Iwe ni Mind game au iwe ni uhalisia, mimi nazungumza kama mdau wa michezo.
- Ukimsikiliza Haji kwenye audio inayozunguka mitandaoni, Moja ya malalamiko yake ni kwamba anashutumiwa kuihujumu Simba kutokana na ukaribu uliopo baina yake na uongozi wa GSM.
- Kama hoja ni hiyo, sioni kosa la Babra kumuita Manara na kumuuliza.
Leo hii wanayanga wanamshutumu mwenyekiti wa klabu ya Yanga kisa anafanya Kazi kwa Mohamed Dewji.
- Lakini pia kuelekea kwenye hizi mechi za watani wa jadi, kiongozi wa timu fulani kuwa karibu na viongozi au wadhamini wa timu nyingine, kiuhalisia inaondoa uaminifu KWA mashabiki na wanachama.
- Tukumbuke kuwa Haji huyu huyu aliwahi kumshutumu aliyewahi kuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kisa kukutana na Ibenge aliyekuwa kocha wa AS Vital KWA kile alichokisema anataka kuihujumu Simba. Alikwenda mbali mpaka akasema kuwa kama Simba itafungwa basi Zahera atakiona.
Alisahau kuwa Zahera alikuwa kocha msaidizi wa Ibenge kwenye majukumu ya National team.
- Hakuishia hapo Haji. Bado alikuja kumshutumu Senzo, kisa kukutana na kocha wa Al Ahly ya misri, KWA kile alichodai Senzo anataka kuihujumu Simba.
Alifikia hatua ya kumtisha Senzo mpaka juu ya uraia wake.
- Sasa ajabu ni nini yeye kushutumiwa juu ya hujuma za kuihujumu Simba?
- Ukichunguza Sana unagundua kuwa huu Ujinga waliufuga Simba wenyewe. Mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba walimwamini Haji mpaka wakashindwa kumtofautisha Haji Manara na Afisa Habari wa Simba.
- Mashabiki na wanachama hawa ilifikia hatua hata ishu personal za Haji walizibeba kama ishu za Simba sc.
Na hapa ndipo Haji alipoanza kuota mapembe na kujiona yeye yupo sahihi kwa kila atakachokizungumza. Alijiona kuwa neno lake laweza kuwa sheria.
Haji alikuwa anaweza kuanzisha vita ya maneno na mtu, anapoona anakosa hoja anarudi kwa mashabiki na wanachama wa Simba kwa kisingizio cha kuitetea Simba. Na mashabiki nao bila kufikiri wanaingia mkumbo huo huo na kuwatukana watu hovyo.
Leo hii baada ya kuwachafua waliopo nnje ya Simba sasa anawachafua waliopo ndani ya Simba.
Akimaliza na Bara anakuja na Mo, na hapo ndipo mtakapokuja kujua ule msemo wa "MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO" AND "WHAT GO AROUND, COMES AROUND"