Hii nguvu si mchezo: Kitenge, Zembwela na Hando wapewa escort ya ving'ora Dubai

Hii nguvu si mchezo: Kitenge, Zembwela na Hando wapewa escort ya ving'ora Dubai

Mkiambiwa mtokee barabarani kwa maandamano mnajificha chini ya uvungu wa kitanda. Lakini kwenye mtandao mnapIga kelele nyingi.😂
 
Mkuu nitakuwaje poa na tunauzwa?

Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.

Zaburi 137:3
Akuuze nani mkuu?. Panua uelewa wako ili uondokane na hayo mawazo hasi yaliyopandikizwa kichwani mwako.
 
Hata kipindi kile Cha biashara ya utumwa na ukwapuaji wa rasilimali za Africa...
Wakoloni waliwatumia Ndugu zetu kuwa kamata ndugu zetu!
Hali ni ile ile!
Wasiuzwe Rwanda waliojenga dry port kwa ajili ya biashara hii ya DPW.

Wasiuzwe Uingereza wenye bandari mbili zinazomilikiwa na DPW.

Wasiuzwe USA wenye bandarini nane zenye kusimamiwa na hawa jamaa, tuje tuuzwe sisi watanzania!.

Panua uelewa wako unaweza kuwa unaachwa mbali na dunia halisi inayokwenda kasi.
 
View attachment 2666300

Nani amefatilia Wasafi media leo asubuhi? Hawa watangazaji watatu tangu juzi wapo Dubai na wanajinasibu Kama ni wageni rasmi wa DP world kutoka Tanzania. Na wanapata escort ya ving'ora Kama wageni wa heshima.

Leo walikuwa wanawahoji watanzania ambao wanafanya kazi hapo bandari ya Dubai. Kiuhalisia wote waliohojiwa ni kutoka kwa ndugu zetu unguja na pemba (Zanzibar).

Mambo mengi mazuri Sana ya DP world yameongelewa,ikiwa pamoja na bandari kupokea meli 30 kwa wakati mmoja na kuhudumia meli sita zenye magari 3k kwa siku mbili tu. Mambo ni mengi.

Lakini Hawa jamaa ni wanajizima data au hawajui kilio Cha wanaowapinga hao DP world kuwa siyo ufanisi wao Bali ni MKATABA mbovu na wa kinyonyaji na wakivhief Mangungo baina yao na Tanzania?

Hata dada yetu wa Jf bi Faiza Fox nae aliandikw uzi wenye mtazamo huu huu wa kina Zembwela kuwa "DP world wapo hadi Uingereza iweje nyie walala hoi watanganyika mnawakataa". Akapigwa maswali haya haya,umeuona mkataba wa Uingereza? Au mkataba wa Uingereza na huu wa kwetu unafanana?

Alafu kingine; hivi ni nani amawafadhili Hawa jamaa watatu? Huko Dubai? Maana wanajimwayamwaya kama wafalme. Na Wana ego balaa,full kujisifu.

Hii nguvu ya DP world kwenye media za bongo siyo mchezo.

Lakini Hawajui kuwa ukimsisitiza Sana Mtu kuwa kitu chako ni ni kizuri ndivyo unavyomfanya astuke kwamba kwa nini jamaa ananilazimisha Sana nione hiki kitu chake kipo sawa? Jamaa wanafosi mpaka kila mtu Sasa anajua kwamba wanalazimisha!!

Hii tabia tunayo Sana sisi mawinga/ wazee wa kulenga hapa kariakoo. Nikiona hiki kiatu ni 'mdosho',nguvu ninayotumia kukuaminisha kwamba ni kiatu genuine ili uingie mkenge siyo ya nchi hii. Ukifungua wallet tu tukamalizana napita hivi,utajijua mbele ya safari. Ukikivaa ukapiga hatua zako 20,mguu unanyanyuka,soli inabaki chini.

