Hans Pope: Manara hataki kusaini mkataba ambao atalipwa milioni 4
Yote uliyoongea ni sawa na solution ni yeye kutoka Simba kwenda kuenjoy hio freedom ya kufanya kazi bila kuingiliana na maslahi ya Simba.

But the question is Haji Manara relevant kwa hayo mashirika without Simba?

Haji anaihitaji Simba kuliko Simba inavyomuhitaji hata hao GSM, Azam, Asas na wengineo wamewekeza kwa Haji sababu ya uwepo wa Simba fans behind Haji Manara Brand. Imagine leo Haji atoke Simba ile audience yake haitakua entertained na Haji tena.
 
Sasa subiri afukuzwe Simba ndy atajua kama kweli hy endorsement ni mhm, maana atakuwa unfollowed na wengi watapoteza interest kwake, ataomba hata apewe mshahara wa laki moja.

Afukuzwe tu? Mbona hata ile audio kaikana sio yake baada ya mashabiki kumgeuka [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Bahati nzuri GENTAMYCINE nakujua vyema tu kuanzia ukiwa Mwenezi CCM, wana Familia wako ( hasa Dada zako pale Kwenu Buguruni na Ilala ) na pia ulipokuwa Msemaji wetu Simba SC.

Kabla sijasahau nisiwe mchoyo wa Shukran na Pongezi kwa input yako Kubwa uliyoiweka ndani ya Klabu yetu ya Simba SC na niseme tu Kwako Asante kwa Utendaji wako Klabuni Simba kwa muda wote uliokuwepo.

Sasa naanza Kukusiliba ( Kukusema )

USWAHILI
Haji Manara binafsi nilivyoona Simba SC imeanza kuwa ya Kiustaarabu basi hata nawe pia ungekuwa na huo Ustaarabu ila bahati mbaya ukaendeleza Uswahili wako wa Kariakoo, Ilala Bungoni na Buguruni.

KUDEKA KITOTO SANA
Haji Manara mara nyingi sana pale ukiguswa tu na Wapinzani wako umekuwa ukipenda zaidi Kudeka ili uonekane ni Muhimu zaidi ya Wengineo Klabuni Simba.

ULEMAVU WAKO KUTAFUTA HURUMA
Haji Manara hujaanza leo kupenda kuutumia Ulemavu wako wa Ngozi ulionao kama sehemu ya kutafutia Huruma kwa Mashabiki wa Simba pale tu ukishambuliwa na Maadui zako wa Kimchezo ili utetewe zaidi.

KUJISAHAU NA DHARAU
Haji Manara ulivyoanza Kazi ya Usemaji Simba SC ulikuwa na Nidhamu nzuri ila baadae ukaanza kubadilika taratibu na kuwa na Dharau ambayo ndiyo imekugharimu sasa.

UMAARUFU ULIOKUPA KIBURI
Haji Manara kataa uwezavyo ila ukweli utabaki kuwa ya kwamba Umaarufu ulionao kwa kuupatia Simba SC ndiyo umekupa Kiburi ulichonacho ambacho Kimekugharimu zaidi.

KUKENGEUKA KIMAADILI
Haji Manara hujaanza Kulalamikiwa leo na Waandishi wa Habari ( ambayo pia ni Fani yako ) kwa tabia yako ya kupenda Kuwatukana, Kuwaxhihaki na hata Kuwadhalilisha Kitendo ambacho ni very unprofessional and unethical kwa nafasi muhimu uliyokuwa nayo ndani ya Simba SC.

Haji Manara je, Professional Ethics zako zinasema umtishie na umdhalilishe immediate Boss wako CEO Mitandaoni wakati channels za Kupeleka Malalamiko yako unazijua? Huu ndiyo Usomi wako.ulionao na ulipoishia?

UNA KIPAJI CHA UNAFIKI SANA
Haji Manara ni Wewe huyu huyu mara nyingi ukiwa katika Interviews zako ulikuwa ukimsifia mno Senzo Mazingiza (Former Simba CEO), Barbara Gonzalez (Simba SC Current CEO) na Zackaria Hanspoppe ila leo umegeuka na Kuwashutumu na Kuwachafua kwa wanasimba ili Kuwaharibia kama Wewe ulivyojiharibia.

