Hii nguvu si mchezo: Kitenge, Zembwela na Hando wapewa escort ya ving'ora Dubai

Acheni Kitenge na wenzake wajipigie hela. Hakuna sheria ya nchi waliyovunja. Ninyi CHADEMA mkishika dola mtaweza kufuata utawala wa kisheria? Au mtaiweka katiba kando? Sababu mnakosa kabisa uvumilivu kwa watu walio na mtazamo tofauti na wenu.
 
mnatushosha bwana. kila mara nikeleleza dp dp. kuandamana hamtokei
Mpaka mambo yake sawa. Wewe unadhani katuni ya Kipanya inaonekanaje machoni mwako. Msisitizo"....unadhani....inaonekanaje machoni mwako..."
 
Inatakiwa orodha ijulikane ya wale wote ambao wanaonekana Wana Nia ya kuboresha "stomach infrastructure" zao badala ya kuboresha maslahi ya Taifa!!!

Lengo tujue tunaanzia wapi kuweka mambo sawa. Asante
 
Inavyoelekea wananchi hawakatai uwekezaji,bali ni jinsi mkataba ulivyo,na jinsi ulivyowakilishwa bungeni.Mama yapasa afanye maamuzi magumu kulingana na heshima aliyoijenga kwa jamii
 
Watu mliozoea kula bila kunawa wa GSM mna wakati mgumu sana miezi michache ijayo. Hamuwezi nyinyi wachache mkaendelea kuidhulumu nchi yenye watu milioni 62 eti mpaka mfe, nyinyi mmekuwa kina nani?.

DPW anakwenda kufunga mitambo yake bandarini na haya magumashi yenu ndio yanafikia mwisho. Nchi hii imedhulumiwa vya kutosha.
 
Hao kina Kitenge, Zembwela, na Hando ni wasaliti wa Tanganyika yetu.

Usishangae hao jamaa wakijiachia, bahasha zimeshatembea kwao, kama zilivyotembea kwa wabunge.
Wanachopewa ni kidogo kulinganisha na kuwaachia bandari wapiga wasiolipa kodi hata senti moja.
 
Watanganyika tumepigwa. Tudai mali yetu kuuzwa. Kwanin wangngania si waache wafanye mambo mengine.
 
CHADEMA mkipata madaraka mtaweza kuwa na utawala wa kufuata sheria (rule of law)? Kwa sababu mtu akiwa na mtazamo tofauti na wenu mnamponda, kumtukana na kumwita majina yote mabaya. Maulid Kitenge na wenzake hawajavunja sheria yoyote ya nchi ila wewe tayari umeshawahukumu. Mtaweza kuheshimu ibara ya 18 ya katiba inayotoa uhuru wa watu kutoa maoni? BADILIKENI.
 
Hauna akili.
 
Nakumbuka kuna Mtangazaji mmoja wa Kenya Yule jamaa alikuw nondo WA kuchimbua taarfa kwa umakin na anakuja na nakala yake iliyokamilika YENYE uzani Sawa wa TAARIFA .


Taifa Leo linashda sana katik Tanssinia ya habari wakat wao ni sehemu muhimu kuto lalia upande wowote na kuielemisha jamii si kimehemko kiusahihi na ufasaha katk mambo ya kimsingi YENYE hatma na Taifa letu.


Sasahao unaona tuu uendaji wao tayar niwakikampend hakuna hata muandsh hapo alisoma mkataba na kuamka na nondo za maswali za kuwaaliza Zaid tuu yakuomba mualiko ili wasikile side B [emoji16] (sifa njema Tuu)


Sis waTz ni shidaaa aseee[emoji243][emoji243]
 
Hata kipindi kile Cha biashara ya utumwa na ukwapuaji wa rasilimali za Africa...
Wakoloni waliwatumia Ndugu zetu kuwa kamata ndugu zetu!
Hali ni ile ile!
 
Mkuu,

Habari,tumepotezana muda Sana. Uko poa?
Mkuu nitakuwaje poa na tunauzwa?

Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.

Zaburi 137:3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…