Haya haya ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imewadia. Leo tarehe 20/10/2023 Tanzania itashuhudia mtanange wa kihistoria kati ya timu ya Simba ya Tanzania dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Mechi hii ni ya ufunguzi wa michuano ya African Football League ambayo inachezwa barani Afrika kwa mara ya kwanza.
Mechi itakuwa Mubashara Azam Sports 1HD kuanzia saa 12:00 Jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki lakini mapema kutakuwa na sherehe za ufunguzi huku Ali Kiba akiongoza burudani.
Yanayojiri yote utayapata katika uzi huu…
Yapi maoni yako kuhusu mechi hii?