UWONGO
Haji Manara nadhani kwakuwa CCM ilikupeleka nje Kusomea Propaganda (Uwongo) huenda Masomo ya huko yalikuingia vizuri na sasa unakifanyia Kazi.

Umasema kuwa hapo Simba SC hulipwi Mshahara na kwamba sijui huna Mkataba.

Haji Manara una uhakika wa haya? Haji siyo Wewe ambaye kila Mwezi ( ukitoa Posho ) zako huwa unapewa Tsh Milioni Mbili na Simba SC huku Posho zako za Mwezi zikikaribia Tsh Milioni Moja? Hiyo Tsh Laki Saba unayoisema umetoa wapi wakati hiyo huwa ni Pesa yako ya Vocha ya Simu na Internet yako kwa Mwezi mzima? Haji Manara Uislamu ulionao unaruhusu kuwa Muongo hivi?

Mbona hujasema mpaka leo umekataa Kusaini Mkataba mpya wa Mshahara wa Tsh Milioni Nne ( 4 ) kwa Mwezi?

MCHOCHEA CHUKI NA MGAWANYIKO BAINA YA WACHEZAJI WA SIMBA SC
Haji Manara hivi kuna asiyekujua Wewe kuwa na tabia ya Kuchochea Chuki kwa Wachezaji wa Kigeni na wazawa?

Haji siyo Wewe uliyetukanwa na aliyekuwa Kocha wa Simba SC Patrick Aussems kwa Kukuita Mpumbavu na usimuingilie Kazini alipokuwa hawapangi Wachezaji wako unaokuwa nao sana Baa Kulewa?

HUNA UKOMAVU WA KIUME
Haji Manara ni nani alikuambia kuwa ukigombana na Wakuu ( Viongozi ) basi Suluhu ni Kukimbilia Mitandaoni Kulalamika na kutafuta Huruma kwa Mashabiki?

Haji Manara hivi Yanga SC walipomsimamisha aliyekuwa Katibu Mkuu wao ( Mwanasheria kama sijakosea ) Patrick Simon ulimsikia akipaparika Mitandaoni kama Wewe vile kulia lia na Kudeka?

Simba SC kuna muda ilimsimamisha Meneja wake Patrick Rweymamu ( Mtani wangu wa Kihaya ) je, Yeye nae alipaparika hovyo Mitandaoni kama Wewe?

SIMBA SC ULIIKUTA AU IMEKUKUTA?
Haji Manara acha Kudanganya Watu kuwa Wewe ndiyo umehamasisha Mashabiki wa Simba SC kujaa Viwanjani.

Klabu ya Simba imekuwa na rekodi ya kujaza Uwanja kutokea kwa Mashabiki wake tangia miaka ya 80 mpaka hii leo.

Ni Soka safi la Simba SC ndiyo linavutia na Kuhamasisha Mashabiki kujaa na siyo Sauti yako na maneno yako ya Kihuni na wakati mwingine ya Kishamba.

KUTUMIKA NA YANGA SC NA KUISALITI SIMBA SC KILA IKIKUTANA NAO
Haji Manara nani asiyejua kuwa Wewe ili Kumridhisha Mkeo (Shabiki wa Yanga SC japo unadai umembadili kuwa Simba SC), Baba yako Mzazi (Kipenzi chako kabisa), Gharib Said Mohammed (GSM) na Injinia Hersi Said (Marafiki zako na Mabosi zako wakubwa) na Kiongozi Mmoja Mstaafu Tanzania ambaye uko nae karibu wote hawa huwa wanakutumia kuihujumu Simba SC kila ikicheza na Yanga SC?

Labda leo nikupasulie ukweli wako Haji unadhani wana Simba SC hatujui kuwa Mechi yetu na Yanga SC hii ya Juzi tu Wewe ndiyo uliuza Ramani ya Vita kwa Yanga SC na ukalipwa na GSM kwa Kuwatahadharisha Yanga SC wasipitie Mageti yale makubwa Mawili ambayo Simba SC tulikuwa tayari tumeshafanya Unyangindo (tumeroga mno) na wakapita Kwingineko?

Nilikutana na Kocha Msaidizi wa Simba SC (Mtani wangu wa Kiha) Selemani Matola Veron Mzambia na kumuambia kuwa nina Hasira zaidi nawe na ningebahatika kukutana nawe ningekuzaba Kibao japo najua unatembea na (unamiliki) Bastola yako.

