FT: Simba 0-3 Raja Casablanca | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.02.2023
Bocco Off na Sakho hana mchezo leo labda abadilike kipindi cha pili.

Chama kucheza pembani lilikuwa kosa kwa Kocha Robertinho.. Nguvu Moja [emoji881]
 
IMG-20230218-WA0016.jpg
 
Nilisema kwa aina ya kikosi cha simba, wakijitahidi ni sare! Kuna watu walichukia. Hata kesho kwa Yanga; wasipokuwa makini, mambo yatajirudia.

Uwekezaji wetu bado uko chini ukilinganisha na wenzetu. Ni hamasa pekee ndiyo itakayo zisaidia timu zetu. Ila siyo kwa kupitia wachezaji aina ya John Rafael Bocco.

Kweli Uwekezaji Mdogo. Tunahitaji Billioni 500 kwa kila Timu (Simba na Yanga) hizi Timu kama Zitaka Kufanya Vizuri
 
😅😅😅 cham bwana vipasi vyake ambavyo havina maana...

Nilisema toka juzi huwezi kshinda laja ukiwa na
Sawa dogo
Henock
Sakho
Chama kiungo mbovu anayeonekana mechi dhaifu za Nbc. Toa chama weka phiri,toa Sakho weka Kibu toa Saido weka Baleke.
 
Simba Sijui tatizo nini ni kocha mpya mfumo wake wachezaji hawauelewi au ni wachezaji ndio hatuna.

Hatuna wachezaji mzee,kiufupi tuna magarasa mengi,wachezaji wengi umri ,angalia raja ina vijana wengi ndio maana unaona mchaka mchaka simba anapigishwa wa kutosha,viwango vya wachezaji wengi wa simba ni vya chini,msimu huu tutatia aibu kimataifa,kama uto tunashindwa kumfunga ligi kuu ndio ujue hatuna wachezaji
 
Wachezaji wako very slow wanapaka paka sana rangi mpira na back pasi nyingi

Chama ajitahidi kuongeza spidi
Toa sewadogo ingiza mkude
Toa Sakho ingiza mshambuliaji mwingine
Baadae toa Boko ingiza mshambuliaji mwingine
 
Hii game Simba anashinda kabisa kuna uzembe wanafanya pale mbele wakitulia kuna chuma mbili mpaka tatu tulieni.
 
Quality ya wachezaji ni ndogo mno
Bahati mbaya hautokei TBS taasisi iliyodhaminiwa kwa ajili ya kutoa takwimu za Quality

Hivyo maoni yako yanabakia kuwa ni upuuzi tu
 
Simba haijacheza mpira wa Robertinho toka alivyokwenda kwao. Mipira ya back passes nyingi na kushindwa kunepetrate pale mbele ni mpira Simba walikuwa wanacheza kipindi cha Mgunda. Wamemwambia aende slow na style yake matokeo yake ndiyo haya.

Kumuonea haya Bocco nalo ni tatizo sugu. Unakuacha Baleke, Phiri benchi kwa ajili ya Bocco kweli?
 
Inahitaji moyo wa chuma kuishabikia timu mbovu kama Simba
Kama kuishabikia Simba mbovu kunahitaji moyo wa Chuma (nadhani ulimaanisha chuma chakavu!), basi kuishabikia Yanga mbovu kunahitaji kuwa na moyo wa Chuma cha pua.
 
Back
Top Bottom