kwa niger kwenyewe ECOWAS wamenywea, Gabon ndio imewavuruga mazima. Soon ukanda wao yatatokea tena mapinduzi mengine tena na watazidi kuvurugikiwa washindwe waingie wapi na kubaki kila mmoja akijipambania nchini mwake. Mapinduzi yanazidi kupamba moto na kuonekana ni mtindo mpya wa kuleta mageuzi ya kisera na uongozi kwa haraka. Kwa mtindo huu zipo nchi ukiziangalia tawala zao unaona ni dhahiri mapinduzi ya kijeshi kutokea wakati wowote. Nchi kama Cameroun, Uganda, Rwanda na zingine zenye demokrasia za magumashi kuna dalili za kutokea mapinduzi ya kijeshi au raia wakaungwa mkono na jeshi kutwaa madaraka