Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Una hoja usikilizwe na pia kueleweka inahitaji mtu atafakari kwa kina.

1.Ili mtu aweze kufanya kitu vizuri zaidi sharti hicho kitu kimvutie.
Ndio maana kuna ule msemo usemao ukitaka kufanikiwa penda unachofanya,hiyo hutoa uwezo wa kuwekeza mawazo yako hapo na resources zote hivyo itaonekana ni kipaji chako mwisho wa siku.
2.Kwahiyo mtoto anapozaliwa akianza kukua hujikuta amependa jambo fulani ambalo akili yako hu concentrate upande huo na analifanya vyema,ila kwa mwingine analipenda lakiniakili yake inashindwa ku focus vzr.
3.Baada ya kupenda jambo hilo ili uzidi kuwa mzuri lazima uliendeleze,tunasikia vipaji huendelezwa ili ujenge uzoefu mwingi na kumaster hilo jambo

TAKEAWAY
Ili kutengeneza kipaji vitu hivi ni muhimu
1.Penda unachofanya/kutoka moyoni.
2.Focus kiakili na kiroho.
3.Practice mara nyingi.
 
Mkuu hii comment yako nitaihifadhi kabisa ili niitumie kuwaelewesha vijana kama akina Nomadix
 
Hakuna anaye zaliwa anajua.

Wote tunazaliwa tukiwa hatujui chochote.

Utofauti unakuja pale tunapoanza kujifunza vitu, kuna ambao huelewa kwa haraka zaidi. Na wengine huelewa polepole.

Hakuna anayezaliwa na kipaji cha aina yeyote ile. Isipokuwa utofauti huja pale tunapoanza kujifunza mambo.
 
Kipaji ni ule uwezo wa kuelewa au kufanya jambo/kitu fulani kwa wepesi na ufanisi zaidi kuliko wengine.

Binadamu wote tunazaliwa sawa. Bila ufahamu wala kipaji chochote kile.

Utofauti huja pale tunapoanza kujifunza mambo na vitu.

Hapa ndio kuna ambao huelewa kwa haraka zaidi na kufanya mambo kwa kiwango cha juu zaidi, na wengine huelewa polepole na kufanya mambo kwa kiwango cha wastani au kidogo.
 
Mkuu umeongea facts,na hicho ndicho nimeelezea huko juu,lkn bird 🐦 mi sijaelewa anataka majibu gani,naona kakamaa na msimamo wake!!!,
Anatakiwa atambue kwamba ubongo wa binadamu una pande mbili au umegawanyika mara mbili,kuna upande wa akili inayofikika na upande wa akili isiyofikika ( subconscious mind),, conscious mind ndo upokea dhamili, yaani kile tunachojifunza aidha kwa kuona ,kusikia,kuhisi nk,kutokana na mazingira tulimo na kufundishwa mfano shuleni nk.
Sasa subconscious mind huko ndo kuna kipaji,,unapolala ukaota jambo hapo unakuwa umeamsha upande huu, hili kufanyia na hilo jambo likawa dhamili lazima ihusike ili kupata data,kwa lengo la kupata ufanisi katika jambo husika,,mfano watu wawili wanaweza kuwa wote wanaelimu sawa,lkn katika utendaji wa kazi mmoja akawa na ufanisi kuliko mwenzake,,je wajua kinawatofatisha ni nini ?,ni kipaji tu..ndipo hapo unapokuta mwenye kipaji, kwingine wanaita wito,huyu mwenye wito ufanya kazi kwa bidii na kuridhika na furaha tele,lkn asiye na wito ufanya kazi ini mradi tu siku ipite,ni kama vile analazimishwa kufanya kazi afanyayo.
 
Kuna ambao wanelewa kwa haraka mambo ya elimu . Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye ufundi. Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye sanaa na michezo. Hapo ndipo unakuja kujua maana ya kipaji.
 
Full stop!
Uzi huu upigwa kufuli zito na mamodinyo wa Jamii Africa.
 
Ninachoendelea kuikataa ni kuwa hakuna mtu anayezaliwa na uwezo wa kufanya kitu.

