FT | Yanga SC 2-0 Singida Fountain Gate | NBC Premier League | Benjamin Mkapa Stadium | 27.10.2023

FT | Yanga SC 2-0 Singida Fountain Gate | NBC Premier League | Benjamin Mkapa Stadium | 27.10.2023

Mwanangu sio kuwa nakupangia ila umekosa hela hivi hivi kwa utabiri wako mzuri na imekuwa hivyo, next time bashiri please [emoji120]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Cha ajabu sasa, kila nikibet napigwa tu, sijui kwa nini?
 
Simba wa nini tena? Umesema Kama Azam alifungwa Singida hawezi kaza nikakuambia Singida kwa Yanga hata Azam angeshinda historia inaonyesha asingekaza.
Poa mkuu pumzika, maana hii imeisha kihivyo.
Tungoje ya kesho itakuaje.
Je Ihefu wanaikazia Yanga tu ama vipi?.... majibu yote ni hapo kesho.
 
Diara Leo Tena ameleta utani wake uliosababisha ihefu wasawazishe .

Kama anataka kucheza ndani aache kudaka.

Yao performance yake ni nzuri lakini anapamba sana na kujisahau kusaidia right back line kuna hatari mbili zimetokea zingeleta madhara .

Kwa uchezaji wa Leo inaonyesha yanga wali relax kutokana na aina ya mpinzani Hata aziz ki hakuonyesha makali ya juzi , lakini hawatakiwi kufanya hivyo Hata mpinzani akiwa hafifu.
 
Bashte!!!!
Nimeanzana nao huko juu....
Wanataka kujilinganisha na Giant...
Kwani giant maanake nini katika ulimwenguni wa mpira wa miguu? Maana nasikia tu giant, giant ndio maanake nini katika soka?
Ili uwe giant kwenye mpira wa miguu unatakiwa uwe na vigezo vipi?
 
Match Day
Yanga SC vs Singida FG
NBC Premier League
Benjamin Mkapa Stadium [emoji2522]
Time: 1815hours
View attachment 2794435

Updates...

Saa 12:04 Jioni
Hali ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa sasa ni Shwari kabisa.

Mashabiki wanazidi kuongezeka hapa.

Mawingu mepesi mepesi yametanda

Vikosi Vinavyoanza
View attachment 2794817View attachment 2794818

Saa 12:10Jioni
Timu zinaingia uwanjani sasa...

Updates...

Naibu Waziri Mkuu yuko hap Uwanjani na Viongozi wengine

Mpira umeanza sasa, Yanga wameanzisha Mpira sasa

Dakika ya 10'
Singida wanapata faulu lakini haileti madhara, kwa wapinza.

Matokeo ni 0 - 0

Dakika 11,
Aziz K anagongana na Mudathir hapa.
Anachechemea kidogo ila anaendelea.

Dakika 15'
Yanga wanapata faulu karibu kabisa na 18.
Inapigwa inatoka Nje

Dakika ya 20'
Kipa wa Singida anapatiwa matibabu hap uwanjani
Magoli ni 0 - 0
hadi sasa.

Dakika ya 21'
Yanga wanapata kona lakini haizai matunda

Dakika 23'
Kunatokea shambulizi kali langoni mwa Singida.
Inaishia kuwa kona ya pili haizai matunda

Dakika ya 28'
Mchezaji wa Singida anapata yellow kadi

Dakika ya 30'
Max anaipatia Yanga goli la kuongoza.

Yanga 1-0 Singida FG

Dakika ya 39'
Max anaipa Yanga goli la 2

Yanga 2-0 Singida FG

Dakika 41'
Mpira umesimama kwa muda Goli kipa wa Singida akipatiwa matibabu.
Amepata maumivu kidogo.
Kwa nje naona kipa namba Tatu wa Singida akipasha.

Singida wamefanya mabadiliko ya Kipa.

Dakika za Nyongeza ni 4.
Kuhitimisha kipindi cha kwanz

Dakika 45'
Zimekamilika
Yanga 2-0 Singida FG.

Updates...

Kipindi cha Pili kimeanza hapa.
Singida wameanzisha Mpira tayari.

Dakika ya 47'
Singida wanafanya shambulizi kwenye lango la Yanga

Hafiz anakosa goli la wazi kabisa hapa

Dakika ya 50'
Keseke anacheza faulu mbaya sana kwa Dickson Job,

Dakika 56'
Kadi nyingine ya Njano inatoka kwa Mchezaji wa Singida

Dakika ya 60'
Singida wanapata faulu eneo la nje kidogo ya box ya 18.

Dakika ya 63'
Azizi anafunga ila inakuwa Offside ya Max

Dakika ya 65'
Kadi nyingine ya njano kwa Singida

Azizi anakosa goli la wazi

Dakika ya 69'
Pacome anaumia

Timu zinafanya mabadiliko
Konikon Out
Musonda Inn

Pacome out.
Skudu Inn

Dakika ya 75'
Yanga wanakosa goli, inakuwa kona haizai matunda.
Game on...

Yanga 2-0 Singida FG

Dakika ya 77'
Lomalisa Out
Kibabage Inn

Kadi nyingine ya Njano kwa Singida

Dakika ya 83'
Aziz Out
Mzize Inn

Game On...

Dakika 90'
Nyongeza ni 4

Sure Boy anapata yellow Card

Full Time.
Yanga 2-0 Singida FG
Reasonable updates
 
Mbinguni kwenu? Are you sure?

Mbinguni hawaendi waongo, watungaji, wafitinishaji na waongeao wasilolijua
 
Back
Top Bottom