Hii akiba ya fedha za kigeni dola Bilioni 6,253 aliyosema Rais Samia kiboko, deni la Taifa lingekuwa hela ya peremende

Kwenye ile speech yake (full text) hebu c&p text inayosema hivyo kama ilivyo.
 
Ni sahihi kwani dola bil 6250 unajua ni shilingi ngapi? Si ni til.14 na huo ndio ukweli..

Acha ujinga mtoa mada ,forex reserves haitumiki kulipa madeni bali kuagiza bidhaa za nje na ku stabilize currency.Tatizo lenu ni mbumbumbu wa uchumi..

Ni mara kadhaa kama huwa mnasoma na kusikiliza bajeti utasikia lugha hiyo ya milioni 3467 nk nk ..

Mpende kujifunza sio kujaza ujinga vichwani
 
Akili za Watawala zimewekezwa kukimbizana na wapinzani tu, basi.
 
Jana tu nilisema aache kusoma hotuba ,,Taifa linaserereka kama gari bovu
 
Kwa hakika kuna watendaji mizigo huko serikalini; ugomvi mkubwa unaoendelea nchini hivi sasa tena baina ya mihimili ya kiutawala ni deni la taifa; Rais vs Speaker.

How comes wanakosa umakini kwenye jambo nyeti kama hili la akiba ya fedha za kigeni kwenye speech muhimu kwa wakati muhimu na msomaji muhimu hivi? Tunadanganywa mangapi kwa uzembe kama huu?
 
Naona umeamua kumlisha maneno mama samia.
 
Mwandishi atakuwa Francophone. Wafaransa ndio wanatumia koma kwenye nukta. Yaani kwa Kifaransa bilioni 6,253 = bilioni 6.253. Lakini kusema ukweli Ikulu yetu ni jumba bovu. Nyaraka za Ikulu km vile press release za uteuzi zimejaa typos!!
Speech imeandikwa kwa Kiswahili wala sio kwa Kifaransa. Speech ya juu kabisa katika nchi ni speech ya Rais; haitakiwi kuwa na makandokando ya aina yoyote!

Inatakiwa inyooke kama rula in all aspects; in short ni final. Haitakiwi aje sijui nani baadaye kurekebisha speech ya Rais ikishaenda hewani. Baada ya hapo ni wananchi kutoa maoni yao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…