Hili suala la wanafunzi kubaki shule lina umuhimu mkubwa kwa maisha ya baadaye ya mtoto wako

Hili suala la wanafunzi kubaki shule lina umuhimu mkubwa kwa maisha ya baadaye ya mtoto wako

Mtoto Darasa la saba miaka 13 au 14 unamsomesha mwaka mzima bila kupumzika shule gani hiyo?? Shule zinatafuta jinsi ya kuongeza mapato zaidi. Kuna shida gani Mtoto kumpumzika na Wazazi hata siku 20?
Kuna wajinga humu hawatakuelewa yaani wanacho penda ni watoto wabaki shuleni wasiwaletee kero majumbani. Mtoto form two anabakia kusoma nini kama sio ujinga?
 
Ushawishi wa ovyo kabisa.
Watoto wanapaswa kupumzika.
Ila sema wazazi wa sasa wameshindwa kabisa kuishi/kuwalea watoto wao. Wanawakwepa mnooo
Na hapo ndio point ilipo wanataka Uhuru ndio maana mtoto akamaliza Shule utasikia Pre form 1 au Pre Form five, likizo Tuition yaani wazazi wanakwepa majukumu balaa hawataki kukaa na watoto wao hawa wawape elimu ya Duniani,
 
alikwambia huko shule wanasoma masaa 24 nani?
Walio panga likizo unazani walikuwa wajinga? Shule za maana kwa sasa watoto wao wako Vacation huko wana badili mazingira, wajinga humu wanaona mtoto kuishi shule ndio maisha, Mtoto apumzike ajifunze vitu nje ya shuleni
 
Mazingira ya wanafunzi katika shule za sekondari za kata mhe waziri na kamishina wa elimu wanayajua? Je watoto wao wamewahi kusomea hizi shule?.Kuna shule hazina walimu totally wa masomo ya sayansi wanapokuwa form one.Mkuu wa shule anatafuta mwl wa kujitolea walao wanapokuwa madarasa ya mitihani.Wakati wa likizo anaona ni muda wa kufidishia magepu bahati mbaya kabisa anakuja mtu kutoa tamko wasisome watoto wa wakulima huko kijijini .Bahati mbaya kabisa walimu wamejitoa wawafundishe watoto bure.Maoni yangu walimu watulie na kurelax kwani hakuna mwl anaweza kufukuzwa kazi kwa wanafunzi kufeli mtihani.
 
Mtoto Darasa la saba miaka 13 au 14 unamsomesha mwaka mzima bila kupumzika shule gani hiyo?? Shule zinatafuta jinsi ya kuongeza mapato zaidi. Kuna shida gani Mtoto kumpumzika na Wazazi hata siku 20?
Mwanangu alikuja juzi yuko la 6.. akaniambia Baba tummeambiwa tupeleke elfu thelathini za kusoma wakati wa likizo..

Nikamwambia hao walimu ni wapumbavu..

Ikaisha.
 
Umetawaliwa na limtaala libovu la kikoloni.. linawaza mitihani tu...

Hovyo kabisa..

Limtaala hili libadilishwe mapema.

Mi natamani hata wanangu wasije fanya mimitihani hii ya NECTA..
Wewe umeona tatizo kwa ukubwa wake ! Tatizo ni mtaala
 
Kila mtu ashinde mechi zake............ Mtihani wa mwisho kuna mtu atajua hajui. Ndio itafahamika likizo ni nzuri au sio nzuri.
Akisha faulu next? Sikilizs ngoja nikuambia Zama za kuabudu A au Divi 1 zisha isha, hii coment kuna siku utaielewa
 
Ukiacha mtoto wako apumzike,wenzio wanamsomesha tuone ipi bora.Mimi naingia form one baada ya kumaliza la Saba wenzangu wanasolve simultaneously equations,Kila mtu apambanie wanawe.Tangu lini serikali ikawa na huruma Kwa wananchi?Ingekuwa na huruma ingefuta tozo na Kodi ya jengo Kupitia luku.
 
Jumatatu serikali na bunge kutoa tamko na maazimio
 
Mazingira ya wanafunzi katika shule za sekondari za kata mhe waziri na kamishina wa elimu wanayajua? Je watoto wao wamewahi kusomea hizi shule?.Kuna shule hazina walimu totally wa masomo ya sayansi wanapokuwa form one.Mkuu wa shule anatafuta mwl wa kujitolea walao wanapokuwa madarasa ya mitihani.Wakati wa likizo anaona ni muda wa kufidishia magepu bahati mbaya kabisa anakuja mtu kutoa tamko wasisome watoto wa wakulima huko kijijini .Bahati mbaya kabisa walimu wamejitoa wawafundishe watoto bure.Maoni yangu walimu watulie na kurelax kwani hakuna mwl anaweza kufukuzwa kazi kwa wanafunzi kufeli mtihani.
Hii ni sick and illest excuse..eti maxingira sijui walimu..

Acha kupotosha watu. Siku 194 za vipindi vya darasani hakuna topic inaacha guswa... Hakuna.. na kuna ample time ya revision ya kutosha. Hata huko vijijini.
 
Kwahiyo solution ya hayo ni kubaki shule...
Kama wote mnaotaka watoto wabaki shule kuepuka haya matatizo ni wazazi wa hovyoo everr..

Halafu huku shuleni tukibaki na hao watoto wenu mtatulipa!??
Mkibaki?? Anhaa kumbe wewe ni ticha.

Sio wazazi wanaotala watoto wabaki shule ni walimu kwa kiasi kikubwa ndio wanataka hilo.
 
Mtoto kurudi nyumbani ni muhimu zaidi ili akili ipate kutulia, sio kuwaza kitu kile kile Kila siku inabidi apate muda wa kurahia hata kama ni kucheza game lakini awe amepumzika, akirudi shule anarudi akiwa na hamu ya kusoma
 
Upon sahihi asilimia 💯 matamko ya kisiasa yanaharibu Sana eimu yetu na wamefeuka kuwa wazazi wakati sisi wazazi ndo tunataka watoto wetu wabaki shuleni kama kukaa nao tutakaa nao Sana wakimaliza.
 
Wazazi mnakwepa majukumu, mmewaachia walimu wawalelee watoto wenu. Iweje mtoto akae shuleni mwaka mzima bwana. Likizo ziheshimiwe watoto warudi nyumbani wawasaidie wazazi kazi na wajifunze taratibu nyingine za maisha ikiwemo kazi. Hizo Shule zenyewe watotni kusoma tuu, kufagia hawawezi, kuosha kikombe hawawezi. Kuna maisha nje ya kusoma, warudi nyumbani haraka, wazazi tutawasi amia wajisomee.
Nashangaa sana Mkuu. Wazazi hawataki kabisa kukaa na Watoto angalau hata mwezi!!!
 
Wazazi mwanao kama yupo form four, aendelee kusoma na kujisomea, haya matamko ya wanasiasa ni matamko ya kisiasa.

Wewe mwanao yupo shule ya kata, na unajua kuwa ili aweze kupata nafasi ya kwenda hata VETA au kuongeza ujuzi wowote basi cheti cha Form four lazima.

So akili kichwani, yaani mzazi unakaa na kusubiri future ya mwanao ambaye yupo shule ya kata iliandaliwe na waziri!

Mwanao akipata zero hata upolisi hawamchukui na huko mtaani ndio kizazi cha singeli hiki, pathetic.

Nimeandika maana nipo uswahilini De es Salaam, nimeona watoto wa kike na kiume wakikaa mtaani wanaishia kupoteza mwelekeo huku mtaani, hakuna mzazi makini wakumpa malezi bora mwanae.
Wamiliki wa shule mmeamua kuja na hii kampeni naona.

Zamani wakati tunasoma hizi hizi shule za st. Kayumba mbona hatukuwa tunabaki mashuleni na bado tulipata matokeo mazuri?

Ina maana ule muda wa watoto kukaa madarasani hautoshi wao ku cover sylabus?

Au watoto wa siku hizi wana vichwa vigumu kiasi kwamba hawahitaji likizo ili wafaulu?
 
Kusoma (learning) ni tofauti na kwenda/kukaa shule (schooling).

Muda wa mapumziko ni muhimu kama ilivyo muda wa schooling. Watoto wapumzike na kucheza.
 
Daah mambo yamebadilika sana. Enzi hizo miaka ya early 80's nikitoka shule Wazazi wananipokea kwa Bashasha Kijijini na Begi langu Kichwani. Halafu anatafutwa Kijana anakimbiza jogoo la Kienyeji kama mita 300 kabla hajamkamata kama kitoweo kwa Mtoto kurudi likizo. Eti tumekuwa Wazazi sasa hatutaki Watoto warudi likizoni. Msitulishe Ujinga huu.
 
Upon sahihi asilimia [emoji817] matamko ya kisiasa yanaharibu Sana eimu yetu na wamefeuka kuwa wazazi wakati sisi wazazi ndo tunataka watoto wetu wabaki shuleni kama kukaa nao tutakaa nao Sana wakimaliza.
Kwa nini hutaki Mtoto arudi likizo angalau upate naye mlo na kuwa na muda wa kumpa hata malezi nje ya shule??? Kiburi chenu cha fedha kitaharibu hata tabia za Watoto.
 
Sikubaliani na swala la kubakisha watoto shule kwa lengo la kutafuta ufaulu, wa Afrika embu tujue kuzingatia ratiba. Maisha ya mtaani ni muhimu mtoto ayafahamu na ajichanganye japo kwa mda mfupi wa likizo maana hao watu wa mtaani ndio atakao ishi nao mara baada ya kumaliza masomo.

Tusifikiri ya kuwa maisha ni kukariri makaratasi tu hawa wanafunzi kuna wengine watakuwa wafanyabiashara sasa atajifunza biashara wapi kama mda wa likizo mmewashikilia? Kuna wengine watakuwa wakulima atajifunza ukulima wapi kama mda wote mmemshikila? Je masoko na wateja atawatoa wapi kama hamtaki ajichanganye mtaani hata kwa mwezi mmoja?

Mimi ninachofahamu ni kuwa akili ikifanya jambo moja mda mrefu inachoka, na hata hao watototo ukiwabakisha shule kipindi cha likizo huku wakifahamu kuwa nilikizo wengi hawatasoma na kuelewa kitu kile watachofundishwa watahudhuria darasani kwa vile tu wanaogopa kuchapwa.

Kipindi cha likizo watoto hukitumia kutembelea ndugu zao kama shangazi, mjomba, baba wakubwa nk. Na hii huongeza mshikamano katika familia. Na waalimu pia mtumie muda huo kufanya kazi zenu za ziada na kutembelea ndugu na jamaa.

USHAURI WANGU KWA WALIMU.
1. Hakikishine mnamaliza syllabus kwa wakati.
2.Wakati wa likizo kila mwalimu wa somo hamkabidhi mwanafunzi mazoezi na maswali ya kutosha ambayo yatamlazimu mwanafunzi ayatafutie majibu na ayalete pindi shule ifunguliwapo tena ikiwezekana mzazi ajulishwe hilo, hii itamfanya mwanafunzi akatafute majibu kutoka kwa wenzake wa shule zingine hivyo atajifunza kitu kipya.

USHAURI WANGU KWA WAZAZI
1 Kipindi cha likizo tuwape watoto kazi nyingivsana za kufanya nyumbani, ikiwemo kupika, kufua, kuosha vyombo, kulima, kufagia mabanda ya ya mifugo, kuchunga na kukamua maziwa, kulima na kupalilia, kuuza maduka yasiyo ya vilevi nk. Hapo mtoto atajikuta hana muda wa kucheza cheza atajikuta anarefresh ya shuleni kwa kufanya jambo jipya wakati huo anawaza kuna mazoezi kapewa shuleni. Wala usimzuie mtoto kuangalia tamthilia wewe hakikisha majukumu uliyempa kayamaliza. Wala usimuingilie mambo yake ya shule maana kule atapewa mkong'oto asipofanya, wewe mpe kazi utamsikia anasema nina mazoezi nilipewa shuleni nifanye mwambie apangilie muda wake vizuri. Mtoto wa namna hii lazima awe active shuleni na nyumbani. Tusitengeneze vizazi vya makaratasi halafu akikosa ajira anazurura mtaani na hajui pakuanzia. Biashara hajui, ujasiriamali hajui, kilimo hajui, kupika hajui, kufua hajui, kufagia mabanda ya mifugo anaogopa kuchafuka, anaishia kukumbilia mjini na kujiunga na biashara haramu za kike au za kiume.
 
Back
Top Bottom