Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
I wish Magufuli angekuwa na angalau 50% ya performance kwenye demokrasia, ukiongezea na hizo dreamliner, SGR, na vingine, angekuwa our best president ever!
kwani hizo dreamliner na sgr ndio zinaletwa na demokrasia,acheni ubinafsi na kujiona nyie wa pekee,maendeleo yanafanyika na yanaonekana nyie komaeni na hizo module zenu za demokrasia mkija kushtuka wananchi wameshawasahau.

Mlizoea kumchezea sharubu mkwere mpaka tukasahau kufanya mambo ya msingi.

Nyinyi si wasomi na wataalamu wa research nendeni kwa wananchi now mkawaulize wanataka demokrasia au SGR??
 
Kwa kweli hapa neno 'maridhiano' halijatendewa haki. Mbowe labda aseme amekosa neno sahihi...

Ndiyo maana huyu jamaa kaanzisha mjadala huu...

Wewe unadhani angetumia "neno" gani badala yake?
 
Wanachama na wapenzi wachadema wanashindwa kuomba msamaha kwà wapenzi na wanachama wa CCM ili wanaCCM waone umuhimu wa hilo.

Pia chadema wanatakiwa waitishe mkutano wawaambie kuwa serikali iliopo madarakan n ya halali na serikali inafanya makubwa kufanya taifa lisonge mbele na wainishe hvyo vitu.

Bungen kila mbunge wa chadema akipewa nafasi ya kuongea aanze na kutambua serikali iliopo madarakan na juhud zake za maendeleo katika Jimbo anapotoka na utaifa kiujumla

Pia chadema ndio wanatakiwa kushusha silaha chini nasio kuemdelea kurusha makombora huku unamwambia serikali muache mapambano

Vinginevyo hakuna maridhiano.

Asante Sana
Aldeo.
 
Watu wanaotaka kukaa pamoja kujenga nchi yao wanakukera nini we mrundi!!!? Tanzania tumezoea kuzungumza pale tunapohitilafiana kama umetumwa kafie mbele huko kwenu,,,ina maana huoni ufa wa kisiasa uliopo???
 
John Shibuda leo kambatiza jina "shitabhonga",kwa lugha ya kaskazini(sukuma) lina maana ya mbegu isiyo bunguliwa.kudeal na Magufuli inahitaji akili pana si hasira vinginevyo..
 
Eti maridhiano! Nasisitiza tena watanzania hawahitaji maridhiano, wanahitaji rule of law, democracy, na mengine mengi yenye manufaa. Chadema kuna baadhi ya maeneo wako clueless kabisa, huwezi kwenda kuomba demokrasia kwa mtu anayepora chaguzi! Mbowe na wenzie hawana political strategists. Tukio la leo sio la kusifiwa! Ni ujinga.
Lianzishe wewe basi, "keyboard warrior " mlishindwa kumuunga mkono mange kimambi tarehe 26 mwaka juzi, alafu eti oho hawana political strategies
 
Kujadiliana na makamanda kwa kutumia akili ni mateso!!
Mimi pia ni Kamanda ila kuna mawazo au mada zingine zinahitaji logic tu na kutafakari. Mfano kwanini jambo flani litokee au lisitokee...?

It's a matter of using our sense...sio Kutokuelewa jambo halafu upinge tuu kisa ni kamanda...daah.
 
Kichwa chako kina ubongo wa nguruwe, kuna ubaya gani kuwa na maridhiano,?? Hata vitabu vitakatifu vinatufundisha maridbiano,

Hata mke na mume kuna wakati huridhiana ili mambo yaende

Maridhiano ni neno laweza kutumika kwa namna nyingine tu.

Maridhiano huwa ni ya watu waliohitilafiana hadi kufikia hatua ya kuumizana.

Sisi tumefikia huko?
 
