Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Yeah ,mapimduzi haya yamekua well organized ,wamewasubiri kuona tume itafanyaje, maana hali yake ya kiafya ilikua hovyo,ila uroho wa madaraka

Acha astaafishwe ki lazima
 
Makoloni ya Ufaransa ni very unstable na mbaya zaidi watu kama hao kina Ali Bongo wako madarakani Kwa miaka Mingi sana Kwa hiyo naunga mkono washughulikiwe ila Jeshi liandae uchaguzi haraka sana.

Huwa sitaki kabisa tawala za Kijeshi Wala wanajeshi kuchukua Uongozi wa Kiraia,waandae uchaguzi haraka iwekezekanavyo Ili kurudisha Utawala Kwa raia maana kinyume na hapo wataishia kuwa madikteta na kukandamiza Wananchi wanaowakosoa.

Mwisho Paul Byiya wa Cameroon ajiandae kisaikolojia.
 
Kwa nini kikosi cha watu 12 tu kipindue na jeshi lote kutii? Wanatumia mbinu zipi?
Hili swali najiulizaga na sijawahi pata jibu, kwa mfano nchi nzima inaweza kuwa na wanajeshi 400k lkn utasikia wanajeshi kumi au kumi na mbili ndo wameipindua nchi nzima hii imekaaje? Je ni kweli kwamba wanajeshi wote nchi nzima nakuwa wanaunga hayo mapenduzi? Sidhani!

Je kwa hao wanajeshi wanaokuwa hawaungi mkono mapenduzi huchukua hatua Gani?? Msaada jamani kwa wajuvi
 
Kweli hili limetia doa ingawa bado tuna nafasi ya kulirekebisha Ndugu yangu.
How,na watu wenyewe wameziba masikio wala hawaoni hawasikii. Hata hivyo kwangu mapinduzi yanayokea Africa is a new dawn.Nadhani tawala zote kandamizi ambazo zimeibia watu wao rasilimali wakae chonjo,I mean zote,without exception,ikiwemo Tanzania.

Haiwezekani baada ya miaka sitini na tatu ya Uhuru tukiwa na rasilimali nyingi kiasi hiki,bado watu wetu wengi hawana maji,na hata hao wachache wanaopata maji si safi na salama;watu wanakufa kwa sababu hawana huduma za afya;watoto wengine hawasomi kwa kuwa wazazi wao hawawezi kuwapeleka shule kwa kuwa hawana michango,madaftari na kalamu au uniform; Elimu inayotolewa ni chini ya kiwango,shule hazina mazingira mazuri ya kusomea na vitendea kazi;watu wetu hawana nyumba bora za kuishi ;watu wetu wanapata mlo mmoja tu kwa siku na wengine hawapati kabisa nk.nk..

No, lazima kama Watanzania tufike mahali tuseme hapana hii haivumiliki tena inatosha,na tufanye kitu ambacho kitatutoa kwenye uonevu huu
 
Najaribu kufikiria hizi nchi zote zinazofanya mapinduzi, mkuu wa majeshi anakuwa hayupo; ile 'power' yake inakuwa imedhibitiwaje?, ingawa jeshini wapo wanaonufaika na mfumo na hawatapenda mapinduzi yatokee.
Kuna utaratibu wa kufanya mapinduzi, ni maelezo marefu labda yapate uzi wake na ambao utafutwa.
Mapinduzi huwa ni rahisi sio kama watu wanavyodhani, ila yanahitaji mazingira ya kusababisha.
Changamoto huwa inakuja kwenye kulinda hayo mapinduzi dhidi ya counter-coups na isolation ya kimataifa
 
Hizi habari za mapinduzi kwa nchi za africa sio nzuri kwa museven , kagame na yule wa congo.

Madaraka mazuri ukiwa nayo ila ukipinduliwa unavyotreatiwa kama choo tu..
 
Propaganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…