FT: Simba 2-2 Al Ahly | Benjamin Mkapa Stadium | 20.10.2023 | African Football League
Labda leo Timu ibadilike kujituma zaidi ila mkicheza kama mlivyocheza mechi mbili na Power mtapotea sana hakuna Timu pale ila wakijituma na kujua majukumu yao watafanya vizuri...
 

Haya haya ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imewadia. Leo tarehe 20/10/2023 Tanzania itashuhudia mtanange wa kihistoria kati ya timu ya Simba ya Tanzania dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Mechi hii ni ya ufunguzi wa michuano ya African Football League ambayo inachezwa barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Mechi itakuwa Mubashara Azam Sports 1HD kuanzia saa 12:00 Jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki lakini mapema kutakuwa na sherehe za ufunguzi huku Ali Kiba akiongoza burudani.

Yanayojiri yote utayapata katika uzi huu…

Yapi maoni yako kuhusu mechi hii?
FB_IMG_1697768364539.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante modes kwa kufanyia kazi Ushauri wangu
 
kUNA KUSHINDA NA KUNA KUFUZU KWENDA ROUND YA PILI(NUSU FAINALI)

MNYAMA ANAWEZA KUPATA MATOKEO KWA MKAPA MAY BE 1-0 AU 2-1 AU 2-0

LAKINI SIONI AKITOBOA ATAKAPOENDA MISRI MAANA KULE MISRI NAONA KABISA AKICHAPWA +4 KWA BILA
 
Kwa michuano hii nasema na nitasema tena Simba lazima afungwe leo kwa Mkapa na All ahly

Nakazia hivyo kwa sababu wachezaji wa Simba hawana self confidence wanapocheza na timu kubwa kama Al Ahly, yaani Simba inategemea mchezaji moja moja tu kama mungu mtu kwenye kikosi chao

Nisiseme mengi sana maana matokeo tutayaona tu

Nipigwe bani iwapo Simba atashinda leo
Simba Sc haina self-confidence inapocheza na team kubwa.? Ahly sio mara ya kwanza kucheza nayo, tena katika miaka hiihii ambayo yuko on fire, achana na nyinyi mnaotembelea historia za miaka 10 huko.

Tumecheza na Ahly mechi 3, Wydad mechi 2, Raja mechi mbili nk. Kipi kinakufanya uione Simba Sc kama wageni sana wa mechi kubwa.?
 
Kila la kheri Al ahly timu Bora zaidi barani Afrika [emoji2957] Sisi Wananchiiiiiiiiiiiiiiiii Mabingwa wa TANZANIA tupo pamoja nanyi
 
Back
Top Bottom