Hans Pope: Manara hataki kusaini mkataba ambao atalipwa milioni 4
hakuna shaka haji manara kama msemaji wa simba sc alikua akiishi kwenye dunia yake aliamini yeye ndo kila kitu pale simba hakuna anayeweza kumtingisha.

alitukana waandishi hakuna aliyemgusa wala kumkanya alidhalilisha watu na hakuna aliyemkanya leo hii kapatikana yeye anakimbia huruma ya mashabiki mm kama yanga damu naona sawa wacha wagombane wakishtuka wamekula tatu kigoma

TWENZETU KIGOMA MNYAMA ANAKUFA
angalua hanspope akifunguka kuhusu manara
 
Kinachoonekana wazi ni kuwa, viongozi wa Simba wakiongozwa na MO na bodi nzima, hawapendezwi na Manara kufanya kazi na GSM pamoja na Azam Ltd.

Na hicho ndicho kimemponza.

Manara alichokosea tu ni kuwa kamkaripia CEO wake. Na kumtishia kuwa atamuondoa Simba. Sawa, ataondoka lakini si kwa matakwa ya Manara.

Ngoja tuone, how will the sagga end!.

Simba tukifungwa, ndo zogo litakuwa tamu balaa.
Ni popote pale, hii ina conflict of interest! Asaini sehemu moja.
 
Amepewa option ya kuchagua eidha awe mwakilishi wa Simba SC au Asas, GSM na Azam Ltd? Simple as that.

Hata mimi binafsi nilikuwa sipendezwi jinsi alivyotumia brand ya Simba kutengeneza brand yake ili kupata endorsements kama za Asas, GSM na Azam
acha wivu wa kikuda mkuu, hii simba sio yako wala ya babu yako, shabiki yoyote anaweza kuitumia kujitengenezea jina na hata kigonga madili wewe inakuuma nini kama sio chuki hizi
 
Sasa subiri afukuzwe Simba ndy atajua kama kweli hy endorsement ni mhm, maana atakuwa unfollowed na wengi watapoteza interest kwake, ataomba hata apewe mshahara wa laki moja.

Sasa Azam au GSM ,Asas hawachezi Mpira ingekuwa anadhaminiwa na yanga sawa..kungekuwa na conflict of interest.
 
Kwa upande wangu regardless na tuhuma za Manara kwa Barbara, Manara njia aliyoitumia amekosea sana. It is very unprofessional kuleta mambo kama yale public halafu unarecord na voice note kabisa, kwa mtu wa caliber kama yake ule ni utoto na uswahili.
Athari zakukulia maeneo kama karia koo
Usishangae

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
GSM ni wadhamini wa Yanga na wana interest na Yanga, Azam wana products ambazo zinafanana na products za wadhamini wa Simba 'mo energy' , kumbuka simba walisaini mkataba rasmi wa udhamini na products hizo na Simba inavuta mpunga. Huoni conflict of interest hapo? Yaani uwe msemaji wa Nike alafu uwe balozi wa products za Adidas.
Sasa Azam au GSM ,Asas hawachezi Mpira ingekuwa anadhaminiwa na yanga sawa..kungekuwa na conflict of interest.
 
Mkataba huo wa milioni 4 ungempunguzia sana mapato kwa kumfanya asiendelee kufanya kazi kwa makampuni kama Azam, Gsm, Asas, Maji ya uhai, n.k

Manara walitaka kumpa mkataba wa kizamani na hovyo kabisa, yani hata account ya instagram ya manara ingekuwa chini ya klabu, kwa umaarufu wa Manara na watu wanavyomfatilia wangeigeuza account kuwa sehemu ya kutangaza bure bidhaa za Mo ama ndugu zake huku wakikataa kutangaza makampuni mengine kama azam, gsm, n.k

Mkataba pia ungemfunga manara kutoweza kusaini dili lolote nje ya usemaji wa club simba, yani huu mkataba ungemfanya awe na jukumu moja tu la kuwa msemaji wa simba na kuacha kuwa balozi au msemaji wa makampuni mengine, hayo madili hadi aingie ingekuwa mpaka apate ruksa kutoka kwa ceo ambae ni babra na pesa anayolipwa inaenda kwenye mapato ya klabu huku yeye akilipwa mshahara pekee.

Huu mkataba ni wa kizamani sana na umekaa kufungiana ridhiki tu, kwa wenzetu huko nje mtu anaweza kufanya kazi kampuni ya NIKE wakati mdhamini wa jezi ya timu anayofanyia kazi ni ADIDAS ambao ni wahasimu wakubwa wa Nike.

Tatizo wivu na roho za kwanini haji apate mafanikio nje ya kuisemea simba? Angalia mfano tu mdogo haji manara ana nyumba yake,magari yake, na mali nyingine, hii ni kutokana na mikataba minono kutoka kwa asas, gsm, azam, maji ya uhai, n.k ambao pasi na shaka wanamlipa vizuri, pengine hata ile faini ya milioni 5 aliyoenda kuilipa kwa cash ofisi za tff huenda alipewa na hayo makampuni mengine ili wamtunzie brand yake, mfano mwengine angalia siku ya harusi ya haji wale GSM walifanya kufuru kumtunza haji, hii kitu huenda ilikuwa inawaumiza sana wamiliki wa simba waliodhani walimkomesha kwa kumlipa laki 7.

Manara kaupiga mwingi hapa, kakataa kubanwa kweye mtego wa kuifanyia kazi simba pekee kitu ambacho kingemlazimu awe anatangaza bidhaa za MO pekee ama ndugu zake, Manara ana familia na inamtegemea kuna kipindi huenda atatoka simba na bado mke wake na wanae bado watabaki kumtegemea yeye, ni haki yake kutafuta michongo nje ya simba ili kuongeza kipato na kuweza kusimama hata pale akiacha kulipwa na simba.

HITIMISHO: Simba wakae upya, watatue hili jambo kwa njia za kidiplomasia na sio kukurupuka kumfukuza manara, nafasi ya kurekebisha kasoro za mkataba bado ipo, mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu mchungu, hao kina Mo na Babra nao wajiweke kwenye hali ya manara.
 
Back
Top Bottom