Ulivyo Mpuuzi ukasahau kuwa tayari Simba SC imeshakushtukia ambapo katika muendelezo wako ule ule wa Usaliti na Kuihujumu Simba SC kuelekea Mechi ya Fainali ASFC juzi Usiku ulionekana Avic Town Kigamboni ilipo Kambi ya Yanga SC ukiwa na Tajiri yako Gharib.

UTETEZI WA KIPUMBAVU ZAIDI
Haji Manara sijui ni kwanini unatumia Nguvu kubwa Kujitetea juu ya Shutuma zako wakati wenye Akili kukuzidi na tunaokujua tumeshakudharau.

Leo umekuja tena na Voice Note yako nyingine ukiwa Unalia huku kama vile Ukiilaani Klabu na baadhi ya Watendaji wake kuwa wana Chuki na Wewe.

VITISHO VYAKO VYA KIPUUZI
Naona umetoka Kuuendeleza ule ule Upuuzi wako katika Ukurasa wako wa Instagram ambako umesema kuwa Umechoka Kusakamwa ma kwamba Jumatatu ijayo utasema kila Kitu (utatema) nyongo na kwamba Tanzania itasimama.

KAULI YA GENTAMYCINE KWAKO
Haji Manara nami nakuambia hapa hapa kuwa ukimaliza tu Kuichafua Klabu yangu ( yetu ) ya Simba SC na Viongozi wake nami nakwenda Kuweka hadharani hapa Mabaya yako yote uliyoyafanya na unayoyafanya sasa.

Nakuonya tumia Siku hizi Tatu (3) kabla ya kufika hiyo Jumatatu kujitafakari na nakuambia usije ukathubutu kutuchafua Simba SC kwani Mimi GENTAMYCINE ndiyo nitakuchafua kuliko ( zaidi ) na hutoamini kwani nakujua ndani nje na nina Siri zako kibao tu ambazo Mbili nikiziweka hadharani lazima Central Police ikuhusu na Ofisi ya DCI ikuhusu.

Najua unayopanga Kuyaongea hiyo Jumatatu ijayo ni yafuatayo.....

1. Uhusiano wa CEO na Mwekezaji

2. Suala la Mchezaji Jonas Mkude

3. Kuondoka kwa aliyekuwa CEO Simba SC Senzo Mazingiza

4. Sakata la Bernard Morrison

5. Hanspoppe na Usajili wa Wachezaji

6. Siri za Ushindi wa Simba SC ndani na nje ya Uwanja

7. Uwekezaji wa Mohammed 'Mo' Dewji ndani ya Klabu ya Simba.

HITIMISHO

Haji Manara wana Simba SC tulikupenda sana na hara Kukutetea ila Mafanikio yako ya Umaarufu na Vijisenti vimekufanya Uvimbe Kichwa na ujione uko juu ya Simba SC ukisahau kuwa ni Simba SC ndiyo imekujenga na kukukuza hadi hao Wanafiki na Marafiki zako wa Yanga SC Wanakupenda na Kukutumia Kuihujumu Simba SC.

Ushauri wangu mkubwa tu Kwako ni kwamba nyamaza, achana na Simba SC angalia Maisha yako mengine baada ya Simba SC.

Tena ikikupendeza zaidi bado hujachelewa Kiungwana kabisa unaweza ukatuomba Radhi ( Msamaha ) wana Simba SC, kiri Makosa yako nasi kwa Roho safi na mkunjufu tutakusamehe na hata Kukuombea Jukumu lingine ndani ya Simba SC ila siyo la kuwa Msemaji Wetu tena.

ANGALIZO

Wale ambao mtapenda kutumia hili andiko langu katika Blogs zenu, Redio na Magazeti tafadhali nawaruhusu mtumie ila tendeni Haki tu kwa kufanya Acknowledging au Source Crediting kwa kusema mmetoa hapa JamiiForums na Kwake GENTAMYCINE na siyo Mdanganye imetoka Ubongoni mwenu kwani mtanivunja moyo kuja na 'analysis' zangu zaidi huko mbeleni.

Cc: billduke
 
Mkuu nimekupata vizuri kwa andiko lako limejaa point tupu.

Ngoja tusubirie hiyo jumatatu tuone kama atasema.
 
Back
Top Bottom