FT: Simba 0-3 Raja Casablanca | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.02.2023
Screenshot_20230218-165101_Google.jpg

Vipers ana point 6 zetu
 
Kwa Mkapa hatoki mtu!!

Hii ni kauli mbiu maarufu kwa mashabiki wa Simba Sports Club linapokuja suala la mechi za Kimataifa za CAF. Kwa kauli hiyo ashakufa Al Ahly, Orlando Pirates, As Vita, Kaizer Chiefs na wengineo na sasa ni zamu ya kufa Raja Casablanca. Nani anabisha?

Ndio, ni Simba Sports Club wakiwaalika Raja Casablanca pale dimba la Benjamin Mkapa, katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa Africa.

Simba watashuka dimbani wakiwa na lengo moja tu la kutafuta alama 3 mara baada ya kupoteza mchezo wa kwanza. Habari njema ni kuwa Saido Ntibazonkiza atakuwepo kikosini ila pengo kubwa ni kukosekana kwa Sadio Kanoute "Putin" kutokana na kadi.

Raja Casablanca nao wataingia kwa tahadhari katika mchezo huu, japo wanaongoza kundi lao mara baada ya kuivurumisha Vipers goli 5 kwa nunge katika mchezo wao wa kwanza!

Mchezo huu utakuwa majira ya saa 1:00 usiku wa leo, na utakuwa mubashara kupitia ZBC2 ya AzamTv na Chaneli 229 ya DStv.

Kila la heri kwa Mnyama, naamini kauli mbiu ya " Kwa Mkapa hatoki Mtu" itaendelea kufanya kazi...

Utabiri:
Simba 2-0 Raja Casablanca
View attachment 2520955
Any update ya kikosi?
 
Back
Top Bottom