Nikimwangalia Gerald Hando ni Kama Mtu mwenye kujistukia tofauti na wenzie. Hawa jamaa wawili wanaupepeta mdomo si mchezo. Hawana breki.
Njaa mbaya sana, angalia walivyokenua meno 😡 😡 😡
Hapo ukute wamekunja mamia ya mamilioni kutoka Dubai na Wizarani
Halafu kuna mtoto wa maskini analia njaa hapa bongo
 
Kwanza sikuhizi kufuatilia traditional media ni uzembe na kupitwa na wakati.
 
Kilichoifanya Dubai kuendelea kwa muda mfupi sii DP world Bali walifuta masheria ya kizamani ya Kodi na kujifanya FREE PORT.

Sisi bandari tunayo, maji yapo lakini kwa nini tusichukue maauzi magumu tuifanye BANDARI YETU FREE PORT?

Tusiwazi kuwa hayo ma Kodi ya kufanya bidhaa iwe mara mbili ndio yatakayoendeleza nchi. Ikiwa free port mizigo itakuja mingi, wageni watakuja wengi Tanzania kununua , mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa, fedha zitakuwa nyingi serikalini na kwa wananchi, kampuni za kisasa za wazalendo za kupakua mizigo zitaibuka. Haya mengine ni mapropaganda ya kizamani kuamini kuwa hao Jamaa Wana ushawishi wowote kwa mtu mwenye akili timamu
Wanauza nchi yao kwa waarabu kwa tamaa ya vipande vya fedha
 
Kwa mtazamo wa DPW kualika vyombo vya habari ni kukuza public awareness wa shughuli zao.

Uone wanachofanya kwa maelezo yao kupitia media na sio kusikiliza unachoambiwa na wengine, wanaita above the line promotion.

Same lobbying ya kualika wabunge, watu kutoka serikani lengo ni waone shughuli zao ni ‘below the line promotion’ ili wapate uelewa wa kutosha kwenye kuwahakikishia uwezo wao.

Kwa wabunge it’s morally wrong ingekuwa wanafanya kwa siri hiyo unaweza tafsiri kama hongo, lakini iwapo mwaliko umepitia njia halali za bunge hakuna tatizo.

Uwezi kwenda kufanya biashara sehemu ambayo watu awakuelewi; wenyeji watakuwa na mtazamo hasi na wewe. Ni jukumu lako kutoa elimu ya shughuli zako na uwezo wako ili ueleweke, na ndio wanachokifanya hao DPW
 
Nchi kuwasikiliza hawa jamaa kama Jounalist /Political analyst ni janga lingine kubwa, sioni jipya hapo zaidi ya kubwabwaja kishabiki.
 
Watu mliozoea kula bila kunawa wa GSM mna wakati mgumu sana miezi michache ijayo. Hamuwezi nyinyi wachache mkaendelea kuidhulumu nchi yenye watu milioni 62 eti mpaka mfe, nyinyi mmekuwa kina nani?.

DPW anakwenda kufunga mitambo yake bandarini na haya magumashi yenu ndio yanafikia mwisho. Nchi hii imedhulumiwa vya kutosha.
ILA WATU WA BANDARI NI WEZI

ova
 
Wasiuzwe Rwanda waliojenga dry port kwa ajili ya biashara hii ya DPW.

Wasiuzwe Uingereza wenye bandari mbili zinazomilikiwa na DPW.

Wasiuzwe USA wenye bandarini nane zenye kusimamiwa na hawa jamaa, tuje tuuzwe sisi watanzania!.

Panua uelewa wako unaweza kuwa unaachwa mbali na dunia halisi inayokwenda kasi.
Kuna kundi kubwa pale bandarini

Miaka nenda rudi wamekuwa wakinufaika na upigaji,uwizi pale
Hao sahv wana pressure si ndogo

Ova
 
Nchi kuwasikiliza hawa jamaa kama Jounalist /Political analyst ni janga lingine kubwa, sioni jipya hapo zaidi ya kubwabwaja kishabiki.
Hao jamaa hawana cha maana walichokifanya kukaa kwao Dubai, walitakiwa waongelee MKATABA wa pande zote mbili na sio ufanisi wa DP HII NDIO SHIDA YA KUPELEKA MAMBUMBU wasiojua sheria na MKATABA ya kimataifa sehemu noetic wamenisikitisha sana
 
Back
Top Bottom