyo fupi, Bwana Mbowe kapendekeza Rais Magufuli aitumie nafasi yake ya urais kuleta maridhiano nchini.

Mimi sikubaliani na hilo. Maridhiano [reconciliation] ya nini? Kwani Watanzania tumetendeana ubaya kiasi cha kufikia hatua ya kuwa na maridhiano?

Afrika Kusini ilibidi wawe na maridhiano baada ya Apartheid kuondolewa. Hilo lilibidi kwa sababu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu uliotendeka kipindi cha Apartheid. Ilibidi waandike ukurasa mpya wa historia ya taifa lao.

Rwanda nao ilibidi waunde tume ya kudumu ya Umoja wa kitaifa na maridhiano. Kilichotokea Rwanda nacho kilikuwa ni ukiukwaji mkubwa kupita maelezo wa haki za binadamu. Hakukuwa na njia nyingine ya kusonga mbele kama taifa kama wasingesameheana na kuridhiana kutokana na kilichotokea mwaka 1994.

Mwaka 2008 Kenya nao ilibidi waunde tume ya Ukweli, Haki, na Maridhiano kwa kile kilichotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na pia kwa matukio mengine yaliyotokea kabla ya hapo.

Sasa sisi Watanzania maridhiano ni ya nini?

Ndiyo, kuna matukio ya hapa na pale ambayo yametokea. Baadhi ya matukio hayo yana mwelekeo na harufu ya kisiasa na yenye kukiuka haki za kibinadamu.

Lakini, kama taifa, bado kabisa hatujafikia kiwango cha kuwa na sababu ya maridhiano.

Watanzania bado tuna umoja. Kwa ujumla hatuchukiani kwa misingi ya kikabila, kidini, wala kisiasa.

Tumechanganyikana mno. Waislamu wameoana na kuzaa na Wakristo. Wasio na dini nao wamo humo humo.

Watu wamechangiana makabila. Unakuta mtu babu yake ni Mpare, bibi yake ni Mnyamwezi, mke wake ni Mhaya, yeye mwenyewe ni nusu Mnyamwezi nusu Mhaya, wanae wana asili ya Uhehe, Upare, Uhaya, Unyamwezi, na kadhalika.

Ambalo naliona ni la muhimu ni ustaarabu.

Ustaarabu [civility] katika namna tunavyotendeana licha ya kuwa na tofauti zinazotutenganisha kisiasa na kiitikadi.

Tumezikubali siasa za vyama vingi. Siasa za vyama vingi ni siasa za kiushindani. Ushindani una mambo mengi. Mambo hayo, kwa uchache, ni propaganda, hisia kali, kutambiana, na kadhalika.

Sasa, kwenye muktadha huo wa ushindani, tunaweza kukumbushana kuhusu ustaarabu na uungwana, utawala wa kisheria, haki sawa kwa wote, na ufuatwaji wa katiba. Kwenye hayo sina tatizo.

Lakini hizi habari za kusema sijui tuwe na maridhiano sizikubali. Bado kabisa hatujafika huko.

Najua mpo mtaosema kwamba si busara mpaka tufike huko ndo tuwe na maridhiano na blah blah.

Nami nasema hivi, kama hatujafika huko kwa nini tufanye kitu juu ya jambo ambalo halipo ilhali kuna mengine tuwezayo kuyafanya ili kuboresha hali iliyopo?

Hatuhitaji maridhiano. Tunachokihitaji ni ustaarabu na uungwana katika vile tunavyotendeana.
Unataka mpaka tuuane sana?
 
Eti maridhiano! Nasisitiza tena watanzania hawahitaji maridhiano, wanahitaji rule of law, democracy, na mengine mengi yenye manufaa. Chadema kuna baadhi ya maeneo wako clueless kabisa, huwezi kwenda kuomba demokrasia kwa mtu anayepora chaguzi! Mbowe na wenzie hawana political strategists. Tukio la leo sio la kusifiwa! Ni ujinga.
 
Ingawaje hakukuwa na namna nzuri ya kueleza hili, ila walichokisema wengi wanakifikiria.
Walichokifanya CCM kukosesha mamilioni ya watanzania kuwachagua viongozi wa mtaani wawapendao kimetengeneza hasira. Hawa ndo viongozi pekee ambao wananchi walikuwa na mahusiano nao.
Hali hii si salama kwa nchi.
 
Hilo neno wanalitumia kusaka kula yao baba, hawa wanasiasa wanatafuta neema kwa ajili yao na vizazi vyao sio kwa ajili yetu
 
Hata sielewi haya maridhiano ni aina ipi?
1.Ni ya kitaifa kuwa labda kabila au kanda fulani lina uadui na jingine?

2.Ya Kichama, kuwa Chama tawala ni kinatesa vyama vingine na kuleta uhasama wa kitaifa?
Hilo no 1 ni big NO
Hilo no 2 . Ni sarakasi tupu. Kama chama fulani basi kiridhiane na chama kingine isiwe kiujumla
Mfano. ZZK wakati vyama vingine vinamgomea rais alipohutubia bunge na kutoka alibaki. Akaitwa msaliti. Hapo ccm na ACT walikuwa poa tu.
Leo CDM katia timu Sherehe za Uhuru . ACt ya zzk imekula buyu inaaasema CDM Wamewasaliti.
Mi nadhani kama chama fulani kinabifu na mwenzake nenda mkae mridhiano huko kama ufipa kwa lumumba maana hata hii ya CDM kwenda hatukushirikishwa kama wananchi.
Kama Cuf anabifu na ACT wakakae wao .
Sio maridhiano ya kitaifa .

Mbowe alihitajika kuomba kwenda kuonana na mwenyekiti mwenzake wamalize kisailensa hatarekodiwa kuwa anaenda KUTUBU . Wenzake mbona walienda leo wanakula goodtime. Sisi asitushirikishe kumtongozea
 
Watanzania hatujawa na mvurugano wa kuhitaji maridhiano ya Kitaifa. Maridhiano yanayohitajika ni ya viongozi wa vyama vya siasa. Na Vyama vina platform yao ya TCD chini ya Shibuda, Mbowe angeamua kutumia nafasi yake vizuri kama M/kiti wa Chama kuwasilisha na kujadiliwa jambo hili huko ktk vikao vyao.
 
Back
Top Bottom