Lianzishe wewe basi, "keyboard warrior " mlishindwa kumuunga mkono mange kimambi tarehe 26 mwaka juzi, alafu eti oho hawana political strategies, kenge nyie
Sihitaji kutukanana na wewe wala mtu yeyote for that matter. Nimeandika nachoamini na nina haki ya kufanya hivyo. Halafu kuandamana sio political strategy pekee na kwa kweli mimi sijazungumzia strategies, nimetaja strategists.

Sijawahi kumfatilia huyo Mange, simdharau lakini sio mtu wa mimi kumfatilia! Ni nani? Ni mtu wa caliber gani? Napenda kufuatilia wanasiasa makini, local and international sio Mange, whoever he or she is! Mange? Seriously!
Humu ndani hatulazimiki kuandika vitu vinavyofanana. Hili ni jukwaa huru na nitaandika kile ninachoamini bila kujali nitaitwa ' keyboard hero' or 'keyboard warrior'. Sheesh!!!
 
Kichwa chako kina ubongo wa nguruwe, kuna ubaya gani kuwa na maridhiano,?? Hata vitabu vitakatifu vinatufundisha maridbiano,

Hata mke na mume kuna wakati huridhiana ili mambo yaende

Maridhiano ni neno laweza kutumika kwa namna nyingine tu.
Maridhiano ya nini? Watanzania tumekorofishana lini? Tumegombana na kuuana lini?. Yaani kundi dogo la watu walioamua kuvuruga utawala wa sheria, haki za binadamu na demokrasia ndio litufanye eti tu call for maridhiano. Idealism ya ajabu kabisa.
 
Sumaye hajui demokrasia,nadhani BWM anajilaumu kumpa 10,anataka lazima ashinde yeye ndiyo iwe domokrasia.
Ndani ya CDM mbona hakuna maridhiano mpaka wazee waandamizi Safari na Sumaye wameamua kujiweka kando..? Angeanza ndani kwanza.
 
Maridhiano ya nini? Watanzania tumekorofishana lini? Tumegombana na kuuana lini?. Yaani kundi dogo la watu walioamua kuvuruga utawala wa sheria, haki za binadamu na demokrasia ndio litufanye eti tu call for maridhiano. Idealism ya ajabu kabisa.
Pambana uLitoe hilo kundi basi, mange
kimambi alijajaribu mkamtukana sana,
Tupe hizi mbinu za kuliondosha hilo kundi dogo katili
 
Hii ni hatua nzuri Sana.
Baada ya hapa Fanya chama kiwe na Sura ya kitaifa.
Na mchezo utakua umeishia hapo na tutakua na upinzani ambao hata Dola linaweza twaliwa.
Asante Kwa busara
 
Mwanza, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na mwenzake wa Chadema, Freeman Mbowe wametumia fursa ya kutoa salamu katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika kumwomba Rais John Magufuli kutumia nafasi yake kulea, kulinda na kukuza demokrasia.

Sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika mjini Mwanza leo Jumatatu Desemba 9, 2019 katika uwanja wa CCM Kirumba na kuhudhuria na watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, vyama vya siasa na Serikali.

Profesa Lipumba ndiye aliyeanza kutoa ombi hilo baada ya Rais Magufuli kuwakaribisha viongozi wa vyama vya siasa waliokuwa wamekaa jukwaa kuu kusalimia wananchi.

Akitumia salaam ya chama chake cha “Haki” Profesa Lipumba amesema pamoja na hatua kubwa ya maendeleo inayopigwa, ni jukumu na wajibu wa Rais Magufuli na Serikali kuendeleza misingi ya demokrasia nchini.

Kauli kama hiyo pia ikatolewa na Mbowe akimueleza Rais Magufuli kuwa anayo dhamana ya kuhakikisha sio tu demokrasia inalindwa na kukuzwa, bali pia uwepo wa haki na usawa kwa wote bila kujali tofauti zao.

“Nimeshiriki maadhimisho haya kuthibitisha misingi ya umoja, mshikamano na undugu miongoni mwa Watanzania. Nakuomba mheshimiwa Rais kutumia nafasi na dhamana yako kulinda demokrasia. Kusiwe na wanaofurahi huku wengine wakilalamika,” amesema Mbowe.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom