Hii nguvu si mchezo: Kitenge, Zembwela na Hando wapewa escort ya ving'ora Dubai

Sijui ni nini kifanyike. Lakini Picha hii hapa. Hawa watu wameenda Dubai kula maisha na Wakarudi hapa kuja kupigia chapuo DP world. Hii ni hujuma zidi ya Watanzania.


View attachment 2666193
Mimi naendelea kuwapa hongera Kitenge na Zembwela kwa kufanikiwa KIUJANJAUJANJA bila Shule(formal education).
 
Hoja yake haina mashiko ila mtazamo wake ni kwamba maswahiba wananyanyaswa
 
wivu unakusumbua. na hili taifa halitoendelea watanzania tuna wivu sana na kulogana.
Wivu gani? Sasa hapo. kuwa naona wivu kuhusu mtu kumiminiwa maziwa ama wivu kuongea ukweli? hawa wote ni wajinga ama kuona wivu upi.
 
Pia hao kina Kitenge na Zembwela kwenye hilo suala la DP world tuwasamehe tu maana wao kwenye huo mkataba ni kama ilivyokuwa kwa Feisal na Yanga. Yaani wanachokielewa ni kile wanachoambiwa kwa mdomo lakini hawajui kilichoandikwa.
 
Waendee tu kuhangaika na waarabu verisuni watainamishwa.
Waarabu hawajawahi kuwa na urafiki wa maana na mtu mwenye ngozi nyeusi.
 
Hao kina Kitenge, Zembwela, na Hando ni wasaliti wa Tanganyika yetu.

Usishangae hao jamaa wakijiachia, bahasha zimeshatembea kwao, kama zilivyotembea kwa wabunge.
Hao watu kule hawajijipeka wenyewe.

Wamepewa Pochi Nene kutetea huo umangungo.

Mambo yakusikitisha

Ole wao ije siku mambo yakabumbuluka

Tatizo hii nchi hakuja street justice vingine Hawa watu saivi wangebaki huko huko.

Shwaini wanatetea mkataba wa kinyonyaji wa nchi yao.

Aisee
 
Unauliza nani anayefadhili!! Jibu mbona kila mmoja analijua. Hiyo ni package ya rushwa iliyokamilika.

Na ole wao DP wasipofanikuwa kuzipora bandari zote za Tanganyika. Mwarabu hawezi kuwaacha hivi hivi tu.
 
Kwa upeo mdogo wa Kitenge, sidhani kama hata anaelewa, tatizo liko wapi.
 
Manunuzi ya umma ikiwemo kutoa tender hayatakiwi kushawishiwa kwa namna yoyote ile, hii ya watu kuendelea kulamba asali kwa kigezo cha kuwa chawa wa kampuni inayoomba tender nchini tayari inakiuka sheria ya manunuzi ya umma.

Kimsingi DP world amekuwa disqualified na sheria ya manunuzi ya umma kuendelea na mchakato wa kuomba tender ya kuendesha bandari kwani kahusika kutoa ushawishi kwa wanasiasa na wanahabari ili apewe hiyo tender.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…