Tunakuja duniani then tunaanza safari mpya.

Narudia tena kukuuliza hili swali:- Je, kama Messi na Neymar wote walizaliwa wakiwa na vipaji/uwezo wa kucheza mpira kwa nini namna yao ya uchezaji inatofautiana?/Kwa nini hakuna uniformity katika utendaji wa kile walichotoka nacho tumboni mwa mama zao?
 
Kuna ambao wanelewa kwa haraka mambo ya elimu . Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye ufundi. Na kuna ambao wanaelewa haraka kwenye sanaa na michezo. Hapo ndipo unakuja kujua maana ya kipaji.
Sisi tunachokikataa siyo kuuelewa haraka, tunachokikataa ni madai kuwa mtu huzaliwa tayari akiwa na uwezo wa kufanya kitu au jambo fulani ambapo nyinyi mnasema ni kipaji.
 
Siwezi kusema chochote ila nadhani wewe huna kipaji nikushauli tu kwamba binadamu ana akili sana lakini binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiri.

Binadamu akipata changamoto huamsha ubongo kutafuta suluhu kama hana files alizo save kuhusiana na changamoto aliyo nayo haiwezi kulitatua,.(kupata suluhisho)
 
Neno kipaji ndo linatuharibu sisi waafrika, linatuaminisha kuwa watu fulani wamezaliwa na uwezo fulani na sisi hatuwezi kitu funi kwa sababu hatujazaliwa na uwezo wa kitu hicho.

Ni neno baya ambalo linaweza kujaribu kizazi chako.
 
Huko kuelewa haraka ndio talent yenyewe, nilichogundua you guys mnachanganya talent na skill.

Let's break it down a bit, Talent is not taught, it's a natural ability to see or do something in a certain way. But skill is something that we have become good at and love doing but have been taught. It's taken hours, days, weeks, months, years to master. It's something that you get better at over time and that you desire to do and master.
 
Mkuu kipaji hakuna?. Okay twende na Leonardo Da Vinci ambae alikuwa mtu hatari sana kwenye kuchora kama wewe.

LEONARDO DA VINCI
Leonardo Da Vinci alikuwa Anatomist, Architect, Astronomer, Botanist, Cartographer, Engineer, Geologist, Hydro-dynamasist, Mathematician, Musician, Theater producer, Inventor. Sasa Noma zaidi ni Jamaa alikuwa anaweza kuchora picha na mkono wa kushoto alafu mkono wa kulia anatandika advanced calculus na abstract algebra kwao wakati mmoja, wait a minute, kama hujaelewa jamaa alikuwa anaweza kwao mkono wa kulia ukawa anapiga mtihani wa physics advance alafu mkono wa kushoto anapiga mtihani wa wa pure mathematics. Mkuu imagine jamaa maandishi yakee yote aliyaandika kwao mirror scripts na aliandika kutoka kulia kwenda kushoto badala ya kushoto kwenda kulia na ili uweze kusoma yale maandishi lazima umulike kwenye kiyoo.. Mkuu bado tu hamna kipaji?.... Mwaka 1994 Bil Gates alinunua notebook ya jamaa kwa dola milion 30 ilokuwa na madini ya ugunduzi wa vitu mbali mbali, unaweza ukaimagine bilion 70 ya mwaka 94 ni shs ngapi ya leo?...Mkuu acha kabisa.
 
Sasa mbona ana vipaji vingi wakati tulikubaliana kuwa kipaji huwa ni kimoja tu😀.

Alizaliwa na uwezo wa kufanya hivyo vitu vyote ulivyovitaja?
 
Sasa mbona ana vipaji vingi wakati tulikubaliana kuwa kipaji huwa ni kimoja tu😀.

Alizaliwa na uwezo wa kufanya hivyo vitu vyote ulivyovitaja?
Yaaah alifanya hivyo vyote, jamaa ndio inasemekana jitu lenye akili nyingi kuwah kutokea ujue ni hatari sana mtu mkono wa kushoto unachora na wakulia unatandika equation za physics. We kamsome alafu utakuja na majibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…