Mkataba huo wa milioni 4 ungempunguzia sana mapato kwa kumfanya asiendelee kufanya kazi kwa makampuni kama Azam, Gsm, Asas, Maji ya uhai, n.k
Manara walitaka kumpa mkataba wa kizamani na hovyo kabisa, yani hata account ya instagram ya manara ingekuwa chini ya klabu, kwa umaarufu wa Manara na watu wanavyomfatilia wangeigeuza account kuwa sehemu ya kutangaza bure bidhaa za Mo ama ndugu zake huku wakikataa kutangaza makampuni mengine kama azam, gsm, n.k
Mkataba pia ungemfunga manara kutoweza kusaini dili lolote nje ya usemaji wa club simba, yani huu mkataba ungemfanya awe na jukumu moja tu la kuwa msemaji wa simba na kuacha kuwa balozi au msemaji wa makampuni mengine, hayo madili hadi aingie ingekuwa mpaka apate ruksa kutoka kwa ceo ambae ni babra na pesa anayolipwa inaenda kwenye mapato ya klabu huku yeye akilipwa mshahara pekee.
Huu mkataba ni wa kizamani sana na umekaa kufungiana ridhiki tu, kwa wenzetu huko nje mtu anaweza kufanya kazi kampuni ya NIKE wakati mdhamini wa jezi ya timu anayofanyia kazi ni ADIDAS ambao ni wahasimu wakubwa wa Nike.
Tatizo wivu na roho za kwanini haji apate mafanikio nje ya kuisemea simba? Angalia mfano tu mdogo haji manara ana nyumba yake,magari yake, na mali nyingine, hii ni kutokana na mikataba minono kutoka kwa asas, gsm, azam, maji ya uhai, n.k ambao pasi na shaka wanamlipa vizuri, pengine hata ile faini ya milioni 5 aliyoenda kuilipa kwa cash ofisi za tff huenda alipewa na hayo makampuni mengine ili wamtunzie brand yake, mfano mwengine angalia siku ya harusi ya haji wale GSM walifanya kufuru kumtunza haji, hii kitu huenda ilikuwa inawaumiza sana wamiliki wa simba waliodhani walimkomesha kwa kumlipa laki 7.
Manara kaupiga mwingi hapa, kakataa kubanwa kweye mtego wa kuifanyia kazi simba pekee kitu ambacho kingemlazimu awe anatangaza bidhaa za MO pekee ama ndugu zake, Manara ana familia na inamtegemea kuna kipindi huenda atatoka simba na bado mke wake na wanae bado watabaki kumtegemea yeye, ni haki yake kutafuta michongo nje ya simba ili kuongeza kipato na kuweza kusimama hata pale akiacha kulipwa na simba.
HITIMISHO: Simba wakae upya, watatue hili jambo kwa njia za kidiplomasia na sio kukurupuka kumfukuza manara, nafasi ya kurekebisha kasoro za mkataba bado ipo, mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu mchungu, hao kina Mo na Babra nao wajiweke kwenye hali ya manara.