FT: Simba 2-2 Al Ahly | Benjamin Mkapa Stadium | 20.10.2023 | African Football League
Kila la heri mnyamaaaa....
Rarua hao wàafrica weupe...
Screenshot_20231005-194942_WhatsApp.jpg
 
Watu wameshapata ma crush wao wa kiarabu...nyiee Tanzania tuna sehemu yetu special mbengoni...
##Nenda mnyamaa##
 
Hatimaye tarehe 20/10/2023 imefika. Saa 12 jioni ya leo, itapigwa mbungi ya kukata na shoka kati ya wenyeji Simba na wageni Al Ahly.

Kwa kutazama vikosi vya timu zote mbili, hakika, Al Ahly wako juu mno ya Simba. Utofauti huu wa Dar na Washington upo pia kwenye mafanikio ya timu hizi.

Lakini, kutokana na soka kujaa matokeo na matukio ya ukatili na ya kustaajabisha, bado Simba itaipa tabu Al Ahly Uwanja wa Mkapa almaarufu Lupaso.

Nieleweke, sijasema kuwa Simba itashinda au itafungwa. Matokeo ni dakika 90. Lakini, kutakuwa na mechi ngumu na ya kustaajabisha. Kila mmoja atataka kuonesha anavyostahili kuwepo mashindanoni.

Wachezaji wakataoibeba Simba ni Kibu, Onana na Baleke. Ni kutokana na uchezaji wao usioeleweka au kutabirika. Wataupiga mwingi mno. Watatakata. Wengine watakuwa wa kawaida tu.

NB: Siri ya viongozi wa FIFA na CAF kuwepo kwa Mkapa mnaijua? Afrika inatumika kama uwanja wa majaribio kwa mashindano kama haya kwa ngazi ya klabu.

FIFA na UEFA waligonga mwamba Ulaya. Tukaonekana uwanja wa majaribio. Kwakuwa kuna pesa zimewekwa mbele kama tai!
 
Back
Top Bottom