Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Kama watu walitaka kimpindua hata Nyerere unafikir kuna mtu ana guarantee ya kubaki salama kama ataendelea ku mess up na maslahi ya watanzania walio wengi kIsa tu awafurahishe wachache?

Never say never
hakuna nchi iliyo salama afrika kwamba haina uwezekano wa kutokea coup . Watu wasijifariji sana
 
 
Bado ccm
 
ECOWAS hapa hawajui washike la Gabon au waache la Niger. Nyakati nzuri sana hizi kuishi, Mungu atupe umri mrefu tuone mwisho wa hili vuguvugu ukoje.
kwa niger kwenyewe ECOWAS wamenywea, Gabon ndio imewavuruga mazima. Soon ukanda wao yatatokea tena mapinduzi mengine tena na watazidi kuvurugikiwa washindwe waingie wapi na kubaki kila mmoja akijipambania nchini mwake. Mapinduzi yanazidi kupamba moto na kuonekana ni mtindo mpya wa kuleta mageuzi ya kisera na uongozi kwa haraka. Kwa mtindo huu zipo nchi ukiziangalia tawala zao unaona ni dhahiri mapinduzi ya kijeshi kutokea wakati wowote. Nchi kama Cameroun, Uganda, Rwanda na zingine zenye demokrasia za magumashi kuna dalili za kutokea mapinduzi ya kijeshi au raia wakaungwa mkono na jeshi kutwaa madaraka
 
Sijui kama tunaenda au tunarudi nachojua tupo njiani.
 
Mapinduzi yalikuwepo sana miaka ya mwanzo ya uhuru wa nchi za kiafrika, sasa yamerudi kwa kasi mpya na yanaonekana ni fasheni mpya mbadala wa demokrasia. Wananchi wameyapenda baada ya kuchoshwa na ulaghai wa chaguzi za kidemokrasia kwenye masanduku ya kura. Wanaona hawana cha kupoteza bora wanajeshi wapindue tu kuliko kuhubiriwa demokrasia feki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…