" Wenye Akili Yanga SC nzima ni Watu Wawili tu Rais Mstaafu Kikwete na Baba yangu Mzazi Mzee Manara waliobakia wote hawana," alisema Haji Manara alipokuwa akihojiwa na EFM Radio Kipindi cha Sports Headquarters mwaka 2021.
Baada ya Nukuu ( Kumbukizi ) hii sasa Maswali Kuntu ya GENTAMYCINE yanaanza............
1. Haji Manara hivi ni Wewe ndiyo umetengeneza Brand yako kama unavyojitapa Kutwa au ni Simba SC na sasa Yanga SC uliko ndiyo zimekutengenezea Brand yako kutokana na Ukubwa wa Vilabu hivi Viwili na Ushawishi wao nchini?
2. Haji Manara hivi ungekuwa ni Msemaji wa Ihefu FC au Gwambina FC una uhakika ungejulikana na ungekuwa Maarufu mpaka kuwa na hiyo Brand yako Kubwa inayokudanganya mpaka Unadharau Watu na kujiona uko juu ya Mpira wa Tanzania?
3. Haji Manara kama umesema jana kuwa unajua Siri nyingi za TFF ( hasa Maadui zako Rais Karia na Katibu wa TFF Kidau ) je, kwanini hukuzitoa ( hukujilipua nazo ) Siku nyingi ili utusaidie Wadau wa Mpira kujua tusiyoyajua na badala yake Umeyatoa jana kwa Mtindo wa Kukomoa, Propaganda na Kulipiza Kisasi?
4. Haji Manara je, TFF ( Unayoichukia zaidi ) ingekuwa inakuonea ingekufungulia ilipoingia Madarakani baada ya Kufungiwa na aliyekuwa Rais wa TFF ( Mwana Yanga SC ) Jamal Malinzi?
5. Haji Manara bila Busara na Nguvu Kubwa ya TFF Kukulinda unadhani kwa Kosa lile Kubwa na la Jinai ulilomfanyia Mtangazaji wa Kike wa Michezo wa Clouds FM Prisca Kishamba na ile Kauli yako ya HATARI Kiusalama, Kimichezo na Kiutalii uliyoitoa dhidi ya Timu Ngeni zilizokuwa zikija Kucheza na Simba SC ( katika CAFCL na CAFCC ) kuwa wawe Makini kwani Simba SC inatumia Sumu na hata Kuua una uhakika kuwa leo hii usingefungiwa Maisha katika Medani za Soka na pengine hata Kufungiwa na Serikali?
6. Haji Manara aliyekushtaki hadi Kufungwa Kwako huko ni Uliyegombana nae Arusha Rais wa TFF Wallace Karia au ni Sekretarieti ya TFF? Je, ule Msamaha wako wa Kinafiki ulitakiwa uutoe wa Sekretarieti ya TFF au kwa Rais wa TFF Wallace Karia tena Nyumbani Kwake?
7. Haji Manara je, unajua kuwa kwa Kitendo chako cha Jana tu kusema ( tena Kijeuri kabisa ) kuwa Wewe bado ni Msemaji na Mhamasishaji wa Yanga SC wakati tayari Unatumikia Adhabu Kisheria kinaweza kukufanya Uongezewe Adhabu yako zaidi na sasa ikawa Kali kuliko hiyo Ndogo tu uliyopewa?
8. Haji Manara ni kwanini Matatizo yako Binafsi yakipelekea Wewe Kuadhibiwa na Mamlaka huwa unapenda Kuihusisha Klabu ya Yanga ili upate Huruma na Sapoti yao?
9. Haji Manara je, Maudhui yako ya Jana ( pamoja na Matusi, Dhihaka na Kashfa ) katika ile Press ya Jana yalikuwa ni yako Binafsi au yana Baraka za Yanga SC kwa 100%?
10. Haji Manara je, una uhakika una Washauri wazuri na kwamba Watu wengi Wanaokuzunguka Wanakupenda na Wanakutakia Kheri kama Unavyojidanganya na Kujimwambafai Kutwa?
11. Haji Manara je, ikitokea Rais wa TFF Wallace Karia akiamua Kukushtaki 'Kijinai' kama tulivyohakikishiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF iliyokuhukumu kuwa Ulimtishia Maisha Rais wa TFF Karia huku ukimwambia kuwa ATAKUKOMA na UTAMUONYESHA utaendelea kuwa Salama?
Wachezaji wa Kucheza Mpira ni Kumi na Moja ( 11 ) na Mimi GENTAMYCINE nimekuuliza haya Maswali yangu Kumi na Moja ( 11 ) na nasubiria sasa Majibu yangu kutoka Kwako Haji Manara na wana Yanga SC Wenzako wote hapa JamiiForums ili nijue kama mna Akili au hamna Kabisa kama inavyojulikana tokea Uhuru wa Taifa hili la Tanzania.