Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

Hebu muulize lengo lilikuwa ni nini kwa kusisitiza kwake hii hoja ya kupumzika. Alikuwa anataka habari hizi ziwafikie wakina nani walioko wapi?
Shehullohi,

Kuna neno au maneno "ujumbe umefika"
Dososoa tu 'habari ndio hiyo'
Hao watakaofikiwa na habari hiyo utawasikia nao
 
Nikifikiri kuweka mikono nyuma ni hulka yake tu.

..Warioba alishiriki kampeni za Ccm 2015 na 2020.

..alishuhudia kwa macho yake kampeni za matusi, ubaguzi, na ukabila, zilizokuwa zikifanywa na Ccm.

..angekuwa na msimamo wa dhati angejiweka mbali na Ccm, lakini yeye aliendelea kuwa nao karibu.

..hata sasa hivi ukimsikiliza Mzee Warioba hayuko tayari " kumvika paka kengele ,"na kueleza bayana unyama waliofanyiwa wapinzani.

..kwao Mzee Warioba, mkoa wa Mara, ni moja ya eneo ambako wapinzani wamefanyiwa mambo mabaya kupitiliza, lakini Mzee badala ya kuwatetea wananchi ananyenyekea na kuwasitiri watawala.
 
..Mzee Warioba hawezi kuwa na msaada wowote.

..Yule Mzee yuko soft sana, na akiona wakubwa ananyong'onyea kabisa.

..Hana kifua cha kuwaambia watawala ukweli mchungu.
Lakini nashindwa kabisa kuwaelewa baadhi ya hawa wazee, hasa huyu Waryoba.

Hivi woga ni wa kulinda maslahi yake au ya watoto wake?

Huyu mzee angeamua na kusimama (mithili ya Nyerere wakati ule baada ya kung'atuka); na kusimamia anayoyaamini bila kuyumba kabisa, angejijengea heshima kubwa sana kwenye taifa hili kuliko heshima aliyonayo kutokana na utumishi wake aliotumikia.

Kuna kitu gani zaidi katika umri wake ule zaidi ya Uzalendo kwa nchi yake tu basi!
Hata akitishiwa kufukuzwa ndani ya chama, hapo ndipo atazidi kuaminiwa zaidi na wananchi wanaotaka Katiba Mpya.

Sasa yeye sijui ni nini kinachomtisha zaidi. Bado anadhani atazabwa vibao kama vile alivyozabwa na Bashite wakati ule?
 
Waogope sana wenye hulka hizo. Wako kama Chatu, ngozi laini, wanang'ara Wakikamata wanakamua!

..angekuwa kijana sawa.

..lakini sio kwa umri wa Mzee Warioba.

..wanaodhani hakuna watu laini-laini toka mkoa wa Mara wamuangalie Mzee Warioba.
 
AhamduliLlah, corona ilinikwepa salama. Nilijificha nilikuwa na "heshima ya woga", bwana yule alifanya tujifiche tukitaka tusitake.
Na nyinyi tatizo lenu mmezidi kupiga ma deal hadi unaogopa kinvuli chako mwenyewe!? Achaneni na ma deal hata akija Rais kutoka aangani na bado mtaishi kwa amani bila ya uwoga!!
 
Lakini nashindwa kabisa kuwaelewa baadhi ya hawa wazee, hasa huyu Waryoba.
Usishindwe, jaribu kumwelewa alivyo. Ni nguli wa sheria na amebobeka huko. Isitoshe ni mwanasiasa anayejua kosoma nyakati.
Hivi woga ni wa kulinda maslahi yake au ya watoto wake?
Sidhani kama ni woga, kwani naamini hata woga ni ujasiri.
Maslahi ya watoto? ni Wakubwa au bado ni wadogo? sijui, kwani nnayemjua alipandishwa jukwani jimbo la kawe kama sikosei na huyu ni Kijana mkubwa tu Unamlinda vipi mwanasiasa mwenzako? sina jibu ila nafikiri hilo la mjadala mwingine.
Huyu mzee angeamua na kusimama (mithili ya Nyerere wakati ule baada ya kung'atuka); na kusimamia anayoyaamini bila kuyumba kabisa, angejijengea heshima kubwa sana kwenye taifa hili kuliko heshima aliyonayo kutokana na utumishi wake aliotumikia.
Ninachojua ni CCM haijakuwa bila ya 'power strugle' au vigenge genge Cleopa na genge lake nafikiri hawakuwa na nia ya muendelezo wa "Nyerereism" na hili ni mwono tu wa siasa za nyakati nafikiri wakina Salim A.S na Warioba alike waliona mikanganyo ndani yao yalikuwa hayana tija nje ya Siasa za Chamani hivyo wakajitunzia heshima zao kuepuka kuigaragaza CCM... kisiasa na hata kulinda heshima ya Chama na sio kibinafsi... ni mwono wangu wa wakati huo.
Kuna kitu gani zaidi katika umori wake ule zaidi ya Uzalendo kwa nchi yake tu basi!
Hata akitishiwa kufukuzwa ndani ya chama, hapo ndipo atazidi kuaminiwa zaidi na wananchi wanaotaka Katiba Mpya.

Sasa yeye sijui ni nini kinachomtisha zaidi. Bado anadhani atazabwa vibao kama vile alivyozabwa na Bashite wakati ule?
Hilo la Bashite, binafsi naona tu "Wenyewe"baada ya kuonja asali, nderemo za vyama vya upinzani wa kiaiasa ilibidi wazime Katiba and who had the guts? pamoja na Nguvu za "Wenyewe" You guessed right!! Kama alivyotumika Hayati JPM kupunguza nderemo za vyama vya upinzani kisiasa pamoja na ujangiri uliokithiri ndani mwao na kurudisha heshima kwenye Chama na Nchi Warioba ilikuwa vile kwenye Katiba.
"Wenyewe" watajijiju😁

Hivyo basi, sio woga, sio heshima kibinafsi, sio kulinda watoto-huu mjadala mwingine- bali Heshima ya nchi yake na heshima ya Chama. Kama nilivyosema juu, Ni nguli wa Siasa za nyakati. Strategic.
 
Na nyinyi tatizo lenu mmezidi kupiga ma deal hadi unaogopa kinvuli chako mwenyewe!? Achaneni na ma deal hata akija Rais kutoka aangani na bado mtaishi kwa amani bila ya uwoga!!
Anaitwa Foxy huyooo, angalia asikurarue
 
Watoto wa nyerere wangeishi maisha kama ya watoto wengine wa vigogo,wanaotaka kumchafua wangepata cha kusema.Nyerere ni very exceptional leader kuwahi kutokea na kumbukumbu hizi nzuri zinawakera wengi.
 
..huyu jamaa ni mlevi-mlevi tu anabugia mshahara kwa kodi za Watz kwasababu ni mtoto wa Nyerere.

..ndio maana KATIBA MPYA ni muhimu ili wananchi wasiendelee kubeba mizigo kama hii.
Lakini walevi ni watu peace sana, hawanaga shida na mtu.

Cha msingi kama mtu anatimiza majukumu yake basi swala la kupiga mtungi hilo ni lake binafsi.
 
Usishindwe, jaribu kumwelewa alivyo. Ni nguli wa sheria na amebobeka huko. Isitoshe ni mwanasiasa anayejua kosoma nyakati.

Sidhani kama ni woga, kwani naamini hata woga ni ujasiri.
Maslahi ya watoto? ni Wakubwa au bado ni wadogo? sijui, kwani nnayemjua alipandishwa jukwani jimbo la kawe kama sikosei na huyu ni Kijana mkubwa tu Unamlinda vipi mwanasiasa mwenzako? sina jibu ila nafikiri hilo la mjadala mwingine.

Ninachojua ni CCM haijakuwa bila ya 'power strugle' au vigenge genge Cleopa na genge lake nafikiri hawakuwa na nia ya muendelezo wa "Nyerereism" na hili ni mwono tu wa siasa za nyakati nafikiri wakina Salim A.S na Warioba alike waliona mikanganyo ndani yao yalikuwa hayana tija nje ya Siasa za Chamani hivyo wakajitunzia heshima zao kuepuka kuigaragaza CCM... kisiasa na hata kulinda heshima ya Chama na sio kibinafsi... ni mwono wangu wa wakati huo.

Hilo la Bashite, binafsi naona tu "Wenyewe"baada ya kuonja asali, nderemo za vyama vya upinzani wa kiaiasa ilibidi wazime Katiba and who had the guts? pamoja na Nguvu za "Wenyewe" You guessed right!! Kama alivyotumika Hayati JPM kupunguza nderemo za vyama vya upinzani kisiasa pamoja na ujangiri uliokithiri ndani mwao na kurudisha heshima kwenye Chama na Nchi Warioba ilikuwa vile kwenye Katiba.
"Wenyewe" watajijiju😁

Hivyo basi, sio woga, sio heshima kibinafsi, sio kulinda watoto-huu mjadala mwingine- bali Heshima ya nchi yake na heshima ya Chama. Kama nilivyosema juu, Ni nguli wa Siasa za nyakati. Strategic.

..kwa Mzee Warioba ni bora wananchi tuuwawe, tutekwe, tudhalilishwe, lakini serikali na watawala wasipoteze heshima yao.

Cc Kalamu1
 
Haaaa haaaa juzi mtoto wa ikulu mwenzake nilimsikia.akikemea ufisadi huko kwa lukuvi.watoto wa kishua hawapepesi macho siku hizi
 
Makongoro akiwa anapiga speech live on a national yelevision inahitaji ujasiri maana street language za kutosha
Jamaa kitaa sana na anaweza kutoa boko any moment
Kuna maneno kayasema ni deep street am sure hata rais hakuyaelewa...
The man is funny and free soul creature with a bottle of hennessee in his hand.
Eti hata Raisi hakuyaelewa. Hii lugha haijakaa vizuri na ni utovu wa adabu uelewe wewe pangu pakavu kisha asielewe Rais Pua pua pua kabisa
 
Makongoro alienda vita ya Uganda bila hata baba yake kujua, Makongoro alijiunga na upinzani NCCR na kupata Ubunge
Makongoro aliwahi kukataa ubunge wa kuteuliwa na Mkapa

Kama jina la Nyerere ndio linambeba mbona lisiwabebe hao watoto wengine wa Nyerere?

Siametupa dongo kwa wenzake akina marope Februari
 
Hivi ukiwa mtoto wa kiongozi Tanzania hufai kuwa kiongozi?... kwani utaratibu wa kuwa kiongozi Tanzania ukoje?...
 
Rais anapaswa kuchagua mtu yeyote mtanzania mwenye akili timamu na ambaye ni Mbunge katika Bunge la jamhuri ya muungano... maana yake uliwa mbunge na akili timamu unaweza kuwa Waziri...

Uzuri mwimgine kwa nchi yetu, huhitaji kuwa genius au na miakili miingi kuwa kiongozi, ni connection tu na influence yako tu mahala fulani fulani hili ni kwa wooote waliowahi kuwa mawaziri na viongozi hapa Tanzania..
 
Mzee wa shy isijeukawa hujaiona Asali. Ndio kujisogeza sogeza mbele ya nyuki! Ndio upate hiyo asali!
Wamezidi kufadhiliana wenyewe kwa wenyewe ambao tayari ni matajiri kwenye nchi hii kupitia wazee wao !! Hata Hao wafia chama wenyewe wamebaki kushangaa shangaa tu na kinachoendelea ndio maana wengine wameanza kutoa ya moyoni !!
 
Rais anapaswa kuchagua mtu yeyote mtanzania mwenye akili timamu na ambaye ni Mbunge katika Bunge la jamhuri ya muungano... maana yake uliwa mbunge na akili timamu unaweza kuwa Waziri...

Uzuri mwimgine kwa nchi yetu, huhitaji kuwa genius au na miakili miingi kuwa kiongozi, ni connection tu na influence yako tu mahala fulani fulani hili ni kwa wooote waliowahi kuwa mawaziri na viongozi
Hivi ukiwa mtoto wa kiongozi Tanzania hufai kuwa kiongozi?... kwani utaratibu wa kuwa kiongozi Tanzania ukoje?...
Unajitoa ufahamu kisha unajiweka sawa mwenyewe safi.
 
Back
Top Bottom