Hatimaye ndoa yangu imevunjika

Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
Anatafuta huruma uyo,
majanga kayaleta mwenyewe kwenye ndoa yake.

Afu hana heshima kwa watu ndio maana yanapomkuta watu wanamgongea mkewe na shombo wanammwagia
 
Pole sana mkuu, magumu katika maisha yanatuimarisha, kama una elimu nzuri nenda offisi yoyote kaombe kufanya kama volunteer siku za usoni watakupa ajira nenda kwenye banks, usikae nyumbani tu ndiyo unaongeza tatizo
 
Lazimaaa. Halaf ni mtu mzima kabisa huyu[emoji23][emoji23]
Ila hapa munamsema na kumcheka katika umri ambao yeye pia alikua anayafanya haya. Fainali ndo imekuja vibaya hv. Na nyie mtakaangwa kwa mafuta hayahaya pia wakati ukifika
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]nishakaangwa nikatia akili, tukayajenga upya na ndoa sahv ina amani tele.

Mtoa mada arudishe majeshi nyuma, aombe msamaha wayajenge kwa mustakabali wa watoto.

Kumpata mwanamke wa kuanza nae moja, akakuelewa vwma kabisa kama yule wa mwanzo nao ni mtihani sana mkuu.
 

Mkuu kutafuta pesa sio jambo la kukumbushwa au la kuwekea kauli mbiu ni swala lipo utaishije bila pesa , na pia isiwe kutafuta pesa kwasababu ya mwanamke hapa ndiyo vijana wengi mnapokosea, utaratibu wa kutafuta pesa uwe tu katika utaratibu wako wa kuishi na sio vinginevyo au ziwe pesa za kuhonga wanawake vijana mnafeli sana,
 
Amen!
Bro huyu mwanamke kanizimisha ndoto zangu nyingi saana hususani za kielimu na biashara. Nashukuru Mungu am free now I can move on!
Na nitapata maendeleo kweli kweli

Ulianguka kwenye mapenzi zaidi ukajisahau, mwanamke anakukwamishaje kusoma kupata elimu au biashara, maana umesema chanzo cha ugomvi wenu ni swala la pesa sasa iweje ukaacha biashara ukakaa nyumbani, cha msingi anza upya usijejisahau tena, ndoa yako ulifungia RC!? kama ni RC hiyo ndoa haijafunjika
 

Tafuta hela na Omba Mungu! Inawezekana anguko lako la kifedha ni uchawi na ushurikina wake! Wanaume tuna hali ngumu sana bila kushika Imani!

Jitahidi sana kuwa mtu wa sala na kumfuata Mungu, otherwise utakuja kufa kwa mawazo na stress, Mungu na a kusaidia!

Mbili za huyo Mama Sio za Mda mrefu, atakuja tu kukwama, Hakuna namna! Usijali, watoto watakuwa tu, Mungu ndiyo hutupa riziki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…